Mapacha wawili washukiwa wa ujangili wapigwa risasi, mmoja afariki dunia

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
730
2,957
Ndugu wawili ambao ni pacha wamepigwa risasi na mmoja amefariki dunia na mwenzake kujeruhiwa kwa risasi na askari wa wanyamapori ndani ya pori la akiba la Grumeti wilaya ya Bunda, wakituhumiwa kwa ujangili.

Akizungumza na Mwananchi, kamanda Daniel Shila amesema tayari uchunguzi umeanza kuhusiana na tukio hilo na amemtuma kamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mara kufuatilia kwa kina.

“Kwa sasa sina taarifa kamili za tukio hilo, ndiyo maana nimemtuma RCO kwenda huko, akirudi atanipa taarifa nitakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia kwa kina,” amesema kamanda huyo.

Hata hivyo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nyerere, Tanu Warioba amesema Oktoba 14, 2019 Saa 5 asubuhi, walipokea mwili wa Kurwa Marwa (46) na majeruhi mmoja, Dotto Marwa (46) ambao wote ni wakazi wa Kijiji cha Manjimweru ambao wanadaiwa kupigwa risasi.

“Majeruhi tunampeleka kwenye chumba cha upasuaji jioni hii ili kutoa gololi za risasi ambazo amepigwa mkono wa kushoto na tumboni. Mwili wa Kurwa utafanyiwa uchunguzi lakini nao bado una risasi,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom