Mapambano ya polisi na raia Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapambano ya polisi na raia Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Jan 19, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Yaliyojiri Zanzibar leo (Channel Ten 7pm news bulletin):

  Mgambo wakiandamana na polisi wamevamia eneo maarufu la biashara la Darajani Zanzibar kutaka kuwahamisha kwa nguvu wafanyabiashara wadogo wa Jua Kali.
  Vijana hao wa Zenji wakakataa kuhamishwa kwa nguvu bila kupewa taarifa na ikazuka vurugu kubwa.

  Picha za TV zimemuonesha mtu mmoja mwenye hasira ambaye alikuwa tayari kutoa maisha yake mhanga akimfukuza mgambo mmoja na kisu akiwa na nia ya kummaliza kabisa. Polisi wenye mitutu walishikwa butwaa wakabaki wakiangalia tu kijana huyo akimfukuza mgambo na kisu kwa lengo la kumchoma. Katika purukushani hizo, polisi mmoja alipigwa na jiwe usoni lakini hakuumia sana.

  Polisi wa Zanzibar hawakutumia mabomu ya machozi, maji ya kuwasha, rubber bullet au risasi za moto kama wenzao wa Arusha. Wakaamua kuahirisha zoezi la kuwahamisha kwa nguvu wafanyabiashara wadogo na kuagiza manispaa na wafanyabiashara hao wakae pamoja kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

  FUNDISHO


  1. Watanzania hawakubali tena kuonewa na kunyimwa haki yao hata kwa kutumia mitutu ya bunduki

  2. Vita ya mgambo ma machinga hapa nchini ni time bomb. Kuna siku maafa makubwa yatakuja kutokea.

  3. Polisi wa Zanzibar wamejifunza kosa la mauaji la polisi wenzao lilitokea hivi karibuni Arusha. Polisi wanaendelea kuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani hapa Tanzania kwa wepesi wao wa kupiga na kuuwa raia wasio na silaha.
   
Loading...