Maonyesh ya sababa 2008 na kasheshe zake

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
25
Maonyesho ya sabasaba ya mwaka huu yalionyesha ubora zaidi ya yaliyotangulia. Maonyesho ya sabasaba yanaliingizia taifa fedha nyingi sana.Na pia maonyesho haya hutoa ajira ya msimu kwa watanzania asilimia fulani.

Tatizo la maonyesho ya saba saba ni jinsi ya watu kuingia uwanjani hapo ili kujionea biashara zilizoletwa kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya Tanzania. Lengo la makampuni mbalimbali na mashirika kuleta bidhaa ni ili kujitangaza. Ninashindwa kuelewa ina maana wanaoratibu shughuli za maonyesho hayo wanashindwa kubuni njia ya kupunguza msongamano wakati wa maonyesho hayo.

Mimi binafsi ni mdau wa biashara ila nilishindwa kuingia uwanjani siku yenyewe ambayo ni tarehe saba kwani watu walikuwa wengi mlangoni wakigombea kuingia uwanjani. Ninashauri pawepo na utaratibu wa watu kukata tiketi sehemu nyingine na si lazima iwe siku hiyo ya maonyeho ili kupunguza msongamano.
 
Last edited:
Back
Top Bottom