Maonyesho ya Saba Saba yanawanufaishaje Watanzania?

asha ngedere

Member
Nov 6, 2009
92
11
Wakuu,
Kwa miaka mingi Watanzania tumekuwa tukisherehekea maonyesho ya Saba Saba. Huko vijijini Saba Saba ni sikukuu kubwa sana tofauti na wale wa mijini wanavyoichukulia. Lakini katika uhalisia wake, sikukuu hii imebadilika na kubaitizwa jina la maonyesho ya biashara ya kimataifa.

Msingi halisi wa kuanzishwa kwake umeondoka na badala yake sasa wahusika wanaangalia pesa zaidi kwa washiriki (makampuni nk.) na tozo la watu wanaoingia. Kinachoendelea huko ni upuuzi mtupu kwa sababu hakuna elimu yoyote ambayo wananchi wanaweza kujifunza zaidi ya kukutana na biashara za washiriki ambao wanataka kufidia gharama walizolipa.

Hivi tuseme ukweli ndugu zangu, kuna haja ya kuendelea na maonyesho haya kwa msingi ule ule wa awali ama yabadilishwe kwa namna nyingine?

To me this is just a bs
Mwenye hoja achangie.
 
Hayo maonyesho yalisha kufa rasmi. Nyerere, CCM na sabasaba vilikufa siku nyingi, kilicho baki sasa ni usanii mtupu.

hadi mifupa yake imeshaoza kabisa, bora hata soda ya 7up kuliko saba saba ya majizi ya sasa. ukienda kule utakuta mabepari tupu asaivi.
 
Back
Top Bottom