Mapedeshee ndio wakina nani?

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,687
2,534
Kukubalika kwa muziki wa kikongo na wingi wa wanamuziki kutoka DRC wanaofanya kazi katika bendi za Tanzania kumeathiri hata lugha ya Kiswahili, kwani hata watanzania sasa wanalazimisha kuimba katika lafudhi ya kikongo ili kupata soko. Sio tu lafudhi hata baadhi ya maneno ya kikongo sasa yanatumika kama maneno ya Kiswahili au ya kawaida na yaliyokubalika na jamii.

Sina hakika kama huku ni kukua kwa lugha au la. Miongoni mwa maneno hayo ni hili PEDESHEE, PEDEGHEE, au predeshee ili mradi kila mtu analitamka kivyake na kwakuwa ni neno geni hakuna aliyetoka na kulidadavua nini hasa maana yake na linatamkajwe. Binafsi likitamkwa naelewa ni kama mtu mwenye fedha na cheo mara nyingi wanaolitamka kila mtu anatafsiri yake. Ni wakongo wa FM academia wametafsiri neno lingine lilozoeleka la Kitokololo ambao wamesema maana yake Kuku, ni wakati muafaka sasa kwa wajuzi kujitokeza na kutueleza maana ya maneno mbalimbali yanayojitokeza na kukubalika na jamii yetu kuliko kuwa na neno linalotumika hivi hivi tu.

Inawezekana hapa isiwe mahali pake, lakini naamini kwenye wengi apaharibiki neno na members wa jamiiforums hawawezi kukosa jibu katika hili. Katika tafiti ndogo niliyofanya niligundua neno PEDEGHEE/Pedeshee/Predezee ni PDG katika lafudhi ya kifaransa na kifupisho cha maneno President Director General na likiashiria mtu mwenye madaraka makubwa katika taasisi/kampuni na fedha. Kwa Kongo watu wanamna hii ndio wamekuwa sponsors wakubwa kwa wanamuziki na ndio maana wamekuwa wakitajwa na kutukuzwa na wanamuziki katika matamasha na nyimbo mbalimbali kwa muda mrefu.

Sina hakika kama maana hii ndio inayotumika hapa kwetu kwani bongo au pia ndio maana halisi ya neno lenyewe. Wasiwasi wangu ni kuna wauza unga, majambazi, mafisadi na misheni towns ndio mapedeshee wa bongo, madeshee kibao walitajwa katika list ya majambazi na wauza unga kama miaka miwili imepita hivi. Kulikubali neno isiwe pia ndio kigezo cha kusafisha watu na shughuli wazifanyazo hata kama si halali na wamuziki walijue hili na waungane nasi katika vita dhidi ya uovu na wasiwe wasafishaji na kuwapa watu umaarufu tu.

I am standing to be corrected na dhamira ni kujifunza zaidi. Nawasilisha
 
Pedeshee ni mtu mwenye faranka mingi...
Yaani mkwanja au kisu au ngawila au mapene au Pesa nyingi tunaweza kusema ni tajili.
 
Pedegee au vyovyot utakavyotamka....ni French for P.D.G.President, Directeur, Generale..ni vyeo..kwahiyo wanamuziki katika kukoleza muziki wao hutumia PDG kuwasifu baadhi ya watu hasa wahisani/wafadhili wao."Kuwatukuza" huku..huwavimbisha kichwa wahusika na kuwafanya kumwaga mahela jukwaani!Wajinga ndo waliwao!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom