Mapambano dhidi ya ufisadi yachangia maendeleo ya kasi ya China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,033
Ufanisi wa utawala wa chama cha kikomunisti nchini China umesifiwa sana kutokana na ufanisi wake katika kutokomeza ufisadi nchini humo. Sera dhabiti za uongozi zilizopo zimeweza kuwakabili mafisadi ipasavyo na kuiweka China katika nafasi nzuri ya kutamanika kote duniani kutokana na hali. Haya ni maneno ya msomi wa masuala ya kidiplomasia kutoka Kenya, Fred Omondi akizungumza na mwanahabari.

Kwa takriban miaka mia moja tangu kuasisiwa, chama cah kikomunisti cha China kimefanya mengi ya kupigiwa mfano. Aidha, swala moja ambalo lipo wazi kabisa ni namna cha hiki kimechangia pakubwa katika kupigana na ufisadi nchini China. Bwana Fred Omondi, msomi wa masuala ya kidiplomasia anasema kwamba chama cha CPC kinapendwa sana na Wachina

Vita dhidi ya ufisadi si rahisi. Mataifa tajika ulimwenguni yanajaribu lakini yanashindwa. Ufisadi umekuwa kikwazo kikubwa kwa mataifa mengi kuafikia malengo yake. Anavyoelezea bwana Omondi, vita dhidi ya ufisadi vinahitaji kuwepo sera kali dhidi ya washukiwa.

Katika kampeni yake ya kupigana na ufisadi kufikia, Rais Xi Jinping wa China amehakikisha kwamba mafisadi wote nchini wanaadhibiwa. Rais Xi Jinping amefanya vita dhidi ya ufisadi kuwa ajenda kuu ya utawala wake. Maafisa wakuu wa kisiasa wamefungwa hawasazwa kwenye vita hivi.
 
Back
Top Bottom