Mapambano na M23,Tanzania itafaidikaje?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Ndugu Bernard Membe jana amenena. Ya kuwa Tanzania ipo tayari kupeleka wanajeshi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kuwadhibiti Waasi wa March 23 Movement almaarufu kama M23 ambao wanaendelea kumnyima usingizi Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo. Baada ya kuteka Goma,Waasi hao wamefanikiwa kuuteka Mji mwingine wa Sake wakielekea katikati ya Bukavu.

Kwa mujibu wa Membe,Tanzania inasubiri 'ruhusa' ya Umoja wa Mataifa ili kuwapeleka wanajeshi wake huko Kongo-DRC.Sasa,nchi yetu itafaidikaje: kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni? Kwani tumeombwa na Kabila/Umoja wa Mataifa au ni uamuzi wetu binafsi?
 
kama ni kulinda amani na kutoa mafunzo hi ni sawa. kama Nikupigana ni hapana kwa vile hakuna faida yeyote kwetu sisi.
 
Kwa mujibu wa Membe,Tanzania inapeleka wanajeshi kupambana kivita ili kuwadhibiti M23
 
mimi nakubaliana na membe kwani naamini tanzania huru na yenye amani ni ile tu inayozungukwa na majirani huru na wenye amani!!
 
mimi nipo tayari kwenda kongo kuikomboa dhidi ya uvamizi wa rwanda na uganda kama nitatakiwa kufanya hivyo kama sehemu ya majeshi ya ukombozi , wenzetu wanateseka sana!
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Ndugu Bernard Membe jana amenena. Ya kuwa Tanzania ipo tayari kupeleka wanajeshi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kuwadhibiti Waasi wa March 23 Movement almaarufu kama M23 ambao wanaendelea kumnyima usingizi Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo. Baada ya kuteka Goma,Waasi hao wamefanikiwa kuuteka Mji mwingine wa Sake wakielekea katikati ya Bukavu.

Kwa mujibu wa Membe,Tanzania inasubiri 'ruhusa' ya Umoja wa Mataifa ili kuwapeleka wanajeshi wake huko Kongo-DRC.Sasa,nchi yetu itafaidikaje: kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni? Kwani tumeombwa na Kabila/Umoja wa Mataifa au ni uamuzi wetu binafsi?

Hapa paangaliwe vyema...
 
Swali lako ni sawa na kusema 'utafaidika na nini ukisikia mwizi anabomoa nyumba ya jirani yako nawe ukachukua hatua ya either kumjulisha kwa simu au kelele au kutoka hata na panga ili mshirikiane kumfukuza mwizi huyo! Unajuaje labda mwizi akimaliza mlango wa jirani anakuja kwako!?. Amka think outside of a box.
 
Back
Top Bottom