Mapambano dhidi ya ufisadi na ubadhilifu wa mali za umma umekiimarisha CCM

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Hili halina ubishi kwa wadau wa siasa hapa nchini kuwa wananchi wana imani kubwa sana na chama tawala cha CCM. Hii ni kwa sababu kimejidhatiti kwa kupambana na ufisadi na kuziba mianya yote ya ukwapuaji mali za umma. Japokuwa ni ngumu kudhibiti kwa asilimia mia moja, lakini awamu hii ya tano imejitahidi sana na na habari za skendo kubwa kubwa kama Epa,Richmond ,Escrow n.k zimesahaulika.

Hatua hizi madhubuti za kudhibiti mianya ya rushwa na ufisadi ndio zimesababisha upinzani nchini Tanzania kuishiwa nguvu hii ni kwa sababu wapinzani walikuwa miaka yote wakisubiri kuikaba Serikali ya CCM pale tu wanapobaini kuna ufisadi. Jambo hili limewamaliza nguvu kabisa wapinzani na sasa hawana hoja yoyote ya kuisumbua CCM.

Na kwa kutumia mwanya huu wa kudhibiti ufisadi na ubadhirifu serikali ya CCM imekuwa na uwezo mkubwa wa kukusanya mapato na hatimae kutekeleza ahadi na ilani yake ya uchaguzi.

Ukienda ziwa Nyasa kuna meli mbili mpya zimetengenezwa. Ziwa Victoria tayari New Mv Victoria hapa kazi tu imeanza kuchapa kazi. Miradi mikubwa kama ujenzi wa SGR na JNHPP inatekelezwa bila kigugumizi. Na hii ni baadhi ya mifano tu maana kwenye sekta ya afya na elimu ndio mambo makubwa yamefanyika.

Matokeo ya hatua hizi madhubuti ni kukipa CCM ushindi mkubwa kwenye uchaguzi unaokuja hapo Oktoba maana vyama kama Act wazalendo na Chadema havina hoja yoyote ya msingi ambayo wataweza kusimama jukwaani na kuwaambia wananchi.
 
Mpaka sasa karibu saa nzima imepita hakuna anayewaelewa nivyi watumwa wa magu. Kuweni huru washkaji.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom