Mapendekezo mapya kwa Dar kupambana na Korona

ngusillo

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
1,064
2,014
Naandika uzi huu, nikiwa najua kuwa kuna hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika ngazi mbalimbali kuanzia mitaa mpaka taifa.

Mapendekezo yangu yanalenda baadhi ya maeneo ya mkoa wa Dar es Salaam.
Maeneo hayo ni yale yanayopokea watu wengi hasa mjini na Kariakoo, business areas.

Napendekeza yaainishwe maadhi ya maeneo yanayosababisha wasafiri wengi kuwepo barabarani kama posta, kariakoo, maeneo maarufu yenye misongamano kama manzese, buguruni, gongolamboto, baadhi ya sehemu za sinza, baadhi ya mahoteli nk.

Maeneo hayo kuainishwe aina za biashara zitakazoruhusiwa kuendelea, zipewe kipaumbele zile zinazohakikisha uhai wa binadamu kwanza. Zile nyingine tulizozoea kama electronics, nguo, entertainment, nk zipewe muda wa wiki kadhaa za likizo.

Ikiwezekana waathirika kama waajiriwa waandikishwe kisha wapewe mafao maalum kwa kukaa nyumbani bila kwenda kutafuta kipato.

Maeneo hayo yaruhusiwe kuendelea na biashara za lazima kwa uhai wa binadamu, mfano maduka ya vyakula, masoko ya nafaka, huduma za madawa, vifaa na madawa ya mifugo na kilimo, nk viendelee.

Hii itasaidia kupungua kwa idadi kubwa ya watu wanaoelekea huko kununua bidhaa za kusafirisha kupeleka maeneo mengine hivyo kusababisha msongamano unaoweza kuhatarisha maisha nyakati hizi za Korona.

Pendekezo la pili ni kufanyika sensa maalum inayoweza kusimamiwa na mamlaka za serikali za mitaa kuanzia ngazi ya mtaa. Hii sensa iorodheshe makazi ya mtu alipo sasa, biashara anayofanya, ruti yake ya safari za kila siku, mawasiliano ya uhakika ya simu nk. Fomu maalum zitolewe kwa kila familia, zijazwe kisha zihifadhiwe na mamlaka husika.

Hili pendekezo la pili litasaidia mamlaka za wizara ya afya itakapolazimila kumpata mtu anayehisiwa kuwa na maambukizi. Pia itarahisisha kufuatilia muenendo mzima wa jamii hasa nyakati hizi ngumu kwa jamii.

Ni maoni yangu binafsi. Japo kunaweza kuwa na ugumu wa kuyatekeleza kama yalivyo, yanaweza kuboreshwa na kutekelezwa kwa namna nyingine inayofaa.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom