Vugu-Vugu
JF-Expert Member
- Feb 24, 2017
- 1,106
- 1,264
Safi sana mamaView attachment 2112267
Kumekuwa na mgogoro mkali wa kibiashara hasa ya Parachichi baina ya Tanzania na Afrika ya Kusini uliodumu kwa mwongo mzima(miaka kumi) sasa bila muafaka wowote.
Mtakumbuka February, 2021 kabla ya ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan Jumla ya tani 3.514 za avocados|parachichi toka Tanzania zilizokuwa zinasafirishwa kwenda Africa ya Kusini mali ya Kuza African Company ziliharibiwa vibaya na mamlaka za Serikali ya Africa kusini.
Leo miezi tisa baadae chini ya Utawala madhubuti na imara uliojaa neema na furaha wa Rais Samia Suluhu Hassan Sasa rasmi ni ruksa kwa Mtanzania kuingiza na kuuza Parachichi Africa ya kusini,Hivi Watanzania tumtake nani kama sio Samia Suluhu Hassan?
Hili linafuatia ikiwa ni baada ya Serikali ya Africa ya kusini kupitia kwa taasisi yake inayoshughulika na Uhifadhi wa Mimea yaani National Plant Protection Organisation of South Africa (NPPOZA) kukubali kuruhusu biashara hii baada ya miaka kumi ya msuguano mkali baina ya nchi hizi mbili.
Makubaliano haya ni kwa mujibu wa barua kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Mimea Africa ya Kusini yaani South African Plant Health Ndg Jan Hendrik Venter ya tarehe 16|11| 2021 ikiwa ni baada ya nchi hizi mbili kukubaliana kwa njia ya Mtandao.