Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,316
- 33,125
MAJAMBAZI wenye silaha wiki hii wamevamia nyumba ya Mapadri wa Kanisa Katoliki Changanyikeni, Dar es Salaam na wakarusha risasi kabla ya kutoweka na kompyuta ndogo na baadhi ya nyaraka za padri mmoja, Raia Mwema limethibitisha.
Habari zilizothibitishwa na maofisa wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, zimeeleza kwamba majambazi hao waliokuwa na silaha walivamia nyumba hiyo iliyopo karibu na Chuo cha Takwimu, usiku wa kuamkia juzi Jumatatu.
Imeelezwa kwamba Padri mmoja ambaye eneo lake lilivunjwa na majambazi hao, alinusurika kuuwawa kwa risasi baada ya kuruka na kuangukia katika bonde lilipo kando ya nyumba hiyo, huku majambazi wakiamini kuwa wamekwisha kummaliza kwa risasi.
Akisimulia alivyonusurika, Padri Francis Laswai, wa Parokia ya Kipawa, anayeishi katika nyumba hiyo alisema: Ni muujiza tu maana nilipovunja mlango wa ghorofani na kurukia bondeni, muda huo huo nikawa nimesikia sauti zikisema mmalize na mlio wa risasi ukafuata. Sikujitambua nilijikuta nikiwa bondeni karibu na maji.
Nyumba hiyo inayomilikiwa na Shirika la Kikatoliki la Francisca Capchia, ndimo wanamoishi Mapadri wawili, Laswai na mwenzake Damas Mahali, Buruda mmoja na watumishi wawili ambao wote hawakupata madhara yoyote.
Padri Laswai katika sauti iliyokauka, ameliambia Raia Mwema kwamba mbali ya kuchukua kompyuta hiyo ndogo (laptop) na nyaraka zake muhimu zilizokuwa katika begi la laptop hiyo, majambazi hao waliondoka na simu pamoja na saa zake mbili ambazo alisema hata hivyo zilikua mbovu.
Miongoni mwa vitu vilivyoibwa ni leseni ya kufungisha ndoa, vyeti vya elimu na leseni ya udereva ya Padri huyo pamoja na kamera ya mtumishi wake.
Akielezea jinsi majambazi walivyokusudia kumuua, Padri Laswai ambaye yuko chini ya Shirika la Roho Mtakatifu (Holly Ghost Fathers) anasema; Nilipoangukia bondeni nikasikia mmoja akisema, tayari tumemmaliza, kwa hiyo nikaona nitambae na kuondoka eneo hilo wasije wakagundia niko hai.
Kabla ya kumvamia Padri Laswai, majambazi hao walimbana mtumishi wa nyumba hiyo, Marceli John, ambaye alitakiwa kuonyesha alipo Padri Laswai, na alipowaambia hajui alipo walisikia sauti ya padri huyo na kuamua kuvunja mlango na kumuingilia kabla ya yeye kutoweka kwa kuvunja mlango mwingine.
Marceli anasema; Walianza kuniuliza bosi wangu alipo, nikawaambia hayupo.. kwa kweli sikua najua kama amerudi nikajua yuko Kipawa. Wakaniambia niwape laptop yake na pesa. Mara wakaniambia mbona wameliona gari lake jeupe nje, mara nikasikia sauti ya Padri, na wao wakamfuata huko. Ndipo na mimi nikaenda kujificha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, hakuweza kupatikana jana lakini wasaidizi wake muhimu waliliambia Raia Mwema kwamba tayari taarifa hizo wamekwisha kumkabidhi kwa kuwa wao si wasemaji wa Mkoa huo.
Imeelezwa kwamba wakati tukio hilo likitokea, eneo la Changanyikeni lililopo karibu kabisa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chenye Kituo cha Polisi, hakukuwa na gari la polisi wa doria kama ilivyo kawaida kwa maelezo kwamba gari hilo kwa sasa ni bovu.
http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=2089