Mapendekezo: Magufuli awe Mwenyekiti, Makongoro Nyerere Katibu CCM

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,673
1,571
Napendekeza kwa spidi ya mh. Magufuli "the heavy weight" kama atakuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM, basi katibu wake awe Makongoro Nyerere "Mako".

Makongoro alionesha kuwa na moyo wa dhati katika kurekebidha mwenendo wa CCM wa;
Fitina
Majungu
Ubwanyenye na
Ufisadi ambao aliukemea ndani ya chama chake wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea ndani ya CCM.
 
Jamaa katulia kimyaa, inaonyesha ananidhamu ya hali ya juu sana huyu Mako.
 
Mkitaka kweli kukikarabati chama na kukirudisha kwa wakulima na wafanyakazi na kukiondoa toka kwa wauza unga basi mpeni uenyekiti PHILLIP MANGULLA!!! Huyu mzee ndio aliyewaokoa saa hizi ccm ingekuwa chama cha upinzani!! Sioni mantiki ya kumruka huyu na kumpa uenyekiti mtu mwingine kwani kwa sasa hamna mtu akijuae chama zaidi yake!!
 
Last edited:

Mkuu kwa taratibu za ccm mwenyekiti wake ni Raisi alieko madarakani au aliemaliza muda wake sasa unamanisha wafute utaratibu wa kofia mbili ili mangula akwae uenyekiti?Au ulimanisha apewe ukatibu?
 
huyu mzee huwa hatabiriki hata kidogo. maana unakumbuka alishawahi kuhama chama!!? sasa unaweza ukampa mtu huyu ukatibu wa chama alafu kesho ukamkuta yupo kwenye jukwaa la ACT wazalendo karudisha kadi ya ccm.
 
Ameshajirekebisha siku hizi ni ccm damu huyu bwana
 
huyu mzee huwa hatabiriki hata kidogo. maana unakumbuka alishawahi kuhama chama!!? sasa unaweza ukampa mtu huyu ukatibu wa chama alafu kesho ukamkuta yupo kwenye jukwaa la ACT wazalendo karudisha kadi ya ccm.

Acha fitina za ajabu wewe kwenye siasa hakuna kitu kama hicho mbona watu wanahama vyama na wanapewa Vyeo vikubwa au huoni?
 
Mako jamani watawezana kweli na pombe zake zile? Maana Mako ni mlevi . Watawezana na JPM na Mangula? Sidhani! Kwa sasa Katibu Mkuu wampe Nchimbi.....au Shigela arudi kwenye Chama! Naona anapwaya kwenye RC
 
Back
Top Bottom