Mapato ya mbuga za wanyama hasa Ngorongoro Crater na Serengeti vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapato ya mbuga za wanyama hasa Ngorongoro Crater na Serengeti vipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtumishi Wetu, Aug 10, 2011.

 1. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Wapendwa wadau wa JF naomba kupewa taarifa rasimi na wizara au taasisi inayohusika na mbuga zetu za wanyama, mapato yake yanasaidia vipi maendeleo ya taifa?

  Wananchi wanaoishi kwenye mikoa ya Manyara,Arusha, Mara iliyoko karibu na mbuga hizo wanafaidika vipi? Mahotel kama Birila Kempisk yamejengwa na nani kwa fedha kutoka wapi, kama ni wageni mbona nasikia zinauzwa kwa nini?

  Nawaomba tafadhari mwenye taarifa atujulishe, waziri au taasisi, maana ni fedha nyingi zinakusanywa kila siku tupewe pia mahesabu yake.

  Kwenye bunge budget yake iko vipi wabunge wa maeneo hayo mnayo taarifa au nayo ni meremeta? Nawasilisha.
   
 2. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Duh sasa mkuu hili swali lako mbona halijakaa sawa sawa. Kwanza unauliza hapa jamvini swali ambalo umelilenga kwa wizara na taasisi zake ?

  Na hizo hoteli sio za serikali bali za hao wanyonyaji wanaoitwa wawekezaji ( au swali lako limejificha hapa maana kuna wanaodai mvumbuzi ana share/miliki one of the luxury tented camps..). namjua huyo fogo wa kimarekani ambaye kawekeza sana mitaa hiyo, na sio kwa nia njema bali kwa kujijengea mazingira mazuri ya kukomba maliasili zetu kiulaini.. !!

  Mapato kweli ni makubwa- kuna mbuga zaidi ya 14 sasa (including the newly gazetted/about to be gazetted kama Saa Nane, Mkomazi, na ile ya kule kwa wakwere. Ila kuna komba wanayatafuna sana ikiwemo chama twawala. Ndo maana yule waziri mshamba na kiazi, na ubitoz wake wa kizamani amepachikwa pale kulinda maslahi ya fisadi namba moja nchini aka mgamba mkuu mtembezi. Hana lolote na ndiyo maana unasikia midege inabeba wanyama laivu kila siku...!
  Dili zao feki nyingine ni za kujigawia pesa kwa visingizio vya kutangaza utalii. Yule dogo Pinto kazila sana fweza pale kwa mama, na aliyempigia pasi ni huyo huyo mgamba mkuu mtembezi. Baada ya hapo ndo akamrudisha na kumpachika hapo Taswa.... huku wakiwa na miradi mingine kibao y kisanii na ya kuishi kimjini-jini..!

  Kule Oman, ndo utajua utajiri wa baadhi ya hao wanaovuna na kufaidika na utalii.
   
 3. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  mm
  Mkuu taarifa ulizoweka hapa ni chachu ya kuweza kujua zaidi mambo yaliyojificha katika mapato na matumizi ya fedha za mbuga zetu maana nasikia mapato yake yanatosha kuwa budget ya wizara kama tano hivi. Tena tunasema Tanzania maskini ni kwa vipi, tunahitaji kujua ukweli???????
   
 4. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Aliyekutuma mwambie asubiri hotuba ya kambi ya upinzani. Hapa mnataka kujua CDM wananini kwa ajili ya hotuba yao ama ? Hotuba ni jumatano next week so subiri.
   
 5. i

  iMind JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mbuga za wanyama Tanzania ziko katika mamlaka tatu. Hifadhi za Taifa ziko chini ya TANAPA, Ngorongoro iko chini ya NCAA, na game reserves ziko chini ya Idara ya Wanyamapori. Hifadhi za Taifa zinazoingiza pesa ni Serengeti na kilimanjaro. Zingine zote zilizobaki haziwezi hata kujiendesha. Hivyo TANAPA hutumia mabilion yanayokusanywa katika hifadhi hizo mbili kugharimia uhifadhi wa hifadhi zingine zote takribani 14. Pia TANAPA kama mashirika mengine hulipa kodi zote ikiwa ni pamoja ya cooperate tax ambayo hukaatwa kwenye gross collection ya shirika. Pia kuna kiwango maalum ambacho wizara ya fe
   
 6. i

  iMind JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mbuga za wanyama Tanzania ziko katika mamlaka tatu. Hifadhi za Taifa ziko chini ya TANAPA, Ngorongoro iko chini ya NCAA, na game reserves ziko chini ya Idara ya Wanyamapori. Hifadhi za Taifa zinazoingiza pesa ni Serengeti na kilimanjaro. Zingine zote zilizobaki haziwezi hata kujiendesha. Hivyo TANAPA hutumia mabilion yanayokusanywa katika hifadhi hizo mbili kugharimia uhifadhi wa hifadhi zingine zote takribani 14. Pia TANAPA kama mashirika mengine hulipa kodi zote ikiwa ni pamoja ya cooperate tax ambayo hukaatwa kwenye gross collection ya shirika. Zaidi ya cooperate Tax TANAPA na NCAA huchangia 10bil kila moja kwenye bajeti kuu. Faida kubwa ya mashirika haya ziko indirect kwani ndo kitovu cha biashara ya utalii. Wananchi mbalimbali wameajiriwa na wengine wamejiajiri katika shughuli mbalimbali ambapo kwa namna moja au nyingine huchangia pato la taifa.
  Kwa upande wa game reserve mapato mengi hutokana na uwindaji wa kitalii. mapato haya hufikia 25bil kwa mwaka. Asilimia 25 ya mapato hayo hupelekwa kwenye mfuko mkuu hazina na yanayobakia hutumika katika shughuli za uhifadhi. Kwa ujumla uhifadhi wa wanyama ni kazi ngumu inayohitaji rasilimali fedha na watu kwa kiasi kikubwaa.
   
 7. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Sio zote bana, Tarangire, Manyara, Arusha aka momela pia hazipo mbali sana ktk kuingiza mapato. Kisingizio cha kusema mabilioni yote yanakwenda kusaidia mbuga nyingine kujiendesha hakina nguvu kabisa. Mafweza mengi pia yanaliwa tena kiulaini sana. Kuna chains kuanzia juu hadi chini ktk mageti na vitabu vya permit feki, achilia zile zinazoliwa huko huko HQ na wanazojichotea CCM anytime. Wewe inji masikini kama bongo halafu unasikia sitting allowances za bodi za IM Tsh wapi na wapi. je, unajua bodi ikimaliza muda wake wa 3 yrs wanakomba zaidi ya milioni 28 kama bonasi, halafu hao hao wanateuliwa tena na wengi wakiwa wabunge wa CCM, na wastaafu !! Je, unajua extraordinary meetings ngapi wanajipangia ili kuvuta hiyo Milioni, na unajua safari zao za nje ya nchi kwenda eti kutangaza utalii huku wakikomba mabilioni...!!
  Ndiyo maana sishangai mtu kama Mh. Lembeli kukenua kulipiwa ndege na barrick yeye akiwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya maliasili na mazingira kwenda kuwakagua ho hao ( kumbuka post hii bunge lililopita alikuwa nayo ndugai, na wote hao walikuwa wafanyakazi wa wizara moja..)

  Hayo ya kujifanya yeye ni mpiganaji wa ufisadi anawaongopea malofa tunaomjua hawezi kufungua bakuli maana yeye kwenye pesa mijicho humtoka kama simblis na zile mvi hugeuka rasta. Ni mtafunaji mkubwa sana na ubitoz wake ndo kabisa. Alizikomba sana akiwa PR wa Tanapa na ndiyo zilizompa ubunge licha wa ukihiyo wake wa kujifanya ana madigirii ya ujerumani kumbe ana kacheti cha darasa la elimu wa watu wazima ila kwa vile aliishi kule na anajua kukipopoa kijerumani basi akapata ulaji.... !! Post iliota mbawa maana walikomaa alete cheti au apigwe chini....
   
Loading...