zimmerman
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 1,628
- 3,155
Kwa style ya uongozi wa JPM (ukali wa pilipili, hataki kukosolewa, mbanaji pesa, fukuza fukuza, very undeplomatic, n.k) usingeweza kuamini kwamba mtu kama huyu angeweza kupendwa na watu. La kushangaza JPM ni kiongozi pekee aliyeweza kukonga mioyo ya watu wengi nchini na hata nje ya nchi. Why mtu mgumu kama yule aweze kugusa mioyo ya watu?Nilimsifia Magufuli kwa mambo matatu [kuhusu corona].
1. Consistency [bila kujali matokeo].
2. Kutenda kama alivyokuwa akisema.
3. Kutokuwafungia watu ndani [‘rockdown’].
Mpende Magufuli au umchukie, jambo ambalo huwezi kusema ni maneno yake hayakuendana na matendo yake, ni hili la corona.
Hii kitu mi naamini iwape funzo wanasiasa wote nchini na duniani kote. Kumbe ubora wa kiongozi si kuto speech nzuri nzuri au kuonekana mtu "cool". Sifa ya kwanza ya kiongozi bora na kuishi kile anachokihubiri. Kwa vurugu za JPM asingekuwa anaonyesha kwa mfano wake mwenyewe kwamba "Hapa Kazi Tu" nadhani angekuwa kiongozi mbovu kabisa kuwahi kutokea kwa aina ya personality yake. Lakini kumbe people wanajali mambo deep zaidi nayo ni kuishi kile unachikihubiri -- na hapo ndipo JPM alifanikiwa.
Legacy ya kwanza kabisa ya JPM ni ya kiongozi aliyefia akiwa mstari wa mbele vitani kabisa. Iwe ni kwa Corona, iwe ni kwa adui mtu, the man feared no evil, aliipambani nchi yake hadi pumzi yake ya mwisho.
Rest in Peace JPM, your services to this country will always be hardcoded onto the souls of the nation.