#COVID19 Mapambano dhidi ya Uviko 19 - viongozi wa dini mbalimbali watakiwa kuendelea kuisaidia Serikali

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO 19 - VIONGOZI WA DINI MBALIMBALI WATAKIWA KUENDELEA KUISAIDIA SERIKALI

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Jokate Urban Mwegelo amewasihi Viongozi wa Dini kuendelea kuisaidia Serikali kupambana na Ugongwa wa Virusi vya Korona ( UVIKO 19).

Mhe. Mwegelo ametoa rai hiyo leo Julai 27 , 2021 wakati akizungumza katika kongamano la viongozi wa Dini , lililofanyika katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC).Kongamano ambalo lililenga kutazama nafasi ya viongozi wa dini katika utoaji wa elimu kwa umma kuhusu UVIKO 19 ,sambamba na kuhakikisha kwamba waumini na umma kwa ujumla unafikishiwa taarifa sahihi kuhusiana na UVIKO 19, pamoja na miongozo ya serikali katika kupambana na ugonjwa huo, ikiwemo namna ya kujikinga na kuwakinga wengine kuepuka maambukizi.

Akizungumza wakati wa hotuba yake Mhe Mwegelo amewasihi viongozi hao kuendelea kuwa msaada kwa Serikali katika kuelimisha jamii juu ya ugonjwa wa uviko19, kwa kuendelea kutoa taarifa sahihi, na kuhimiza utii juu ya maagizo ya watalaam na serikali juu ya ugonjwa huo.

Aidha Mhe. Mwegelo amewapongeza viongozi hao kwa kuandaa kongamano hilo litakalokwenda kusaidia kutoa elimu kwa wananchi wanaohudhuria katika nyumba za ibada. "Nawapongeza viongozi wa dini kwa kutambua nia ya dhati ya serikali katika kuwaelimisha wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huu".Alisisitiza Mhe Mwegelo.

Nae Askofu wa jimbo Katoliki la Mtwara, Mhashamu Askofu Titus Mdoe amemshukuru Mhe. Mwegelo kwa kuendelea kufanya kazi kwa ujasiri ,ameahidi kwa niaba ya viongozi wa dini zote mbili (Waislamu na Wakristo) kwamba wataendelea kushirikiana na Serikali katika kutimiza majukumu ya kulinda wananchi na afya zao.

Mhe. Mwegelo ameendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Temeke pamoja na Taifa kwa ujumla, wanatambua namna bora za kujilinda dhidi ya maambukizi ya UVIKO 19 , na kupata taarifa sahihi kutoka kwa watu sahihi tangu kuibuka kwa wimbi la 3 la ugonjwa huo nchini huku akishirikikiana na watendaji wa Serikali pamoja na wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini nchini.
Kwa upande wao Viongozi wa Dini katika umoja wao, wamekubaliana kuwa watajikita katika kubuni mbinu mbalimbali za kuwaelemisha wananchi wao kupitia nyumba za ibada na hata vyombo vya habari.

Viongozi hao wamekubali pia na kuona kwamba suala la chanjo ya UVIKO19 ni la haraka, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu sahihi ya chanjo, kuelimisha kuhusu aina za chanjo na kwa nini kama Taifa tumeamua kutumia chanjo hizi. Zaidi Viongozo wa Dini wameomba na wamedhamiria kuendela kupata taarifa za kina za maendeleo ya ugonjwa katika Taifa letu ili kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana nazo. Lakini kwa namna ya pekee wamekubaliana kuendelea kufanya maombi kuhusu ugonjwa huu kama sehemu ya wito na utume wao lakini pia kutumia utaalamu na wataalam katika kupambana na UVIKO 19.

-cyhlkk.jpg


-ndv64d.jpg


20210727_211418.jpg


20210727_211421.jpg
 
Back
Top Bottom