Mapendekezo: Serikali ianzishe wiki ya Dar es Salam

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,502
2,046
Kutokana na ukubwa wa uchumi mkoa wa Dar es salam na umuhimu wa mkoa huu kwa uchumi wa taifa letu, napendekeza Serikali ianzishe wiki maalum na kuutangaza mkoa huu kitaifa na kimataifa.

Katika wiki hilo kuwe na vipindi na matukio mbalimbali yanayoielezea Dar es salam kinagaubaga vipindi hivyo na matukio virushwe kitaifa na kimataifa.

Aidha ikibidi serikali ianzishe wizara maalum kwa ajili ya dar.

Nina hakika haya yanaweza kukuza uchumi wa dar kwa kasi sana kuliko ilivyo sasa!
 
Hatujastaarabika vya kutosha kuitangaza Dar kimataifa. Ngoja kwanza tumalizane na kuwaondoa wamachinga na vibanda vyao kwenye maeneo yote wasiyostahili kuwepo, kufunika mitaro ya majitaka, kuondoa bodaboda wote wahuni barabarani, kujenga masoko ya kisasa ya vyakula sehemu mbalimbali, kumaliza matatizo ya kudumu ya maji na umeme na kuboresha miundombinu mingine kama barabara.

Baada ya hapo ndiyo tuzungumzie kuitangaza Dar es Salaam.

Bila hivyo tujiandae kutangaza aibu tu.
 
Dar bila watu ni magofu tu na hao watu waliopo dar karibia asilimia 80 wanatoka mikoa mingine

Naona hii tabia ya mtindo wa watu kuanza kusifia mikoa wanapoishi, wanahisi ni ufahari wakati ni upumbavu tu usio na maana
 
Back
Top Bottom