Mapadri watatu wa Kanisa Katoliki jimbo la Same, wamefariki dunia ndani ya saa 72

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
871
1,000
Mapadri.jpeg

Mapadri watatu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Same, wamefariki dunia ndani ya saa 72. Kanisa limesema vifo vya aina hiyo havijawahi kutokea.

Waliofariki wametajwa kuwa ni Padre Ubaldus Kidavuri, Padre Arbogast Mndeme na Michael Kiraghenja, wote wa jimbo hilo. Wawili kati ya hao walifariki ghafla usingizini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo, padre mmoja ndiye aliyekuwa akiumwa na alifariki akiwa katika Hospitali ya KCMC.

Taarifa ya vifo vyao ilitolewa jana na Askofu wa Jimbo la Same, Mhashamu Rogath Kimario.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mapadri hao wanatarajiwa kuzikwa Aprili 17, katika Makaburi ya Mapadri Jimbo la Same.

Taarifa ilisema haijawahi kutokea vifo vitatu vilivyopishana kwa saa 24 katika jimbo moja.

“Jana nilionana na Padri Kidavuri na alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda kuzika wenzie na nikampa pole pale St. Joseph, alikuwa mzima wa afya. Wapumzike kwa amani, amina,” alisema Padre Kimario.

Akithibitisha vifo hivyo jana, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Raymond Saba, alisema kanisa limepokea kwa mshtuko mkubwa kufuatia vifo hivyo vya ghafla.

“Vifo vimetushtua sana maana vimekuwa vya ghafla mno, tulikuwa nao na walikuwa wazima kabisa,” alisema Padre Saba.

Alisema wanatarajia mazishi yatafanyika Jumanne ijayo, Same.
 
Zuwenna

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
1,849
2,000
Mwenyezi Mungu ndio mjuaji kifo cha mwanadam kitakuwaje
hakuna haja yakuanza kujengeana hofu
 
Gambino

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
3,461
2,000
Pole ndugu na jamaa.

Watakua walikua na presha na sukari.

Presha is a silent killer. Unaongea na mtu yuko poa just a couple of hours unaambiwa kafa.

Presha ni hatari kuliko ukimwi.
 
la cezz

JF-Expert Member
Oct 4, 2013
258
250
Poleni mapadre kwa kuondokewa na wenzenu, naamini kila kitu kitajulika it's all about time.
 
dega

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,468
2,000
Hivi mapadri huwa Na makabur yao maalum hawachanganyiki Na waumini?? Na kama ni hvyo ni kwa mantiki gani??
 
Gerasmus

JF-Expert Member
May 23, 2016
401
500
Wapumzike kwa amani amina, kanisa jipeni moyo, Mungu analitunza kundi lake, hakika hatoliacha yatima.
 
JFK wabongo

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
3,891
2,000
Hivi mapadri huwa Na makabur yao maalum hawachanganyiki Na waumini?? Na kama ni hvyo ni kwa mantiki gani??
Wanachanganyika tu, ukienda misioni za zamani utakuta kuna makaburi ya waumini na pia ya mapadre. Ila kwa vile kanisa lina maeneo makubwa kutenga eneo moja kwa ajili ya makaburi siyo vibaya.
 
wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
3,784
2,000
Mapadri watatu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Same, wamefariki dunia ndani ya saa 72. Kanisa limesema vifo vya aina hiyo havijawahi kutokea.

Waliofariki wametajwa kuwa ni Padre Ubaldus Kidavuri, Padre Arbogast Mndeme na Michael Kiraghenja, wote wa jimbo hilo. Wawili kati ya hao walifariki ghafla usingizini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo, padre mmoja ndiye aliyekuwa akiumwa na alifariki akiwa katika Hospitali ya KCMC.

Taarifa ya vifo vyao ilitolewa jana na Askofu wa Jimbo la Same, Mhashamu Rogath Kimario.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mapadri hao wanatarajiwa kuzikwa Aprili 17, katika Makaburi ya Mapadri Jimbo la Same.

Taarifa ilisema haijawahi kutokea vifo vitatu vilivyopishana kwa saa 24 katika jimbo moja.

“Jana nilionana na Padri Kidavuri na alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda kuzika wenzie na nikampa pole pale St. Joseph, alikuwa mzima wa afya. Wapumzike kwa amani, amina,” alisema Padre Kimario.

Akithibitisha vifo hivyo jana, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Raymond Saba, alisema kanisa limepokea kwa mshtuko mkubwa kufuatia vifo hivyo vya ghafla.

“Vifo vimetushtua sana maana vimekuwa vya ghafla mno, tulikuwa nao na walikuwa wazima kabisa,” alisema Padre Saba.

Alisema wanatarajia mazishi yatafanyika Jumanne ijayo, Same.
CCM wamefanya yao tayari..
.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom