Mapato ya CHADEMA kuporomoka kwa zaidi ya 50%

mnyamiwono

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
708
71
Wanajamvi habari,

Imebainika kwamba mapato ya chama kikuu cha upinzani hapa nchini (CHADEMA) ambayo yanatokana na ruzuku ya serikali yataporomoka sana hasa baada ya uchaguzi mkuu mwakani. Kwasasa chadema inapata ruzuku ya takribani sh milioni 203 kwa mwezi kutoka serikalini ikiwa ni ruzuku.

Wadau mbalimbali wa kisiasa wanadai kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa chadema kupoteza nusu ya majimbo waliyoshinda katika uchaguzi wa 2010, hii ni kutokana na wabunge wengi wa chadema kuendekeza siasa za bungeni badala ya majimboni ambapo mpaka sasa wengi wao wanalalamikiwa kushindwa kazi ya uwakilishi wa majimbo yao.

Sababu nyingine ni kwamba chadema kimepoteza uelekeo hasa katika kujiimarisha kwa wananchi na badala yake imejikita katika siasa za UKAWA ambazo kimsingi hazina mantiki yoyote kwa maendeleo ya chama.

Pia sababu nyingine inayodaiwa na wanachama wa chadema ni matumizi mabaya ya ruzuku ya chama na ukiukwaji wa demokrasia ndani ya chama ambapo mpaka sasa uongozi uliopo ni wakifalume na kibiashara(saccos) na kupelekea wanachama wengi kuondoka kimya kimya kuliko wanaojitangaza.

Hali hii inapelekea watu kuamini kuwa kuna anguko kubwa la kisiasa ndani ya chadema baada ya uchaguzi mkuu 2015.
 
Na mapato yako binafsi vipi? Utaendelea kuchangamkia LB7? Kajipange upya, kuandika hujui!
 
unatumia unajimu kutabiri au utafiti wa kisayansi kaka?
 
Hivi baada ya kifo cha shekh yahaya bado kuna watabiri wengine? ni kweli tunapoelekea 2015 kutabiria ushindi CCM kunalipa sana,muda si mrefu tutawasikia REDET wanafufuka
 
Kuporomoka kwa mapato sijui. Lakini hivi wale wafuasi wa CUF kwa shabaha na tabia vinaendana kweli hadi waadhimie kuwa pamoja ktk UKAWA na Chaguzi zijazo?

Noo let's think twice. Naona giza mbele. Ushauri sahihi upatikane.
 
Mtei alishaa onya jamani maana tangu Mbowe anze kuzini hamsukilizi tena mzee wetu mtei
 
Back
Top Bottom