Uchaguzi 2020 Mapendekezo, maoni, ushauri kwa CC ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu hususani Jimbo la Kigamboni

omtiti

JF-Expert Member
Jun 19, 2019
655
1,000
Kama mwana ccm mkereketwa naomba uongozi wa juu hasa kamati kuu ya ccm, ambayo itahusika na uchujaji wa majina ya wagombea watakao peperusha bendera ya ccm kwenye uchaguzi mkuu October mwaka huu kwa nafasi ya ubunge jimbo la Kigamboni yafuatayo

Nashauri na kupendekeza Jina la Makonda ndio lirudi na lipeperushe bendera ya ccm jimbo la kigamboni, ni kijana ambae anaijua vizuri Dar, fitina zote anazijua, pia anaimudu vizuri kasi na maelekezo ya Rais Magufuli, hii itakua ni chachu nzuri kwa utawala huu ikiwa Makonda atapata uteuzi kwa nafasi ya uwaziri, sipati picha huku Makonda kule Alexander Mnyeti, Jaffo, Kigwa, Bashe, Bashungwa mchakamcha wa hatari. Hakuna kulala, vijana wana ndoto na matamanio ya utumishi uliotukuka.

Baraza la mawaziri lijalo linahitaji vijana zaidi kukimbiza, isipokua kwa nafasi ya waziri mkuu, waziri wa fedha, waziri wa mambo ya nje na waziri wa sheria wawe watu wazima kutokana na unyeti wa wizara hizo.

Ndugulile ateuliwe kuwa balozi nchi yoyote huko Ulaya, na aachwe kipindi chote cha miaka mitano, asitumbuliwe, cha msingi atimize majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu.

Ni maoni yangu tu, si lazima kuyazingatia
 

t2t

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
343
500
Hakushindwa ule ni mchakato wa mwanzo kabisa kuelekea teuzi na alishika nafasi pili,bado nae ni mshindi kwenye tatu bora
Na hapo ndipo mchakato mzima wa kura za maoni unapo kuwa hauna maana. Sasa Kama maoni ya wengi yanaonesha wanamkubali zaidi mgombea fulani, kwa nini apitishwe ambaye hakubaliki na wengi? Kamati zilitakiwa ziangalie kama mchakato ulifuata taratibu walizo jiwekea mfano kuhakikisha mgombea hakupita kwa kutoa rushwa. Siyo kukataa chaguo la wengi kutokana na mtu mmoja kuamka vibaya siku hiyo.
 

NJOLO

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
568
1,000
Ndugulile iatakuwa halali kuhamia upinzani na atakuwa na uhakika wa kushinda.

Dusiue Demokrasia kwa kukataa maoni ya wanainchi ambao walifanya uamuzi bila kuhongwa.

Historia itatuhukumu.

Makonda ni bora apewe ubalozi kwa sababu wanainchi hawampendi pamoja na kuwa ni mchapakazi.

Yesu kristo hakupendwa na watawala baada tu ya kuzaliwa hadi alipokua na watawala wakamuua.

Jina la Yesu ni jina kuu baada ya jina la mwenyezi Mungu.
 

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,000
2,000
Nashauri na kupendekeza Jina la Makonda ndio lirudi na lipeperushe bendera ya ccm jimbo la kigamboni,ni kijana ambae anaijua vizuri Dar,fitina zote anazijua ,pia anaimudu vizuri kasi na maelekezo ya rais Magufuli
Mukiandika mrudie kusoma kabla hamjapost. Huyu alikaidi maelekezo ya JPM, labda kama JPM ana utani na sisi ndio jina lirudi vinginevyo ................ndio kajichinja.
 

Shehullohi

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
1,433
2,000
Kuhusu kura za maoni Kigamboni Kamati kuu CCM wanatakiwa imbue coded msg ya matokeo yale. Macho yao yaangalie mbali zaidi ya usawa wa pua. Waanzie usawa wa pua na kuendelea mbele zaidi ikiwezekana wapite kwenye vijiwe vya gahawa, bao ,migundi ya bodaboda mbalimbali, matokeo ya uchaguzi 2020 yako tayari mbona.
 

omtiti

JF-Expert Member
Jun 19, 2019
655
1,000
Ndugulile iatakuwa halali kuhamia upinzani na atakuwa na uhakika wa kushinda.
Dusiue Demokrasia kwa kukataa maoni ya wanainchi ambao walifanya uamuzi bila kuhongwa.
Historia itatuhukumu.
Makonda ni bora apewe ubalozi kwa sababu wanainchi hawampendi pamoja na kuwa ni mchapakazi.
Yesu kristo hakupendwa na watawala baada tu ya kuzaliwa hadi alipokua na watawala wakamuua.
Jina la Yesu ni jina kuu baada ya jina la mwenyezi Mungu.
Una uhakika?,au imani yako
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom