Mapato uwanja wa mpya wa Taifa; je tunaelezwa kile kilichopatikana au kuna ufisadi?

Magehema

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
428
27
Wana JF, kuna hili suala la mapato yanayopatikana katika mechi zinazochezwa katika uwanja mpya wa Taifa, je tunachoelezwa na Mwakalebela ndicho hasa kilichopatikana au kuna watu wanafanya usanii???
 
Kuna ulazima gani wa kutangaziwa mapato ya uwanja huo? Ili tufanye nini juu ya mapato hayo?
 
Kuna ulazima gani wa kutangaziwa mapato ya uwanja huo? Ili tufanye nini juu ya mapato hayo?

Mkuu nahisi unamatatizo katika ubongo si bure.
Kadri siku zinavyo kwenda mapato yanapungua katika liuwanja la Taifa naona kuna ujanja ujanja flani kama uwanja wa zamani ule uhuru.
 
Wana JF, kuna hili suala la mapato yanayopatikana katika mechi zinazochezwa katika uwanja mpya wa Taifa, je tunachoelezwa na Mwakalebela ndicho hasa kilichopatikana au kuna watu wanafanya usanii???

Ni vema tujue kwanza kwa waliokwenda kutuambia kama Uwanja ulijaa au la. Kama uwanja ulijaa basi huo ni UFISADI mwingine na ni WIZI MTUPU!

Nadhani TFF wanahusika moja kwa moja na huo utata kwanza nilishangaa sana kususikia kuwa kiingilio ni shsh 50,000/-! Ilikuwa ghali mno, Kiingilio cha juu ingekuwa shs 15,000/- na cha chini shs 5,000/- Mapato yangekuwa makubwa mno. Uwanja unachukua watu 60,000 kama wastaniwa kiingilio kingekuwa shs 10,000/- zingepatikana 600,000,000/- Milioni 600!

TFF inabidi wajifunze mahesabu rahisi, kiingilio kikubwa cha elfu 50 maaana yake una-attract ufisadi i.e watu kutumia njia za mkato kuingia kama vile kumpa mlinzi wa mlangoni shs elfu 10 au 5 na kuingia. Kama Kiingilio kingekuwa kati ya elfu 10 na elfu 5, ni wazi watu wengi wangehamsaika kuchangia ili waingie kwa halali.

Otherwise TFF hawawezi kukwepa lawama za wizi maana kila wakati tunasikia pesa kiduchu zinapatika Uwanja wa Taifa kwa mechi kubwa za watu wengi; pengine kuna waru wanaweka viingilio vikubwa ili kuwawezesha kuchora dili watu wapitie njia za panya. KUMBUKA kuwa Uwnaja wa Taifa haiwezekani kuruka ukuta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom