Mapambano dhidi ya corona si ya copy & paste: kisayansi bado mengi hayajajulikana 100% kuhusu gonjwa hili

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,952
4,326
Ugonjwa huu ni mpya. Umeikumba dunia yetu kwa kishindo kikubwa kuanzia mwaka huu. Mgonjwa wa kwanza alitangazwa huko China tarehe 10 Jan 2020. USA walitanganza mgonjwa wao wa kwanza siku 10 baadaye. Zikafuata Ufaransa 23 Jan, Canada 24 Jan, Ujerumani 26 Jan, Finland 28 Jan na Italy 29 Jan. Tarehe 30 Jan 2020 Sweden, Urusi, Sweden, Spain na UK wakatanganza mgonjwa wao wa kwanza. Nchi zingine zikafuata kwa tarehe tofauti tofauti. Hadi leo nchi zaidi ya 202 duniani zimekumbwa na gonjwa hili. Tanzania tulitangaza mgonjwa wa kwanza 15 March yaani wiki 2 tu zilizopita.

Madaktari na watalaamu wengine wa afya ya binadamu na wanyama wamekuwa wakikesha kutafiti gonjwa hili ili kupata suluhisho lake kitiba na kikinga. Kwa muda huu mfupi wa miezi 3 yapo mengi ambayo wameyabaini lakini pia yako mengi ambayo bado hayajajulikana wazi. Hata yale ambayo awali walifikiri yamejulikana, mengine yanaendelea kuonekana aidha yana utata au hayako sahihi. Hii ndiyo kawaida ya utafiti. Na jambo hili la kisayansi haliwezi kuwa la kirahisi rahisi kama kujumulisha mbili na mbili.

Hivyo basi tunapofanya maamuzi ya kukabiliana na janga hili ni vyema tukazingatia ushauri wa watalaamu wetu. Haya mambo si ya kukopi na kupesti toka nchi fulani fulani kama alivyosema spika wa bunge letu. Kunahitajika kuwa na a National Technical Advisory Comittee inayoundwa na madaktari weledi kwenye nyanja mbali mbali zinazoguswa na janga hili eg internal medicine, surgery, epidemiology. Madaktari hawa watoke kanda zote za nchi yetu kama tulivyofanya enzi zile gonjwa la ukimwi lilipoingia nchini kwetu. Hii kamati ni tofauti na ile Technical Nationa Task Force iliyoundwa chini ya katibu mkuu wa wizara ya afya ambayo ni ya utekelezaji/ utendaji wa maamuzi.

Baadhi ya maeneo ambayo bado ni changamoto kwenye uelewa wetu wa sasa kuhusu gonjwa hili ni yafuatavyo:

1. Uenezi wa gonjwa hili (mode of transmission):
Kwa uelewa wetu wa sasa kuhusu mode of transmission ya ugonjwa huu tulitarajia kabisa kuwa mbinu ya total lockdown (wananchi wote kutotoka majumbani mwao) ingekata kabisa uenezi wa virusi hivi ndani ya kipindi cha wiki mbili. Muda huu wa wiki mbili umetokana na uelewa wetu wa sasa kwamba incubation period (muda kutoka kupata virusi hivi hadi kuanza kuugua) ya ugonjwa huu ni siku 0 hadi 14. Na kwamba vijidudu hivi vinauwezo wa kuishi kwenye surfaces (maeneo) mbali mbali kwa siku zisizozidi nne.

Mbinu hii ilitumika kwa mara ya kwanza huko China na ulionekana kufanya kazi sana. Lakini mbinu hii hii huko ulaya na Amerika inaonekana kutokufanya kazi - yaani kwenye hizi mbinu hii badala ya wagonjwa wapya na vifo vipya kupungua, tunashuhudia vinapanda kwa kasi zaidi ya maradufu kila siku. Kwa mfano kwa taarifa za jana huko USA wagonjwa wapya walikuwa 25,948 na vifo 790, Italy wapya 4,782 na vifo 727, Spain wapya 8,195 na vifo 923.

Nchi kama Sweden na Japan ambazo kuwaacha raia wake huru (no total lockdown) wakiendelea kupunga hewa ya nje na kuota ultra violet rays za jua, hadi sasa uenezi wa gonjwa hili uko chini sana (significantly p= 0.01) ukilinganisha na wale walioko total lockup! Kwa taarifa za jana Sweden wagonjwa wapya walikuwa walikuwa 407 na vifo 34 na huko Japani hakukuwa na mgonjwa ye yote mpya wala kifo cho chote.

Kwa hiyo inaelekea kuna njia zingine za uenezi wa gonjwa hili ambazo bado hatujazifahamu. Utafiti unaendelea.

2: Uwezekano wa kifo kwa mtu mwenye dalili za gonjwa hili (Case Fatality Rate or CFR):
Hii inakokotolewa baada ya mgonjwa kufikia hatima (closed cases) yaani denominator ni idadi ya waliopona + waliokufa. Ni tofauti na mortality rate ambayo denominator yake ni population yote, yaani pamoja na wale ambao hawakuugua.
Mtu akiugua gonjwa hili inachukua wastani wa wiki nne hadi kufikia hatima. Hivyo wagonjwa wengi bado hawajafikia hatima, they are still active na hatujui hatima zao.

Kwa waliofikia hatima CFR inatofautiana kwa kiwango kikubwa kutegemea na maeneo ya dunia. Sababu yake bado haijajulikana na tafiti zinaendelea. Kwa mfano:
- World death rate (CFR) average is 19% kwa takwimu za jana yaani 40,655 deaths out of 215,014 closed cases.
- Italy ni vifo 12,428 out of 28,157 = 44%
- USA ni vifo 3,431 out of 9,672 = 35%
- Spain ni 8,269 kati ya 27,528 = 30%
- China ni 3,305 kati ya 79,357 = 4%
Hiki ni kiwango kikubwa sana hasa kwenye nchi hizo za ulaya na amerika ambayo haijawahi kutokea.

3. Broad spectrum disinfectants spraying/ fumigation: These are based on their track records against the same type of enveloped viruses such as influenza viruses. Their effectiveness in the control of this pandemic remains to be studied.

4. The role & effectiveness of facial masks:
- The surgical masks do not block out the tiny particle size of the coronavirus or the influenza virus. This is a fact. May simply act as physical barrier like any other material can do.
- The D95 face mask: These block out 95% of the viral particles. You have to be fit tested before wearing them, a specialized process, otherwise they can also do more harm than good. They are single use only and when they start to get wet which usually happens in about half an hour they need to be changed.

Hence the level of protection the existing PPE offers to the people especially those taking care of affected patients remains to be evaluated. We have witnessed a significant number of health personnel being infected by this virus. In Italy for example, by 19 March 2020 at least 2,629 health workers had contacted the disease and more than 60 doctors had died of the disease, representing 8.3% of the total cases. Thi is according to a report published by Italy's Group for Evidence-based Medicine (Gruppo Italiano Basata sulle Evidence or GIMBE).

5. Chanjo (Vaccine): This is the ultimate solution. Uwezekano wa kupata chanjo dhidi ya gonjwa hili inakisiwa kuwa baada ya miezi 18. Ikumbukwe kuwa chanjo dhidi ya virusi vya gonjwa la ukimwi hadi sasa bado haijapatikana. Inawezekana ikawa hivyo hivyo kwa gonjwa hili. Ila uvumbuzi huwa hautabiriki, inaweza kutokea kanjemba kamoja kakaivumbua hata kesho.

6.Ni lini mlipuko wa gonjwa hili utaisha:
Hii nayo si rahisi kuitabiri kama ilivyokuwa kwenye gonjwa la ukimwi na Ebola. Inaweza kuwa hata miaka kadhaa. Pandemic inaweza ikaisha lakini gonjwa likabaki endemic kwa baadhi ya nchi na kusababisha milipuko kila baada ya muda fulani kama inavyotokea kwa kipindupindu hasa kama chanjo haitapatikana. Sasa sijui itakuwaje kwa nchi ambazo zimeamua kuwa kwenye total lockdown kama kwa mfano mlipuko wa gonjwa hili ukaendelea kwa kiwango hiki hiki au zaidi yake kwa kipindi cha miezi 6 au zaidi?

7. Mass testing: Ni muhimu kwani ndiyo itatupa mwanga zaidi ya gonjwa hili. Hadi sasa uelewa wetu ni kuwa zaidi ya asilimia 50% wanaopata virusi hivi hawaugui gonjwa hili. Yaani wanabakia wanabakia kuwa carriers wa kusambaza gonjwa hili bila wao kuathirika na hatuwezi kuwatambua wala wao hawawezi kujitambua bila kufanyiwa vipimpo. Hivyo simple and cheap specific test kits are needed.

8: Chanzo (Origin) ya gonjwa hili:
Bado ni speculations hususani popo na wanyama wengine kama ilivyokuwa kwa HIV na Ebola. Kuna uwezekano wa zaidi ya hapo. Na tukumbuke binadamu wa sasa hivi anaenda sayari zingine kama Mars na Pluto. Wanaporudi huko kwenye hayo masayari mengine wanaweza kuyaleta ya kuleta kwenye hii sayari yetu.

9: Mpango madhubuti wa kitaifa wa kupambana na gonjwa hili unahitajika kama tulivyofanya kwa gonjwa la ukimwi

10. The Hippocrates Oath:
Watu wanalitafisiri visivyo. The protection/ safeguarding of the health of the community is of paramount importance to the doctor than that of the individual patient's secrecy. Daktari hawezi kuachia mgonjwa akaendelee kuambukiza wenzake kwa makusudi gonjwa lo lote hatari. Anawajibika kuitaarifu mamlaka kumchukulia hatua mtu wa aina hiyo.
 
Nafikiri njia wanayotumia Sweden na Japan ndio njia nzuri ya kuepusha maambukizi..

Nimeona video kutoka kwa Dr mmoja huko Mmarekani akielezea nini hasa Corana Virus

Yeye amesema huu ugonjwa hasababishwi na Virus Bali unasababishwa na MIONZI ya 5G technology..

Ikumbukwe kuwa 5G technology imeanzia China,radio radiation,miozi ya 5G ina nguvu Mara kumi ya 4G,hii inazifanya cells kuwa poisoning,inayotengeneza Virus kwa binaadamu

MIONZI ya 5G inauwa cells (cells poisoning)na kufunya mwili wa binadamu kuwa dhaifu,na ndio maana wanaokufa Sana ni wazee na watu wenye magonjwa mengine

Nchi Kama North Korea,Urusi,Cuba nchi ambazo hazijasimika hii technology maafa ni madogo Sana..

Sio Kama joto ndilo linalouwa virusi vya Corona Kama watu wanavyosema,ukweli ni kuwa ultra sun rays ndio zinapunguza nguvu za radio radiation ya 5G ..

Matokeo yaliyoleta Pandemic :-mwanzo wa kuanzishwa technolog ya radio, Radio wave zilileta Spanish flue pandamic,,mwanzo wa kupandishwa equipment za Satalite 1968 Kuna magonjwa yalitokea Dunia nzima,Sasa tuna.5G Corona inatula...
 
Umeeleza vzr sana mkuu kongole kwako. Jua ni muhimu hata kama hawana jua huko basi hata hewa ya nje ni nzuri zaidi.
 
Huyo dr mmoja hana jina?
Nafikiri njia wanayotumia Sweden na Japan ndio njia nzuri ya kuepusha maambukizi..

Nimeona video kutoka kwa Dr mmoja huko Mmarekani akielezea nini hasa Corana Virus

Yeye amesema huu ugonjwa hasababishwi na Virus Bali unasababishwa na MIONZI ya 5G technology..

Ikumbukwe kuwa 5G technology imeanzia China,radio radiation,miozi ya 5G ina nguvu Mara kumi ya 4G,hii inazifanya cells kuwa poisoning,inayotengeneza Virus kwa binaadamu

MIONZI ya 5G inauwa cells (cells poisoning)na kufunya mwili wa binadamu kuwa dhaifu,na ndio maana wanaokufa Sana ni wazee na watu wenye magonjwa mengine

Nchi Kama North Korea,Urusi,Cuba nchi ambazo hazijasimika hii technology maafa ni madogo Sana..

Matokeo yaliyoleta Pandemic :-mwanzo wa kuanzishwa technolog ya radio, Radio wave zilileta Spanish flue pandamic,,mwanzo wa kupandishwa equipment za Satalite 1968 Kuna Kuna magonjwa yalitokea Dunia nzima,Sasa tuna.5G Corona inatula...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo huko China hiyo 5g ipo kwenye mji mmoja tu wa Wuhan au? Mbona miji mingine kama Beijing haijaathirika na huu ugonjwa?
 
Naomba hii ni copy nikapest kwenye uzi fulani
 
Hakika mkuu hili gonjwa ni hatari haina haja serikali kufungia watu wake ndani, inaonekana ni rahisi kuenea na kuua kwa kasi kubwa pindi watu wanapo fungiwa ndani, jaman Mungu atunusulu na huyu ibirisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama tatizo ni mionzi ya 5G sasa kuambukizana kama virus imetoka wapi
You are welcome bro,unaweza kufanya hivyo..

wanasema Corona ni Flue lakini tunaambiwa tuoshe mikono..

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Kwa hiyo huko China hiyo 5g ipo kwenye mji mmoja tu wa Wuhan au? Mbona miji mingine kama Beijing haijaathirika na huu ugonjwa?
Kila wanapoweka minara ya 5G,maafa makubwa yanatokea

Wewe hushangai kwanini huu ugonjwa ukasambaa kwa Kasi hivi?

Juzi wamekufa watu 500 UK, Marekani,Italy na nchi za Western,nchi ambazo zinatumia Sana hii technology ndio muathirika mkuu,

Watu wanaokufa kutokana na huu ugonjwa ni watu wenye ukaribu mkubwa na technology internet,Hospitali,Nyumba za wazee,.nk

Wachina Kuna miji wameandamana na kuanza kuangusha minara inayotumia technology ya 5G

Kuna mengi yamefichwa,.mengi hatutakiwi kujua.
 
Kama tatizo ni mionzi ya 5G sasa kuambukizana kama virus imetoka wapi

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
Kama umesoma na kufamu nini nineandika ulitakiwa usiulize suali Kama hili

Radiation za frequency za technology ya 5G Sina nguvu Mara kumi zaidi ya 4G,mwili wa binadamu hauwezi kuhimili

Kinachotokea,miozi inauwa baadhi ya cells na kusababisha virusi ndani ya mwili wa binadamu,

hii inatokea Sana kwa wale wenye kinga ndogo kwenye miili yao, mafano,wazee na wenye magonjwa mengine, ambao ndio wanaokufa kwa wingi

Radiation zikiisha uwa baadhi ya cells katika mwil wa binadamu na kutengeneza virusi,mtu alieathirika ni rahisi kumuambukiza mwengine.. that's the theory behind it
 
Ugonjwa huu ni mpya. Umeikumba dunia yetu kwa kishindo kikubwa kuanzia mwaka huu. Mgonjwa wa kwanza alitangazwa huko China tarehe 10 Jan 2020. USA walitanganza mgonjwa wao wa kwanza siku 10 baadaye. Zikafuata Ufaransa 23 Jan, Canada 24 Jan, Ujerumani 26 Jan, Finland 28 Jan na Italy 29 Jan. Tarehe 30 Jan 2020 Sweden, Urusi, Sweden, Spain na UK wakatanganza mgonjwa wao wa kwanza. Nchi zingine zikafuata kwa tarehe tofauti tofauti. Hadi leo nchi zaidi ya 202 duniani zimekumbwa na gonjwa hili. Tanzania tulitangaza mgonjwa wa kwanza 15 March yaani wiki 2 tu zilizopita.

Madaktari na watalaamu wengine wa afya ya binadamu na wanyama wamekuwa wakikesha kutafiti gonjwa hili ili kupata suluhisho lake kitiba na kikinga. Kwa muda huu mfupi wa miezi 3 yapo mengi ambayo wameyabaini lakini pia yako mengi ambayo bado hayajajulikana wazi. Hata yale ambayo awali walifikiri yamejulikana, mengine yanaendelea kuonekana aidha yana utata au hayako sahihi. Hii ndiyo kawaida ya utafiti. Na jambo hili la kisayansi haliwezi kuwa la kirahisi rahisi kama kujumulisha mbili na mbili.

Hivyo basi tunapofanya maamuzi ya kukabiliana na janga hili ni vyema tukazingatia ushauri wa watalaamu wetu. Haya mambo si ya kukopi na kupesti toka nchi fulani fulani kama alivyosema spika wa bunge letu. Kunahitajika kuwa na a National Technical Advisory Comittee inayoundwa na madaktari weledi kwenye nyanja mbali mbali zinazoguswa na janga hili eg internal medicine, surgery, epidemiology. Madaktari hawa watoke kanda zote za nchi yetu kama tulivyofanya enzi zile gonjwa la ukimwi lilipoingia nchini kwetu. Hii kamati ni tofauti na ile Technical Nationa Task Force iliyoundwa chini ya katibu mkuu wa wizara ya afya ambayo ni ya utekelezaji/ utendaji wa maamuzi.

Baadhi ya maeneo ambayo bado ni changamoto kwenye uelewa wetu wa sasa kuhusu gonjwa hili ni yafuatavyo:

1. Uenezi wa gonjwa hili (mode of transmission):
Kwa uelewa wetu wa sasa kuhusu mode of transmission ya ugonjwa huu tulitarajia kabisa kuwa mbinu ya total lockdown (wananchi wote kutotoka majumbani mwao) ingekata kabisa uenezi wa virusi hivi ndani ya kipindi cha wiki mbili. Muda huu wa wiki mbili umetokana na uelewa wetu wa sasa kwamba incubation period (muda kutoka kupata virusi hivi hadi kuanza kuugua) ya ugonjwa huu ni siku 0 hadi 14. Na kwamba vijidudu hivi vinauwezo wa kuishi kwenye surfaces (maeneo) mbali mbali kwa siku zisizozidi nne.

Mbinu hii ilitumika kwa mara ya kwanza huko China na ulionekana kufanya kazi sana. Lakini mbinu hii hii huko ulaya na Amerika inaonekana kutokufanya kazi - yaani kwenye hizi mbinu hii badala ya wagonjwa wapya na vifo vipya kupungua, tunashuhudia vinapanda kwa kasi zaidi ya maradufu kila siku. Kwa mfano kwa taarifa za jana huko USA wagonjwa wapya walikuwa 25,948 na vifo 790, Italy wapya 4,782 na vifo 727, Spain wapya 8,195 na vifo 923.

Nchi kama Sweden na Japan ambazo kuwaacha raia wake huru (no total lockdown) wakiendelea kupunga hewa ya nje na kuota ultra violet rays za jua, hadi sasa uenezi wa gonjwa hili uko chini sana (significantly p= 0.01) ukilinganisha na wale walioko total lockup! Kwa taarifa za jana Sweden wagonjwa wapya walikuwa walikuwa 407 na vifo 34 na huko Japani hakukuwa na mgonjwa ye yote mpya wala kifo cho chote.

Kwa hiyo inaelekea kuna njia zingine za uenezi wa gonjwa hili ambazo bado hatujazifahamu. Utafiti unaendelea.

2: Uwezekano wa kifo kwa mtu mwenye dalili za gonjwa hili (Case Fatality Rate or CFR):
Hii inakokotolewa baada ya mgonjwa kufikia hatima (closed cases) yaani denominator ni idadi ya waliopona + waliokufa. Ni tofauti na mortality rate ambayo denominator yake ni population yote, yaani pamoja na wale ambao hawakuugua.
Mtu akiugua gonjwa hili inachukua wastani wa wiki nne hadi kufikia hatima. Hivyo wagonjwa wengi bado hawajafikia hatima, they are still active na hatujui hatima zao.

Kwa waliofikia hatima CFR inatofautiana kwa kiwango kikubwa kutegemea na maeneo ya dunia. Sababu yake bado haijajulikana na tafiti zinaendelea. Kwa mfano:
- World death rate (CFR) average is 19% kwa takwimu za jana yaani 40,655 deaths out of 215,014 closed cases.
- Italy ni vifo 12,428 out of 28,157 = 44%
- USA ni vifo 3,431 out of 9,672 = 35%
- Spain ni 8,269 kati ya 27,528 = 30%
- China ni 3,305 kati ya 79,357 = 4%
Hiki ni kiwango kikubwa sana hasa kwenye nchi hizo za ulaya na amerika ambayo haijawahi kutokea.

3. Broad spectrum disinfectants spraying/ fumigation: These are based on their track records against the same type of enveloped viruses such as influenza viruses. Their effectiveness in the control of this pandemic remains to be studied.

4. The role & effectiveness of facial masks:
- The surgical masks do not block out the tiny particle size of the coronavirus or the influenza virus. This is a fact. May simply act as physical barrier like any other material can do.
- The D95 face mask: These block out 95% of the viral particles. You have to be fit tested before wearing them, a specialized process, otherwise they can also do more harm than good. They are single use only and when they start to get wet which usually happens in about half an hour they need to be changed.
Hence the level of protection the existing PPE offers to the people especially those taking care of affected patients remains to be evaluated. We have witnessed a significant number of health personnel being infected by this virus.

5. Chanjo (Vaccine): This is the ultimate solution. Uwezekano wa kupata chanjo dhidi ya gonjwa hili inakisiwa kuwa baada ya miezi 18. Ikumbukwe kuwa chanjo dhidi ya virusi vya gonjwa la ukimwi hadi sasa bado haijapatikana. Inawezekana ikawa hivyo hivyo kwa gonjwa hili. Ila uvumbuzi huwa hautabiriki, inaweza kutokea kanjemba kamoja kakaivumbua hata kesho.

6.Ni lini mlipuko wa gonjwa hili utaisha:
Hii nayo si rahisi kuitabiri kama ilivyokuwa kwenye gonjwa la ukimwi na Ebola. Inaweza kuwa hata miaka kadhaa. Pandemic inaweza ikaisha lakini gonjwa likabaki endemic kwa baadhi ya nchi na kusababisha milipuko kila baada ya muda fulani kama inavyotokea kwa kipindupindu hasa kama chanjo haitapatikana. Sasa sijui itakuwaje kwa nchi ambazo zimeamua kuwa kwenye total lockdown kama kwa mfano mlipuko wa gonjwa hili ukaendelea kwa kiwango hiki hiki au zaidi yake kwa kipindi cha miezi 6 au zaidi?

7. Mass testing: Ni muhimu kwani ndiyo itatupa mwanga zaidi ya gonjwa hili. Hadi sasa uelewa wetu ni kuwa zaidi ya asilimia 50% wanaopata virusi hivi hawaugui gonjwa hili. Yaani wanabakia wanabakia kuwa carriers wa kusambaza gonjwa hili bila wao kuathirika na hatuwezi kuwatambua wala wao hawawezi kujitambua bila kufanyiwa vipimpo. Hivyo simple and cheap specific test kits are needed.

8: Chanzo (Origin) ya gonjwa hili:
Bado ni speculations hususani popo na wanyama wengine kama ilivyokuwa kwa HIV na Ebola. Kuna uwezekano wa zaidi ya hapo. Na tukumbuke binadamu wa sasa hivi anaenda sayari zingine kama Mars na Pluto. Wanaporudi huko kwenye hayo masayari mengine wanaweza kuyaleta ya kuleta kwenye hii sayari yetu.

9: Mpango madhubuti wa kitaifa wa kupambana na gonjwa hili unahitajika kama tulivyofanya kwa gonjwa la ukimwi

10. The Hippocrates Oath:
Watu wanalitafisiri visivyo. The protection/ safeguarding of the health of the community is of paramount importance to the doctor than that of the individual patient's secrecy. Daktari hawezi kuachia mgonjwa akaendelee kuambukiza wenzake kwa makusudi gonjwa lo lote hatari. Anawajibika kuitaarifu mamlaka kumchukulia hatua mtu wa aina hiyo.
China anaenda kuwa na nguvu zaid kuliko nchi yoyote kwa kuwa ameukubali mpango wa mpinga kristo ndio mana umeanza kwake lkn sasa umeisha na siri anaijua kipindi hiki tutashuhudia Mengi ila walio wa kristo ni kutubu na kuomba usikumbwe na ushswishi wa mpinga kristo ukamuacha Yesu ni wkt wa kanisa kujiandaa na Africa kuinuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sehemu zinapinga hiyo 5G ni kwanini?
Kwa sababu ya madhara makubwa kwa binadamu ni angalia nchi zenye 5g madahara ya corona ni makubwa kuliko nchi ambazo hazna 5g na ndio mana africa maambukiz madogo sababu hatuna 5g nchi nyingi lkn pia kuna uhusiano na mpinga kristo kutawala dunia na china kuitawala dunia kiuchumi kama muombaji wkt huu ni wa kuomba sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Andiko zuli sana juu ya Corona. Hapo kwwnye namba nne nadhani Mda simrefu dunia itakubaliana na Mchina tu kila mtu avae Mask. Maana kama tunakubali virusi vya Corona vinasambazwa kwa majimaji yanayotoka mdomoni kwa mtu ambayo yanakuwa yamebeba hivyo virusi, na tunashauri mtu anapopiga chafya afunike mdomo, kwanini tusikubali kuwa mask inakuwa imezuia majimaji/ mate yasiruke toka mdomo wa mtu mmoja kwenda kwa mtu Mwengine ama kusambaa hewani na kudondoka kwenye surfaces nyingine?

Lock down. Kwanza tuelewane Lockdown haimaanishi watu wanajifungia ndani wote siku 30 bila kutoka hata mtu mmoja.Watu wanawekewa utaratibu ambapo angalau kila mtu anatoka maramoja kwa siku/ wiki kwa mda maalumu kwa shughuli maalumu kisha kurudi Ndani.

Pia Isionekane kwamba China walo Tumia Njia moja tu ya Lock down. Lock down ilienda sambamba na testing kwanza universal temp check kila mtaa utakao ingiablazima wakupime joto, tracing and testing, disinfection ya kila mahali, kutoa elimu ya kujikinga kwa mtu mmoja mmoja. Rapid response ambapo ukihisi unadalili hauendi hospital unapiga simu unafatwa na watu waliojikinga vyema, majumbani kunadekiwa kwa disinfenctants angalu mara mbili kwa siku. applications nyingi zimetengenezwa kuonyesha mgonjwa alipopatikana na suspected route alizopita ili wale wanaotoka wachukue tahadhari na mengine Mengi. Hawajatumia njia moja ni Mchanganyiko wa njia milioni kidogo. Adui mwenyenguvu usiyemjua unampiga kwa silaha zote huchagui silaha ya kumpiga nayo we piga tu. Mpaka sasa china Hauna mask hautembei barabarani wa kuingia kwenye public transport. Nashauri we Vaa mask, Leso, ama chochote kinachofunika mdomo na pua kuwalinda wengine. kila mmoja akimlinda Mwingine tutafanikiwa kuishinda Corina wote kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom