Mapambano/ Mashambulizi Dhidi ya Viongozi vijana CDM: Saa na Ukombozi Iko Mlangoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapambano/ Mashambulizi Dhidi ya Viongozi vijana CDM: Saa na Ukombozi Iko Mlangoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Mar 6, 2012.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mbunge wa Jimbo la Ubunge Kupitia Chama Cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA) Anashambuliwa, Anatuhumiwa, Anashauriwa.

  Wanaomshambulia ni Vijana wa CCM "Eti Wakijidia kwamba wao ni CDM". Nadhani CCM kwa Mara Nyingine WAMEPOTEA au WAMEKOSEA Strategies. Kinachonifurahisha ni Ukimywa wa Mnyika na Umakini wa Majibu pale anapoona kwamba anapaswa Kujibu Hoja ( Si Majungu) zinazoletwa Dhidi yake. Mnyika Hajawahi kujibu Fitna, hiyo ni Sifa kuu inayowanyima Usingizi vijana wa CCM waliopania Kumprovoke Mnyika.

  1. Wapo wanaojifanya kwamba "WAO NI WAPIGA KURA WA UBUNGO".

  Hawa wamekuwa eti wakimtahadharisha kwamba "Asipkuwa Makini atapoteza Jimbo lake ifikapo 2015". Wanataka Kuaminisha kwamba Kwamba Mnyika toka amechaguliwa na Wananchi wa Ubungo amewasahau Wananchi wa Ubungo na kujikita zaidi katika Shughuli za Chama. Ukiwasoma kwa Umakini watu hawa wana lengo la Kumkatisha Tamaa JJ katika Kuwawakilisha wananchi wa Ubungo.

  2. Wananchi wa Ubunge wapanga Kuandamana Kumpinga Mnyika

  Juzi hapa ilikuja Thread iliyosema kwamba wananchi wa Makuburi wamepanga kuandamana kumpinga Mbunge wao. Mh John Mnyika akawaambia kwamba kama watashindwa kupata kibali angewasaidia na Alipoona Kimya yeye ndio akaandamana kuwafata. Alichokita huko ni tofauti kabisa na Propaganda za CCM Mtandaoni. Kesho yake wakaja na Hanari Mnyika apigwa Mayai Viza.

  Ukiangalia lengo la wana CCM hao si Kushauri Mnyika bali ni Kujaribu kugomanisha Viongozi vijana ndani ya CDM. CCM wameshatambua kwamba Nguzo kubwa ya CDM ni kuungwa mkono na Vijana. NA HILO LINAWATISHA MAANA HAKUNA DALILI KWAMBA VIJANA NCHINI KATIKA MIAKA YA KARIBUNI WATABADILI MAWAZO NA KUANZA KUIPENDA CCM.

  Lengo kuu la CCM ni kuwafanya Vijana ndani ya CDM wajione hawana THAMANi, wajione wao ni DUNI lengo ni KUWARUDISHA NYUMA.

  Mapambano dhidi ya CDM hayako tu kwa Mnyika bali kwa Vijana wote ambao wanaonekana wako LOYAL CDM. Vijana wengi wa CDM wameingia katika Mashambulizi hayo.

  1. Zitto ametukanwa sana na "Vijana wa CDM". Ilifikia Wakati unahisi Kesho Zitto anarudisha kadi ya CDM lakini Zitto ameendelea kusimama Imara kabisa ni moja kati ya Nguzo Imara ndani ya CDM. Zitto wamemshindwa.

  2. Dr. Slaa naye amekuwa Centre ya Masamabulizi kutoka kwa "Vijana hao wa CDM"/ Dr. Slaa ameendela kusimama kidete licha ya Matusi na Kejeli kutoka kwa "Vijana hao wa CDM".


  Wito wangu kwa Vijana wa CDM

  Ni Vizuri Mkatambua kwamba CHADEMA ni Tishio kwa CCM. CCM haipendi na Kamwe HAILALI mpaka kuhakikisha kwamba Nguvu ya CDM ambayo ni VIJANA inabomolewa.

  Nawatakia Usiku Mwema
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Shahisha hapo Mbunge wa Jimbo la Ubunge..
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mbona kujiteteta kwa maneno mengi hivyo inawezekana kuna ukweli ndani yake nini? Mimi siyo wa Dar es Salaam nisichangie sana mada hii.
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Good and brilliant analysis! Wana CDM kamwe hatutishwi na hawa vijana wa CCM wanaoshambulia viongozi wetu makini kupitia mitandao ya kijamii.Hakika wamechemsha.Tuna imani kubwa na Mbowe,Slaa,Zitto na Mnyika.
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nani asiyekujua wewe ni Magamba
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ritz polebi sana nasikia huko Meru mmezomewa njia nzima mpaka mkapotea njia.
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ritz poleni sana nasikia huko Meru mmezomewa njia nzima mpaka mkapotea njia.
   
 8. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,589
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Watadanganyana wenyewe. Tulishawajua.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wengine tulishaona hili tangu siku za mbele kidogo na ndio ukweli kwa nini TULIMUONYA Mh John Mnyika akakae mbali kabisa na hako ka-mdudu kanakoitwa USHIRIKIANO USIORASMI WA WANASIASA VIJANA nchini akiwamo Februari Ma-Ropes pamoja na yule dogo Nape - janja tupu za nyani kula mhindi na kuacha mabua.

  Maadam wenzetu wengine na nyie tayari mmeshastukia hio dili feki, bado ndio kama hivo mchezo wote umekwisha. Vita vya ukombozi mbeeele kama tai huku tukiwapeleka MAFISADI papa na sasa hawa wengine vidagaa kwenye kona ki-sawsawa.

  Twende basi, sinema yote ya pale Jimbo la Ubungo tutakuja kukunjua mkanda wake hivi karibuni ili muone uchafu wa baadhi tu ya vijana wenzetu wanavyoshiriki na kutamani kumhujumu Mnyika kwa kuwa tu nuru njema yaanza kumuangazia kidogo kidogo.

  Narudia hapa, Mnyika kaa mbali sana na hilo genge - lengo ni kukuangamiza wewe.
   
 10. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #10
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujaelewa? Mkuu inaeleweka sana na uchambuzi wako ni wa kina na makini kwani hawa ki na Ritz hiyo kazi ndo wamekabidhiwa kubadirisha ID kila siku na kujifanya wao ndo CHADEMA moyo na kuanza ku criticize viongozi chama. chadema wala haitaki mawazo, maoni na wala ushauri wao. Kiongozi wa chadema anajengwa kabla ya kupewa hiyo dhamana. Chama kiko makini na imara katika kumkosoa na kumwelimisha yeyote anayeonekana kukosea maadili na wajibu wake katika uongozi wa kada zote na wakati mwingine chama hakisiti kumwajibibisha anayeonekana kushindikana. Ritz acha hizo hamna mapenzi na CHADEMA NGUVU YA UMMA.
   
 11. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Kama naelewa sawasawa ni kwamba, vijana wa CCM baada ya kushindwa kuleta mabadiliko ndani ya chama chao CCM (mwulizeni Nape!) eti sasa wamepania kuleta kisirani ndani ya Chadema kwa kujibatiza vijana wa Chadema! Bila shaka ndio maana wanapokabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wapenzi wa kweli wa Chadema, hukimbilia kuwatuhumu kuwa ni watu wasioambilika!

  Binafsi mimi wito wangu kwa wapenzi wa kweli wa Chadema ni kuwa baada ya kusambaratika kwa CUF, ukombozi wa taifa umebaki mikononi mwa Chadema, period. Watatokea akina TUNTEMEKE wengi tu lakini kamwe msikubali kuyumbishwa na hawa wapenzi uchwarawa Chadema kwani ni rahisi kuwatambua. Utakuta wanaungwa mkono na mapandikizi yasio na nia nzuri kwa Chadema!

  Lengo la mtu yeyote mwenye mapenzi ya kweli kwa taifa letu liwe ni kuuondoa huu utawala wa kidhalimu wa CCM, basi.
   
 12. R

  RMA JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red una maana gani? Shule ni kitu muhimu!
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwa ubungo, wanapoteza muda, huyu mbunge anakubalika na anafanya kazi. Wakamuulize Mhe John Pombe atawaambia.
   
 14. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  lugha gani mkuu
   
 15. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Watakuja kwa majina na ID tofauti wakijidai wanaishauri Chadema, kuna watu nilikuwa nawaamini kabisa lakini siku hizi nashindwa kushangaa wamebadilikaje.

  Kitu ninachokiona katika wimbi hili kama mleta hoja anavyosema, CCM wameshindwa kubuni mbinu ya kurudisha imani ya vijana kwa chama chao, kilichobaki ni kutumia baadhi ya vijana (some of them walijulikana kama great thinker wa JF) kujifanya washauri wa Chadema TUNTEMEKE-type, ndio maana unakuta ushauri wa hovyo hovyo unakuja kutoka kwao. Utashangaa siku hizi hadi ritz naye amekuwa mshauri wa Chadema na anaitwa great thinker na watu tuliokuwa tuliowaamini kuwa ni wana Chadema.Lakini uonapo wimbi linakuwa hivi jua ukombozi umekaribia.
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  walipeni vijana msijaribu kupotezea hapa..

  Naona kundi la kupata (Albedo, Maranya, Mag3, Feedback na Molemo wako mbiooooni kusafisha)

  Hii ni vita kati ya kundi la kupata na kundi la kutumika..

  Endeleeni kuficha maradhi...oops
   
 17. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #17
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukisha mjua adui hakusumbui
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Mar 7, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Watu,

  Jimbo la Ubungo ni jimbo gumu sana Geo-politically.Sijui ni mbunge gani wa CCM kati ya wale wote waliopambana kwenye kura za maoni hadi wale wagombea ubunge waliopitishwa na vyama vyao wangeweza kufanya better than Mnyika.Kipindi cha kampeni ubungo kilinipa fursa ya kujua ugumu wa lile Jimbo.Mnyika so far anafanya kazi nzuri kilichopo ni kumpa ushirikiano.Na hasa vijana wa jimbo la Ubungo tumuunge mkono Mnyika kwa kuwa sisi ni agents of change

  Pamoja na mizengwe ya chama dola CCM tangu kwenye kampeni kutangaza matokeo nk,itakuwa jambo gumu kwangu kuamini kwamba CCM hawawezi kumfanyia sabotage katika utekelezaji wa majukumu yake.Tumuunge kamanda mnyika katika kazi ya uwakilishi,kazi yamabadiliko siyo kuitoa CCM tu bali tuendelee kuwaonyesha ni kwa jinsi gani sisi ni chaguo sahihi kwa watanzania
   
 19. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Hicho ndio kitugani?
   
 20. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,674
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  magamba yanajuana!
   
Loading...