Mapato ya vijiji/miji ya watani wetu Tanzania kwa mwaka mzima ni ya kushangaza kama si ya ajabu

mwaswast

JF-Expert Member
May 12, 2014
12,777
6,454
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Selemani Jafo, Leo Jiji i Dodoma amewasilisha Taarifa ya Ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri zote nchini ya mwaka 2017/2018. Jafo amesema umefika wakati sasa wa kubadilisha utaratibu wa kuainisha Halmashauri zilizofanya vizuri nchini kwenye ukusanyaji wa mapato kama ambavyo inafanyika kwenye matokeo ya mitihani ya NECTA.

Jafo alisema kuwa, baada ya Bank Reconciliation, Halmashauri zimepangwa kulingana na ubora wake wa ukusanyaji mapato. Takwimu zinaonyesha kuwa, makusanyo ya Halmashauri zote nchini kwa mwaka 2017/2018 yalikuwa ni asilimia 81% ya lengo nchini la kukusanya bilioni 687.

Makusanyo ya jiji:
Jiji bora:
1: Dodoma - bilioni 25 kati ya lengo la bilioni 19 (180%).

Jiji la mwisho:
Mbeya - bilioni 7.8 kati ya lengo la bilioni 11.10 (71%).

Makusanyo ya Manispaa:
Manispaa bora:
1: Iringa - bilioni 4.4 kati ya lengo la bilioni 4.1
2: Temeke - bilioni 29.4

Manispaa ya mwisho:
1: Ilemela - 40%
2: Ubungo - 43%

Makusanyo ya Halmashauri za Miji:
Halmashauri za Miji zilizofanya vizuri.
1: Geita - 218%
2: Njombe - bilioni 2.6

Halmashauri za Miji za mwisho:
1: Nanyamba - 54%
2: Kahama - 63%
3: Ifakara - 65%

Makusanyo ya Halmashauri za Miji:
Halmashauri za Wilaya zilizofanya vizuri:
1: Kibaha - bilioni 3.9 sawa na 165% ya lengo la bilioni 1.8.
2: Mpimbwe - bilioni 1.5 sawa na 162% ya lengo la milioni 956.

Halmashauri za Wilaya zlizofanya vibaya zaidi:
1: Mbinga - 20%
2: Songea - 33%
3: Rorya - 37%
4: Siha - 39%

Halmashauri (zote) zilizofanya vizuri kiasilimia:
1: Geita Mji - 218%
2: Kibaha Mji - 165%
3: H/W Mpimbwe - 162%

Halmashauri (site) zilizofanya vibaya:
1: Mbinga DC - 20%
2: Singea DC - 33%
3: Rorya DC - 37%

Jumla ya Halmashauri 38 (asilimia 24%) nchini zilivuka malengo ya mwaka 2017/2018 lakini Halmashauri 14 hazikufikia malengo yake ya makusanyo.

Ukubwa wa mapato:
Halmashauri zilizoongoza kwa kiwango kikubwa cha mapato nchini:
1: Manispaa ya Ilala - bilioni 44.5
2: Manispaa ya Kinondoni - bilioni 29.7
3: Manispaa ya Temeke - bilioni 29.4
4: Manispaa ya Dodoma - bilioni 25.5

Zilizokusanya mapato kidogo:
1: Kakonko - milioni 347.1
2: Buhigwe - milioni 371.2
3: Kigoma - milioni 418.7

Mikoa iliyofanya vyema kwa malengo:
1: Dodoma - 170%
2: Geita - 104%
3: Njombe - 103%

Mikoa iliyokusanya kidogo zaidi:
1: Ruvuma - 46%
2: Simiyu - 59%
3: Shinyanga - 66%

Halmashauri 38 zilizofanya vizuri:
Geita Mji, Kibaha DC, Mpimbwe DC, Kaliua DC, Misungwi DC, Bukoba, Pangani, Kilindi, Kilombero, Makete, Dodoma Manispaa, Wanging'ombe, Longido, Ulanga, Kasulu, Bukoba DC, Njombe Mji, Ushetu, Handeni mji, Mpanda DC, Muleba DC, Babati, Mwanga, Kibaha Mji, Ukerewe, Tandahimba, Magu, Monduli, Newala, Handeni, Lushoto, Njombe DC, Iringa Manispaa, Tarime DC na Temeke.

Halmashauri 14 zilizofanya vibaya:
Iringa DC (ya 172), Kyerwa, Mbulu, Kishapu, Igunga, Itigi, Ubungo Manispaa, Ilemela, Siha, Rorya, na ya mwisho Mbinga DC

Waziri Jafo alisema kuwa, ukusanyaji wa mapato 2018/2019, kigezo cha ukusanyaji wa mapato kitakuwa ndicho kipimo cha utendaji kazi wao.
Kikao cha Tathimini ya Ukusanyaji wa Mapato, Taarifa ya Serikali kwenye ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri Nchi nzima 2016/2017, Dodoma Jiji yaongoza - JamiiForums
Mdororo wa uchumi Tanzania: Watu 400 wamepoteza kazi kwa kufungwa mabenki - JamiiForums
 

Attachments

  • 1538740947143.png
    1538740947143.png
    516.1 KB · Views: 67
last year Nairobi collected 11 billion KES = 248 billion TZS
Mombasa 4 Billion = 90 Billion TZS
Nakuru 3 billion KES = TZS 67 Billion
Kiambu 2 billion Kes = 45 billion TZS

combine all the dar municipalities it doesnt come close to mombasa..yet dar has a pop of 6 million
 
last year Nairobi collected 11 billion KES = 248 billion TZS
Mombasa 4 Billion = 90 Billion TZS
Nakuru 3 billion KES = TZS 67 Billion
Kiambu 2 billion Kes = 45 billion TZS

combine all the dar municipalities it doesnt come close to mombasa..yet dar has a pop of 6 million

Very lazy.....
 
last year Nairobi collected 11 billion KES = 248 billion TZS
Mombasa 4 Billion = 90 Billion TZS
Nakuru 3 billion KES = TZS 67 Billion
Kiambu 2 billion Kes = 45 billion TZS

combine all the dar municipalities it doesnt come close to mombasa..yet dar has a pop of 6 million
We are suppost to believe you..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
last year Nairobi collected 11 billion KES = 248 billion TZS
Mombasa 4 Billion = 90 Billion TZS
Nakuru 3 billion KES = TZS 67 Billion
Kiambu 2 billion Kes = 45 billion TZS

combine all the dar municipalities it doesnt come close to mombasa..yet dar has a pop of 6 million
Kujumlisha nayo hujui? Yani nikisema kua huna akili ni kwel

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom