Maono ya Hayati Magufuli bado yanaongoza nchi, huenda na Rais Samia ameshaambiwa

abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
1,436
2,292
Baada ya kuangalia Bunge la Jana na kila hoja Ya mbunge Alie simama kuitoa nilihis Matumain mapya Kwan Wabunge Jana walifanikiwa kutuma ujumbe mzur kwa Watanzania wazalendo wenye kuipenda nchi yao na kwa Asilimia 100% Bunge la Jana lilikua Mwiba kwa wezi wa Rasilimali ZETU na vibaraka wa Mabeberu.

Bungeni Jana palikuwa ni sehemu iliyojaa maono ya Magufuli na pongezi nyingi sana zilienda kwa Hayati, Mungu amlaze mahali pema peponi Amina.

Kwa misimamo walioonyesha wabunge jana nina imani waliokuwa wanataka kuichezea hii nchi baada ya Mzee kuondoka Watakuwa tayari wamekosa nafasi na mama atakuwa ameshaambiwa maana imeonekana lazima miradi yote alioanzisha Hayat lazima iendelezwe pia Na ndege lazima zinunuliwe na Mungu akipenda Tunajiandaa kupokea Ndege Tatu.

Kwa situation ilio onekana Jana ni wazi kabisa Baada ya Hayati kutangulia Kuna team Mafisadi walitaka kurudisha nchi katika upigaji Ndio maana hata Ripot za CAG zilikuwa zina upotoshaji mkubwa juu ya mradi aliyoifanya Hayati na yote tunajua ilikuwa tu kuhalalisha mambo yao ya hovyo hasa ule wa Bagamoyo mana Jana nimemsikia mpaka Zitto anausifia ila hatushangai toka mwanzo Zitto tunamjua alikuwa Mpambe wa Mzee na yeye ndie aliempa hela za chama.

Yaani Zitto eti tuikubali Bandari ya Bagamoyo kisa tu Kuna mimeli mikubwa itakuwa inakuja hatujawahi kuiona.

Nalipongeza Bunge kwa kutokubali kufuata upepo wa Mafisadi na kuamua kusimamia nchi wale waliotaka kumchafua Magufuli now naona wamevimba vibaya pia Mama tunakuomba acha kufungamana nao watakupoteza hao ndio walikusaidia ukapata nafasi ya Umakamu ila sio kigezo hicho cha kuwatekelezea matakwa yao Mabaya juu ya nchi yetu.

Kumbuka we are watching you.
 
MATAGA mnaishi kwa matumaini mpaka mnatia huruma! Hata huyo magufuli wako nae alikuwa ni mpigaji tu!

Kiufupi huwezi kuwa kwenye ukoo wa panya (CCM), halafu usiwe mpigaji.
 
Mleta mada rejea kauli ya Kibajaji kuwa asilimia 100 ya wabunge walikingiwa kifua na SHUJAA kuwa wabunge, logically ni kwamba walisifu na kuabudu kwa kuwa walijua Ubunge na matumbo yao kavishika SHUJAA.

Nakuhakikishia SAMIA anajua vyema wapi pakuwafunga midomo ili waanze kuelewa kwamba hii ni awamu ya sita, Rais ni yeye na anayo maono yake pia.

Ubunge wa CCM unategemea HISANI ya Mwenyekiti wa chama + dola.
 
Mleta mada rejea kauli ya Kibajaji kuwa asilimia 100 ya wabunge walikingiwa kifua na SHUJAA kuwa wabunge, logically ni kwamba walisifu na kuabudu kwa kuwa walijua Ubunge na matumbo yao kavishika SHUJAA...
Ok tujipe muda kidogo
 
Sioni kama Jina la JPM litaachwa kuandikwa hapa iwe Kwa wema au vinginevyo, Je, hii ndio Ishara ya ushujaa wake na mambo mengi mazuri aliyofanya?
 
Back
Top Bottom