SI KWELI Mapacha wanaofanana na alama zao za vidole zinafanana

SI KWELI Mapacha wanaofanana na alama zao za vidole zinafanana

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Je, mapacha wanaofanana na alama zao za vidole zinafanana?
Mana hawa mapacha wanaofanana hufanana vitu vingi sana vipi alama za vidole?
1785665616646.png
 
Tunachokijua
Vinasaba vya mapacha wanaofanana vinafanana, na hivi ndivyo vinavyoamua muundo wa msingi wa alama za vidole.

kwa mfano, kama vidole vyao vitakuwa na michoro ya mviringo, mawimbi n.k. Hata hivyo, DNA pekee haichori alama za mwisho kwenye ngozi. DNA hutoa tu ramani ya ujenzi, lakini mazingira ndiyo yanakamilisha mjengo wenyewe.

Hivyo alama za mwisho za vidole vya mapacha hawa huwa hazifanani kutokana na kupitia mazingira tofauti kwa kiasi fulani licha ya kuwa wapo katika tumbo moja.

Zifuatazo ndizo sababu za kimazingira za wanapokuwa tumboni zinazosababisha kuwa na alama tofauti,

  • Nafasi waliyopo tumboni: Pacha mmoja anaweza kuwa amebanwa zaidi, au yupo karibu zaidi na ukuta wa tumbo la uzazi kulinganisha na mwenzake. Mguso huu wa vidole vyao dhidi ya kuta za tumbo huchonga alama tofauti.
  • Ukuaji wa mifupa na ngozi: Kasi ya ukuaji wa vidole, mifupa, na jinsi ngozi inavyovutika inaweza kutofautiana kidogo sana kati ya pacha mmoja na mwingine. Tofauti hii ndogo hubadilisha mwelekeo wa mistari ya vidole.
  • Vitovu: Jinsi mtoto anavyochezea au kugusa kamba yake ya uzazi hutoa msukumo (pressure) kwenye ncha za vidole, jambo ambalo linaathiri muundo wa alama za vidole.
  • Kugusa maji ya uzazi: Kadiri watoto wanavyosogea na kugusa maji yanayowazunguka tumboni, msukumo wa maji hayo kwenye ngozi zao laini hubadilisha jinsi mistari inavyojichora kwenye vidole vyao. Kila pacha anasogea tofauti.
Back
Top Bottom