Mapato ya Serikali yahujumiwa Arusha,mwekezaji atupwa ndani

Waziri2025

Member
Sep 2, 2019
85
150
Katika hali isiyo ya kawaida maofisa wa idara ya mazingira nchini (Nemc) kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la Arusha wakiwa na askari na maofisa wa Takukuru Leo wamevamia mgodi wa uchimbaji wa moramu eneo la Moivaro na kisha kuamuru kufungwa kwa mgodi huo huku mmiliki wake, Mathew Shamba Mollel akishikiliwa chini ya ulinzi na kusababisha Serikali kupoteza mapato ya sh,milioni 1 kwa kila siku.

Maofisa hao walivamia eneo hilo majira ya saa sita mchana wakiwa na askari Waliokuwa na silaha kali na kisha kuamuru shughuli zote za uchimbaji moramu katika eneo hilo zisitishwe.

Mbali na kushikiliwa kwa mmiliki wa eneo hilo pia askari hao waliamuru kukamatwa na ofisa kutoka ofisi ya kamishna wa madini kanda ya Arusha (Nyambo) anayekusanya mapato ya serikali katika mgodi huo pamoja na mwakilishi wa kampuni ya SUMA JKT ambaye anakusanya mapato upande wa halmashauri ya jiji la Arusha.

Hatahivyo, katika hali isiyo ya kawaida ofisa kutoka Nemc aliyetambulika kwa jina moja la Ben aliamuru kuachiwa kwa watu hao kwa madai kwamba watawasiliana na wakuu wao wa kazi.

Taarifa za uhakika kutoka eneo hilo zimeeleza kwamba Nemc walifika katika eneo hilo kufuatia taarifa kuwa mwekezaji katika eneo hilo amekuwa akiendesha shughuli za uchimbaji Licha ya kuonywa mara kadhaa na taasisi hiyo.

Hatahivyo, mwekezaji huyo mbali na kuonyesha nyaraka mbalimbali za vibali alizopewa na ofisi ya madini sanjari na halmashauri ya jiji la Arusha lakini maofisa hao wa Nemc walishindwa kumwelewa.

Utata umekuwa ukigubika katika tukio hilo kutokana na taasisi mbili za serikali yaani SUMA JKT anayekusanya mapato katika mgodi huo kwa upande wa halmashauri ya jiji la Arusha na ofisi ya madini kanda ya Arusha ambapo wameweka mashine za kieletroniki kukusanya mapato hayo ambapo inakadiriwa jumla ya kiasi cha sh, 1,000,000 zinakusanywa kwa siku katika mgodi huo.

"Katika ngodi huo Jiji la Arusha linakadiriwa kukusanya kiasi cha sh,600,000 kwa siku huku Ofisi ya Madini kanda Arusha inakusanya kiasi kinachofikia sh,400,00 kwa siku" Amesema mmoja ya Wafanyakazi katika mgodi huo

Hatahivyo, kumekuwa na taarifa kwamba baadhi ya maofisa wa idara ya mazingira kutoka halmashauri ya jiji la Arusha wakiongozwa na ofisa anayetambulika kwa jina moja la MBUYA wamekuwa wakishinikiza kutaka chochote kutoka kwa mmiliki wa mgodi huo ili aweze kuendelea na shughuli zake kama kawaida jambo ambalo mmiliki huyo amekuwa akimgomea.

Hatua ya mmiliki wa mgodi huo (Mollel) kukataa kutoa rushwa kumepelekea kusumbuliwa mara kwa mara na maofisa hao mpaka Leo walipofika na kisha kumkamata ambapo kwa sasa anashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi cha Kati jijini Arusha.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinadai kwamba pamoja na mmiliki wa eneo hilo kuonyesha vibali mbalimbali alivyopewa kutoka Serikalini na kusisitiza kwamba ndio maana taasisi mbili za serikali zinakusanya mapato katika eneo hilo lakini maofisa hao waligoma kumsikiliza na kisha kuamuru polisi wamkamate.

Tukio hilo limeibua maswali kwa wakazi mbalimbali wa jijini Arusha ambapo walikuwa eneo la tukio huku wengine wakienda mbali na kuhoji ya kwamba huenda Kuna baadhi ya watendaji ndani ya serikali ambao wamekuwa wakidhohofisha juhudi za ukusanyaji mapato ya serikali ambao unaungwa mkono na Rais Magufuli.

"Hawa Suma JKT wanaokusanya mapato kwa niaba ya halmashauri ya jiji la Arusha na Hawa ofisi ya madini ina maana wao wametoa vibali feki? Unawezaje kumkamata mtu kwa kutokuwa na vibali ihali serikali hiyo hiyo kupitia idara zake ndio zimempa vibali? "walisikika wakihoji baadhi ya wananchi katika eneo hilo

Mpaka sasa mfanyabiashara huyo anashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi Kati jijini Arusha kwa uchunguzi zaidi huku watumishi wawili wa Serikali wanaokusanya mapato katika eneo hilo wakiachiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Hata hivyo kumekuwa na mgongano wa kisheria baina ya taasisi za kiserikali baina ya NEMC , Ofisi ya Madini na jiji la Arusha katika utekelezaji wa sheria juu ya suala hilo ambapo vikao mbalimbali vimefanyika na kumpa Baraka mwekezaji huyo kuendelea na shughuli zake katika eneo hilo.

Lakini kumekuwa na tetesi kwamba baadhi ya watumishi wa Serikali wameligeuza suala hilo kama mtaji kwa nia ya kukwamisha juhudi za Serikali katika juhudi za kukusanya mapato ya Serikali.

IMG-20200312-WA0009.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom