Maonyo Mengine...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,731
40,836
ONYO KUHUSU BAADHI YA BENDI KUWAONYESHA WANENGUAJI NUSU UCHI KATIKA MAJUKWAA YA MUZIKI.

Hivi karibuni Baraza la sanaa la Taifa limeshtushwa na kasi ya mmomonyoko wa maadili ya watanzania kwa baadhi ya bendi za muziki wa dansi nchini kutumia majukwaa ya dansi kwa makusudui kudhalilisha wanenguaji wa kike,kudhalilisha watazamaji na kuwaharibu watoto wadogo kwa baadhi ya wanenguaji wakiwa na vichupi na wanengfuaji kuonekana kuwa nusu utupu.

Baadhi ya wamiliki wa bendi wameiga tabia ya baadhi ya wanamuziki wa nchi jirani kwa kuonyesha wanenguaji nusu utupu.Tabia hiyo imechukuliwa kama biashara katika kumbi za maonyesho ya muziki na mbaya zaidi ni kwamba biashara hiyo haiishii hapo bali imewafikia watoto wadogo kwa kuona dhambi hiyo kupitia vyombo vya habar.Hayo tumethibitisha katika ukaguzi wa kushtukiza uliofanywa na watendaji wa Baraza kati ya tarehe 24/5/2008 hadi tarehe 1/6/2008.

BASATA linachukua fursa hii kuwaaasa wamiliki wa bendi zenye tabia hiyo kuacha mara moja na ikithibitika kuendelea kuvunja agizo hili,bendi hizo zitachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuzifungia kufanya maonyesho au kuzifutia usajili.

Aidha tunawaomba wamiliki wa vyombo vya habari kuacha kuwaunga mkono wadhalilishaji hawa kwa kutoonyesha au kuchapisha picha za wanenguaji waliovaa vichupi ili kulinda maadili yetu ya kutoharibu kizazi chetu ambacho hivi sasa kinaharibiwa kwa kuonyesha watoto mambo ambayo hawastahili kuyaona katika umri walio nao.

Ni nafasi hii pia tunawaomba wanenguaji wakike kuacha kutumika kama chombo katika biashara za watu kwa kudhalilishwa utu wa mwanamke.Aidha BASATA linawaomba wanaharakati wa haki za binadamu,wanaharakati wa masuala ya wanawakae kutokaa kimya katika suala hili,kwani maadili ya watanzania yanapobomolewa umma wa watanzania ndio unaoteketea.

Pia wadau wa muziki tunawaomba zikatae bendi zinazoonyesha vichupi na wasiositiri mwili wa mwanamke hadi watakapobadili tabia hizo,tukiweka tafakari kuwa,watazamaji wangejisikiaje kama binti zao na dada zao wangecheza na vichupi mbele yao.
Tunaamini kuwa biashara ya muziki itafana kwa kuwa ubora wa muziki wenyewe unaoambatana na uzingatiaji wa maadili (mila desturi)na kamwe vichupi havitaupamba muziki mbovu kuwa muziki bora.

Imetolewa na
D.Lauwo
KAIMU KATIBU MTENDAJI
BASATA
2 JUNI,2008
 
Hebu fikiria CCM inamiliki mojawapo ya bendi dizain hii. Ina maana chama kinashabikia muanguko wa maadili ya jamii??? ile bendi ya T-Respect sidhani ni ya Komba ile....
 
This was long overdue?? Halafu we act surprised why there are low levels of respect for women. Watu wakiangalia video hoochies wa MTV wanafikiri thats how music should be danced.
What a system?????
 
loh t respect ya ccm...akudo soundoooo ya kapuya yasemekana, mchinga sound sijui ka bado ipo ya mudhihir mudhihir,twanga pepeta asha baraka woote hao si ni ccm???waanze kutoa boriti kwenye macho yao kwanzaaa
 
Hawa wanawake ni watu wazima na wanafanya kwa hiari yao. Waachwe kama wanataka kuonyesha vichupi vyao. Wengine tunapenda kuviangalia.
 
God point, Bimkubwa, but why start/stop there? Kwa nini wasitoe tu agizo wazuie watu kuangalia TV zote (na MTV, BET, VH1 humo humo)!
Kwa nini wasipige marufuku video za akina Koffi, Wenge, Awilo, n.k.!
Indeed, kwa nini wasipige marufuku hata kwenda beach na swimming pools maana huko pia watoto wataona 'vichupi' vya watu wakioegelea!

Where do we start or where do we stop? Wa-Masai na Wa-Barbaig tunawadharau wakipita na shuka moja, kwani kuvaa suits na jeans ndiyo maendeleo. Hayo maendeleo yakija na mtoto kuvaa vi-mini na vi-chupi mbele ya wazazi, mapaja nje anaangalia video za Beyonce na Twanga Pepeta, tunakuja tena na kelele!

Actually, kule kwetu ambako hawajawahi kuona hiyo MTV huwa wana-dance music akina kaka na akina dada vifua wazi, na baadaye chagulaga. Tofauti tu ni kuwa huwa wanaziita ngoma za kienyeji.
 
loh t respect ya ccm...akudo soundoooo ya kapuya yasemekana, mchinga sound sijui ka bado ipo ya mudhihir mudhihir,twanga pepeta asha baraka woote hao si ni ccm???waanze kutoa boriti kwenye macho yao kwanzaaa

hata kama ni kweli bendi hizo ni za hao viongozi uliowataja, ina maana hilo baraza limepiga marufuku bendi zooote kasoro hizo za viongozi wa ccm ??
 
This was long overdue?? Halafu we act surprised why there are low levels of respect for women. Watu wakiangalia video hoochies wa MTV wanafikiri thats how music should be danced.
What a system?????

kweli kabisa !!
 
Jamani hawa BASATA mbona wanaturudisha nyuma sasa? Wapenda starehe tuko mbioni kupigia chapuo clubs za wacheza uchi nchini. Music nowadays is not all about good vocal, its comes as a package- sura+umbo+ mavazi+ etc.Hakuna mtu anayewashikia bastola hao wanawake wacheze na vichupi, they are adults and ukiwaangalia tu stejini you can tell they love and enjoy what they do.Naweza nikakubali tu kuwe na restrictions kwa watoto kuingia katika kumbi za bendi zinazolalamikiwa na kama ni videos basi ziwe zikirushwa hewani mida ambayo watoto washalala, cammon guys- you only live once!
 
ONYO KUHUSU BAADHI YA BENDI KUWAONYESHA WANENGUAJI NUSU UCHI KATIKA MAJUKWAA YA MUZIKI.

Hivi karibuni Baraza la sanaa la Taifa limeshtushwa na kasi ya mmomonyoko wa maadili ya watanzania kwa baadhi ya bendi za muziki wa dansi nchini kutumia majukwaa ya dansi kwa makusudui kudhalilisha wanenguaji wa kike,kudhalilisha watazamaji na kuwaharibu watoto wadogo kwa baadhi ya wanenguaji wakiwa na vichupi na wanengfuaji kuonekana kuwa nusu utupu.

Baadhi ya wamiliki wa bendi wameiga tabia ya baadhi ya wanamuziki wa nchi jirani kwa kuonyesha wanenguaji nusu utupu.Tabia hiyo imechukuliwa kama biashara katika kumbi za maonyesho ya muziki na mbaya zaidi ni kwamba biashara hiyo haiishii hapo bali imewafikia watoto wadogo kwa kuona dhambi hiyo kupitia vyombo vya habar.Hayo tumethibitisha katika ukaguzi wa kushtukiza uliofanywa na watendaji wa Baraza kati ya tarehe 24/5/2008 hadi tarehe 1/6/2008.

BASATA linachukua fursa hii kuwaaasa wamiliki wa bendi zenye tabia hiyo kuacha mara moja na ikithibitika kuendelea kuvunja agizo hili,bendi hizo zitachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuzifungia kufanya maonyesho au kuzifutia usajili.

Aidha tunawaomba wamiliki wa vyombo vya habari kuacha kuwaunga mkono wadhalilishaji hawa kwa kutoonyesha au kuchapisha picha za wanenguaji waliovaa vichupi ili kulinda maadili yetu ya kutoharibu kizazi chetu ambacho hivi sasa kinaharibiwa kwa kuonyesha watoto mambo ambayo hawastahili kuyaona katika umri walio nao.

Ni nafasi hii pia tunawaomba wanenguaji wakike kuacha kutumika kama chombo katika biashara za watu kwa kudhalilishwa utu wa mwanamke.Aidha BASATA linawaomba wanaharakati wa haki za binadamu,wanaharakati wa masuala ya wanawakae kutokaa kimya katika suala hili,kwani maadili ya watanzania yanapobomolewa umma wa watanzania ndio unaoteketea.

Pia wadau wa muziki tunawaomba zikatae bendi zinazoonyesha vichupi na wasiositiri mwili wa mwanamke hadi watakapobadili tabia hizo,tukiweka tafakari kuwa,watazamaji wangejisikiaje kama binti zao na dada zao wangecheza na vichupi mbele yao.

Tunaamini kuwa biashara ya muziki itafana kwa kuwa ubora wa muziki wenyewe unaoambatana na uzingatiaji wa maadili (mila desturi)na kamwe vichupi havitaupamba muziki mbovu kuwa muziki bora.

Imetolewa na
D.Lauwo
KAIMU KATIBU MTENDAJI
BASATA
2 JUNI,2008

Hivi huyu bwana Lauwo wakati akiandika hii barua alikuwa anawaza nini?

Kutoa onyo ni tofauti kabisa na kuasa au kuomba.

Sijui anaweza kujifunza kuandika tena hizi barua!, aandike upya barua ya onyo bana.
 
Binafsi hata sielewi msingi wa onyo hili ni nini? kama alivyosema Kiungani kwanini tuchague kutoa onyo kwa wachezaji wa bendi hizi wanaocheza live mbele ya watu 1000 lakini wale wanaooneshwa kwenye TV mbele ya ya watu 100000 hatutoi onyo? Kama kweli kuna kitu kinaitwa "maadili ya Watanzania" wangeanza kwa kupiga marufuku TV, MTV na VH na video kibao za bongo flava ambazo ni suggestive?

Wakimaliza hapo itabidi wapige marufuku vikundi vya ngoma za jadi ambazo wachezaji wake wanacheza kwa "kukatikiana" kama zile za Wamakonde, lizombe, n.k Halafu ni lazima wapige marufuku "mduara" pia kwani pamoja na kuwa watu wamevaa nguo lakini jinsi wanavyocheza ni staili ya "nakutia majaribuni"..

Kama kweli wanataka kuloinda maadili na kutokuwadhalilisha wanawake (hadi hivi sasa sijasikia mwanamke ambaye anacheza hivyo kwa vile ameshindwa kisu shingoni!) basi wahakikishe kuwa wanawake hawaruhusiwi kuvaa kaptula za kubana au tsheti za kubana; na zaidi ya yote suruali/sketi ambazo zinaonesha jinsi dada "alivyojaliwa" nazo zipigwe marufuku....

Na wakiamua vizuri nadhani itabidi waombe jeshi la Polisi lianzishe kitengo cha "Polisi wa Maadili" ili wawe wanapita mitaani na kuona ni nani amevaa au anacheza visivyopaswa ili achukuliwe hatua za kisheria.
 
Pia baada ya hapo waingie vichwani mwetu na kutuzuia kuwaza/kutamani mambo hayo pia waende katika mtandao na kublock all adult-related content kisha wamtafute Brazameni na baraza lake wamuimpeach kisha waende kwa Lundenga na timu yake,kisha wawafuate wasukuma na Chagulaga yao kisha wawazuie DSTV&GTV na channels zao kisha...kisha...kishadamn BASATA kama hamna cha kusimamia why can't you stop squandering our taxes?
 
Hawa wanawake ni watu wazima na wanafanya kwa hiari yao. Waachwe kama wanataka kuonyesha vichupi vyao. Wengine tunapenda kuviangalia.

Sio kwenye public places.
kama wanataka kuvaa hivyo kuwe na leseni maalum ya maonyesho yao, ili watu wajiandae kuwa ni ya watu wazima, tu.
 
Pia baada ya hapo waingie vichwani mwetu na kutuzuia kuwaza/kutamani mambo hayo pia waende katika mtandao na kublock all adult-related content kisha wamtafute Brazameni na baraza lake wamuimpeach kisha waende kwa Lundenga na timu yake,kisha wawafuate wasukuma na Chagulaga yao kisha wawazuie DSTV&GTV na channels zao kisha...kisha...kishadamn BASATA kama hamna cha kusimamia why can't you stop squandering our taxes?

duh ulivyogagadafua hiyo report yake na kumpa further more steps za kutake...loh mie hoiii!!kweli ndugu una uchungu na tax ulipazo na starehe zako!
 
This was long overdue?? Halafu we act surprised why there are low levels of respect for women. Watu wakiangalia video hoochies wa MTV wanafikiri thats how music should be danced.
What a system?????

Nawashangaa wanaharakati wa gender wapo kimya kuhusu hili. Wanafurahia kuona mabinti wakidhalilishwa majukwaani? Mbona wanenguaji wa kiume hawapandishwi jukwaani wakiwa nusu uchi
 
Back
Top Bottom