kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,307
- 12,602
Ni watendaji wakuu wa Kata wanaopaswa kuwa miongoni mwa watu wa Kwanza kwenye jamii kuboresha maisha ya watanzania, lakini baadhi yao ni chanzo cha kero Kwa wananchi.
Miongoni mwa kero wanazosababisha Kwa wananchi ni pamoja na
1. Kumaliza misitu. Watendaji wanashirikiana na wahalifu kukata mbao, milunda na mikaa na kuharibu misitu. Hata kama wataonekana wakiwasaka wanavunaji misitu kimakosa lengo lao sio kuilinda misitu bali kukamata wahalifu ili wagawane wanachopata.
2. Kuuza ardhi za wanavijiji. Watendaji wanashirikiana na matajiri kutoka mijini kuuza ardhi za wanakijiji.
3. Rushwa. Watendaji Kwa kushirikiana na polisi wananyang'anya haki za wananchi Kwa njia ya kupokea hongo Kwa wakosaji.
4. Watoto wanaopewa mimba shuleni kesi zote zinaishia mikoni mwa watendaji Kwa njia ya rushwa. Wanapokea pesa kutoka watia mimba, wazazi wa mtoto aliyetiwa mimba au waliomuoza mtoto
5. Migororo ya wafugaji na wakulima. Watendaji wanakula rushwa kutoka Kwa wafugaji na wakulima kwenye migogoro ya wafugaji na wakulima.
6. Kutoza ushuru usiokuwa na maelezo au kinyume na maelekezo.
7. Kubambikia wananchi kesi ili watoe hela.
8. Kutoonekana ofisini nyakati za kazi.
9. Kutia ndani wananchi bila utaratibu maalum na makosa makubwa ili ndugu zao watoe hela kuwakomboa.
10. Kushiriana na watendaji wengine kama wakuu wa shule, wakuu wa zahanati, kilimo, wakandarasi kufuja mali za wananchi na serikali.
Hivyo, kama mkutano wa Rais na watendaji hawa utasaidia kupunguza kero hizi za watendaji Kwa wananchi basi maisha ya wananchi yatakwenda kuboreka.