Maonyesho 77 Yafinyangwe Kuleta Tija Zaidi

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,059
903
Maonyesho ya kimataifa ya biashara ya sura nyingi kimalengo na kimkakati.
Tukiwa taifa changa na lenye kiu ya kupiga hatua maonyesho ya biashara yana mantiki kubwa katika kutangaza fulsa za uwekezaji,fulsa za nini kinazalishwa nchini na nini tunahitaji toka kwa wenzetu wenye teknolojia ndogo na kubwa.

Inasikitisha kuona bado kuna mapungufu mengi ya kimfumo,kiusimamiaji na kimalengo ya maonyesho ya biashara ya 77 ambayo uasisi wake ulidhamiria yawe ya wakulima na wafugaji.

Mosi,Mpangilio wa mabanda ya maonyesho hauakisi mapana yenye tija kwa washiriki wa maonyesho kwa kuwa shaghalabagala.

Pili,Mseto wa bidhaa,teknolojia,huduma zionyeshazo unachosha watembeleaji wenye malengo mahususi na si kuzurula kwa kutapakaa .

Tatu,Maonyesho yamekuwa yakibeba dhima ya gulio kiutekelezaji hivyo kugubigwa na uchuuzi wa bidhaa zaidi tofauti na maonyesho ya kimataifa kama Canton Fair ambapo waonyeshaji hulenga kuonyesha ubunifu,utofauti,ubora,n.k

Nne,

NINI KIFANYIKE.

  1. Kufanyike usanifu mpya wa uwanja wa maonyesho wa 77 utakaoakisi maudhui ya maendeleo ya sayansi,teknolojia na mahitaji yenye malengo ya kimkakati {Tanzania ya Viwanda}.Uwe mpya,wa kisasa,Ukiwa na huduma mtambuka mahsusi kwa kuwakuza wafanyabiashara wa ndani.Parking,B2B Conferences,Digital Showrooms,Beautiful Sceneries,Recreational Spaces..
  2. Tantrade ihusike na utoaji huduma zenye ubunifu zaidi katika kusaidia sekta ya biashara,viwanda,uzalishaji.Tantrade iwe na weredi zaidi wa kutengeneza miradi wezeshi kwa wefanyabiashara,wajasiliamali na kuwa daraja la taasisi za kimataifa,makampuni ya nje yenye uwezo.
  3. Maonyesho yawe na lengo la kuhamasisha washiriki wa kimataifa kuwekeza nchini {viwanda,uzalishaji} na kuepuka kuwa wauzaji tu wa bidhaa.Katika hili ndoa ya taasisi mkakati kama TIC,EPZA,BRELA,TRA,CTI,TPSF,TCCIA ni muhimu ili kufikia malengo mtambuka.
  4. Mapinduzi ya fikra,maono,dhima ya TANTRADE ni muhimu katika kuunda upya dira mahsusi ya ujenzi wa uchumi wa kujitegemea na si kutegemea kuagiza bidhaa.Kutengeneza mazingira wezeshi ya kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa ndani kwa ubora zinapata masoko ndani na nje.
  5. TANTRADE iweke ofisi katika kanda za viwanda kama Mkuranga,Kibaha,Chalinze n.k ili kuwa mhimili wa karibu katika kutatua changamoto za wawekezaji wa ndani na nje.
 
Sawa mkuu unaongea na watanzania wanaoisoma namba kumbuka
 
Back
Top Bottom