Mapadre wa kikatoliki Ujerumani wanaokaidi maagizo ya Kanisa na Kubariki mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,236
9,841
Mapadre wa kikatoliki Ujerumani wanaokaidi maagizo ya kanisa na kubariki mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja.

Baraka hizi hutolewea chini ya kampeni inayosema''mapenzi yanashinda''CHANZO CHA PICHA,EPA-EFE

Kanisa katoliki nchini Ujerumani limeendelea kuonyesha kukaidi maagizo ya makao makuu ya kanisa hilo, kwamba makasisi hawawezi kubariki mahusiano ya watu wa jinsia moja.

Jumapili mapadri wa Kanisa Katoliki nchini Ujerumani, walianza kubariki mahusiano ya kindoa ya watu wa jinsia moja.

Chini ya kampeni waliyoiita 'Love Wins' (mapenzi yanashinda ) iliyoibuka baada ya kanisa Katoliki kutangaza mwezi Mei kuwa Mungu "hawezi kuabudiwa kwa dhambi".

Kabla ya tangazo hilo rasmi kampeni hiyo ilisema: " Wanaoishi kama mume na mke wote wanapaswa mbele ya Mungu - hadharani ".

Hii ni baada ya Papa Francis kusema kuwa anafikiri watu wanaoishi kama mume na mke ambao ni wapenzi wa jinsia moja wanaweza "kisheria ".

Mapadri nchini Ujerumani sasa wanamekuwa wakitoa baraka hizo katika ibada katika makanisa 100 tofauti kwa kipindi cha wiki nzima iliyopita. Baraka hizo zinatolewa katika mikusanyiko ya wazi ya ibada. Hii ni hatua ya hivi karibuni ya Kanisa Katoliki la Ujerumani dhidi ya waraka uliotolewa mwezi Machi na ofisi ya uongozi wa Vatican.

'Kongamano la mafundisho ya imani'' lilisema kuwa mapadre wa kikatoliki hawawezi kubariki mahusiano ya kindoa baina ya watu wa jinsia tofauti kwasababu Mungu " hawezi kubariki dhambi ."Waraka huo uliwaridhisha mahafidhina na kuwasikitisha watetezi wa wapenzi wa jinsia moja, waliobadili jinsia na waliozaliwa na jinsia mbili LGBTQ Wakatoliki kote duniani.

Lakini jibu limekuwa kinyume nchini Ujerumani ambako kanisa la Ujerumani limekuwa msitari wa mbele kufungua mijadala juu ya masuala yanayoibua mjadala kama vile mafundisho kuhusu mapenzi ya jinsia moja kama sehemu ya mchakato wa mjadala na mageuzi.

Makumi kadhaa ya ibada za kanisa za sherehe za kubarikiwa kwa mahusiano ya kindoa ya watu wa jinsia moja yameongeza hali ya wasi wasi baina na mahafidhina na ambao wanataka mambo yaendelee kuwa yalivyo ndani ya kanisa ambao wametaka baraka hizo zikomeshwe mara moja, wakidai sehemu ya kanisa katoliki la Ujerumani linaelekea kuwa mpango.

Papa Francis, ambaye ameongoza mfumo wa kulifanya kanisa kuwa moja tena , tayari amekwisha watahadharisha viongozi wa kanisa hiyo Ujerumani kwamba kanisa linapaswa kubakia kuwa na ushirika na Roma katika mchakato wake wa mamageuzi, yanayofahamikakama "njia ya synodi."

Mjini Berlin, Father Jan Korditschke, kutoka jumuiya ya makasisi wa Jesuit anayefanya kazi ya kuwaandaa watu wazima kwa ajili ya ubatizo na kusaidia kongamano la Mt. Canisius , ataongoza ibada ya kuwabariki wapenzi wa jinsia moja itakayofanyika tarehe 16 mwezi Mei."Nina imani kwamba mapenzi ya jinsia moja sio mabaya, na mapenzi ya jinsia moja sio dhambi ," Korditschke aliliambia Shirika la habari la AP katika mahojiano.

" Ninataka kusherehekea mapenzi ya wapenzi wa jinsia mopja kwa baraka hizi kwasababu mapenzi ya jinsia moja ni kitu kizuri ."

Ndoa za jinsia moja
CHANZO CHA PICHA,EPA-EFE
Kasisi huyo mwenye umri wa miaka 44 alisema ni muhimu kwamba wapenzi wa jinsia moja waweze kujionesha ndani ya Kanisa Katoliki na kupata kuonekana kwa muda mrefu. Alisema kuwa haogopi uwezekano wa athari anazoweza kuzipata kutoka kwa maafisa wa ngazi ya juu wa kanisa au makao makuu ya Vatican.

"Ninaamini kile ninachokifanua, ingawa ni kitu kinachoniumiza kwamba siwezi kukifanya kulingana na uongozi wa kanisa ," Korditschke alisema , akiongeza kuwa "ubaguzi wa kanisa langu unanifanya nikasirike na ninaaibishwa sana na kanisa langu.

"Mkuu wa kongamano la maaskofu wa kikatoliki wa Ujerumani alikosoa uamuzi wa kanisa hilo mashinani wa kubariki mahusioano ya kimapenzi ya za wapenzi wa jinsia moja ambao uliitwa "Liebe Gewinnt" au "Love Wins." Yaani mapenzi yanashinda.

BBC

Screenshot_20210511-205906.png


Screenshot_20210511-205845.png
 
"Hakuna utiifu katika kumuasi mwenyezi mungu "
Mtume Muhammad (s.a.w.)
 
Baraka watoazo ni zao na sio za Mungu. Acha waendelee kujifurahisha.

The world on a slippery slope. Mungu aturehemu tu.
 
"Nina imani kwamba mapenzi ya jinsia moja sio mabaya, na mapenzi ya jinsia moja sio dhambi ," Father Jan Korditschke aliliambia Shirika la habari la AP katika mahojiano.
Inamaana huyu baba askofu hajui kabisa kua samora na gomora waliangamizwa kwa sababu gani?
 
"Nina imani kwamba mapenzi ya jinsia moja sio mabaya, na mapenzi ya jinsia moja sio dhambi ," Father Jan Korditschke aliliambia Shirika la habari la AP katika mahojiano.
Inamaana huyu baba askofu hajui kabisa kua samora na gomora waliangamizwa kwa sababu gani?
Tatizo papa anawachekea mno, watu ushawakataza lakini wabishj timua wakafanye kazi nyingine
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom