MAONO: Uongozi wa TZ baada ya uchaguzi wa 2015 utakuwa hivi;Rais Sita,vice Mbowe,PM Slaa..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAONO: Uongozi wa TZ baada ya uchaguzi wa 2015 utakuwa hivi;Rais Sita,vice Mbowe,PM Slaa.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OLEWAO, Jan 27, 2012.

 1. O

  OLEWAO Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Dalili sasa ni dhahiri shahiri kuwa CCM haiwezi tena kuhimili anguko linalotokana na minyukano iliyosababishwa na utawala wao kufitinika Lakini baya zaidi ni kwamba kwa haya wanayowatendea waja wake inaonesha kwamba hata Mungu hawamuogopi.

  OLEWAO! Maandiko matakatifu yameshasema tangu kale kuwa utawala wowote ukifitinika hauwezi kusimama.

  Sisi sote ni mashahidi wa hali hiyo ndani ya ccm.
  Hali hii haijatokea kwa bahati mbaya bali ni huruma ya Mungu kwa watanzania baada ya kuona hakuna namna iwayo yote ccm wanaweza kuwaongoza watz kuelekea kwenye nchi yenye neema.

  Alichowafanyia ni kama alivyofanya Babeli (sasa Iraq) wakati walipojazana ujinga na kuamua kujenga mnara ambao walidhani ungewafikisha kwa Mungu! Kilichotokea wasomaji wa maandiko matakatifu mnajua.

  Kwa kuwa Mungu ndiye chanzo cha mabadiliko ya kweli ya utawala wa wanadamu, ANGUKO la ccm litakuwa hivi;
  Wafuatao watajitoa ccm na kujiunga CHADEMA (chama mbadala wa ccm) Samwel Sita, Magufuli, Nape na Mwakyembe.
  Baada ya uchaguzi 2015 utawala wa juu utakuwa hivi;

  1. Rais - Samwel Sita
  2. Makamu - Freeman Mbowe
  3. W/Mkuu - Dr. Slaa
  4. Spika - Tundu Lissu
  5. W/M/Ndani - Dr. Magufuli
  6. Jaji Mkuu - Dr. Mwakyembe
  6. W/U&Fedha - Zitto Kabwe, n.k
  7.W/N&Madini - John Mnyika

  Na wapiganaji wote watapewa majukumu; Kweli hapo hatutoki?Mafisadi watapona? Tusubiri tuone.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. k

  kiche JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kwa katiba tuliyonayo sitta hawezi kuwa rais na mbowe makamu labda tu uniambie mbowe au sitta mmoja wao atakuwa ameamua kuwa mzanzibar,na sidhani hata katiba mpya kama itatengua kifungu hiki kwani ni kizuri katika kulinda muungano,na hapo kwa mwakyembe sina uhakika kama itawezekana kutokana na taarifa za ugonjwa wake.
   
 3. M

  MPG JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo Sita hafai kuwa rais mana katika jimbo lake 2 la Urambo mashariki hakuna lolote alilofanya,Urambo ni wilaya maskini kupita kiasi,amekuwa Mbunge kwa vipindi tofauti, mpaka leo ameweza kuwa Mbunge kwa miaka 22 kwanzia mwaka 74 mpaka 95 jimbo likaenda upinzani kwa miaka 5,2000 akachukua karafina wa CCM,yeye Sita akarudi tena 2005 mpaka leo,2012
   
 4. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tuone hali itakuwa vipi hapo 2015
   
 5. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Lakini hii mara nyingine hiki ni kitu kizuri kwa mwanasiasi husika, kwani majimbo mengi yaliyoendelea yametokana aidha na utajiri binafsi wa wabunge husika au wabunge hawa kufanikiwa kuwa mawaziri hivyo kupelekea maendeleo kwao badala ya maeneo mengine pengine yanayohutaji msaada zaidi.

  Ni majimbo machache sana yameendelea kutokana na mbunge wake kupiga piga kelele bungeni juu ya umaskini kwenye jimbo lake. Naomba nitajie jimbo moja ambalo limeendelea kwa njia hii, ambapo mbunge wake (wa CCM), hana uwezo wa kiuchumi, lakini kelele zake zimezaa matunda jimboni.

  Serikali huwa haijali sana hili, especially huko miaka ya nyuma. Kwa hali ya sasa kuna uwezekano, especially majimbo yaliyo chini ya upinzani kwa sababu mbali mbali kama vile, CCM kujaribu kuyachukua, lakini pia kutokana na jitihada binafsi za wabunge husika, ndani na nje ya bunge. Naomba nitajie yale chini ya Chama tawala ambapo serikali ya CCM imekubaliana na kilio cha mbunge husika hivyo kupelekea maendeleo ya maana jimboni.

  Vinginevyo Urais Sitta 2015 atakuwa Mzee sana; it needs mtu wa umri wa miaka 60 maximum, but that's in my view.
   
 6. S

  STIDE JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante kwa thread yako, lakini nahisi umesahau CDM ilivomakini, ni ngumu na haitopata kuwa rahisi mwanachama kutoka ccm ahamie CDM alafu ndani ya miaka 2 ama 3 agombee Uraisi!!

  Hilo sahau mkuu!! CDM pamesheheni vichwa timamu hawawezi kumkaribisha mtu mchumia tumbo kama 6 alafu eti agombee Uraisi, hata U-mwenyekiti wa BAVICHA hapati yule!!

  Alafu Mwakyembe kwani amepona?
   
 7. k

  kicha JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 532
  Trophy Points: 180
  hivi inawezekana kwa chama kinachojiita makini kumkubali mtu kwa mda mfupi tu mpaka kugombea uraisi? wakati ndie huyu huyu anaeitwa mnafiki kila kukicha, mda mwengine nashindwa kuewaewa chadema, nahisi na wao ndo walewale tu wanasubiri zamu yao tu watulize tena wa tz.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni maandiko matakatifu hayo hayo yanayosema kutakuwa na manabii wa uongo kama wewe. Aidha maandiko hayo hayo yanasema kuna wanafiki kama wewe.

  Ni maandiko hayo hayo yanayosema binadamu hana nafasi ya kumhukumu binadamu mwenzake kama unavyofanya. Hivi Chama tawala kinafitinika au kinafitinishwa kwa sababu tu kiko madarakani? na kwa sababu gani umesema Rais atakuwa SItta na siyo Mbowe au SLaa ?

  Hii ni picha ya wazi kuwa hao wawili bado hawana uwezo ukilinganisha na viongozi wengi tu nje ya chama hicho ambao hata huyo SITTA mwenyewe uliyempa hadhi hiyo hawafikii kwa kwa robo. Uongozi siyo kuongea bali ni kutenda. Kama ni safu ya viongozi waongeaji basi uko sahihi , lakini kama ulikuwa na maana ya viongozi watendaji pole.

  Watanzania wameshapembua mbivu na mbichi, Ukiniteulia watu kama SLAA, LISSU, MBOWE na SITTA kweli siwezi kwenda kupiga kura. Wachochezi/wanafiki/waongo/ wenye uchu wa madaraka sana. Mungu atuepushe na viongozi wa aina hii.

  SLAA si alikataa kwenda kwenye sherehe za kuapishwa Rais kwa maelezo kwamba hakubaliani na matokeo, iweje aende ikulu kuonana na Rais huku akimkwepa kwenye mikusanyiko mbalimbali, anaogopa nini wakati siyo Rais wake?

  Tafsi yake ni husuda(kitu kibaya sana hiki, ogopa sana mtu mwenye husuda anaweza kukua pale malengo yake yanaposhindwa kufikiwa). Nakumbuka wakati wa kampeni za urais pale jangwani LISSU alitoa document ndefu kweli kwamba sijui JK alimkosea nini wakati anasoma nje, kwa nini leo hii haendi mahakamani kwani kwa jinsi tunavyomfamu LISSU ni mtu anayejidai kuwa mwasheria mkali kweli ameshindwa nini kufanya hivyo, japo kwenye Kongamano la Katiba mpya pale Chuo kikuu Prof. Shivji alimuumbua pale alipokurupuka kuchangia mada bila kufuata misingi ya sheria. Majungu hayo, chuki binafsi.

  Kwa hiyo mimi naamini kuna viongozi wanafiki na hao huwa sifa yao kuu ni kuongea ili kupotosha umma
   
 9. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Iko kinafiki saana, typical nightmare in the jungle. Maake kuna kuama kwa Sitta, Magufuri na n.k, Muungano kuvunjika, Viongozi wa CDM kumkubali Sitta na Watanzania kumpigia Sitta kuwa Rais.....blaa...blaaaa.
   
 10. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Magufuli kuhamia CHADEMA? Nyie mnaodhani Magufuli ni mkweli mnaota. Magufuli ni opportunist. Anazo ndoto za urais na yuko tayari kwa unafiki wa kila aina ili aweze kutimiza ndaoto yake.

  Njia aliyoamua kutumia ni kujionyesha kuwa ni mchapa kazi na mwenye uchungu na nchi. Lakini hilo halikumzuia kuuza nyumba za serikali kifisadi.

  Kuna maamuzi mengi amefanya ambayo yameishia kulitia taifa hasara kuliko kulisaidia (samaki wa Magufuli, Kituo cha mafuta Mwanza, bomoabomoa isiyo ya haki, n.k). Magufuli atahamia CDM pale tu atakapohakikishiwa kuwa mgombea wa urais na si vinginevyo.

  Hana itikadi. Kusema kweli magufuli akija CDM yatatokea yaliyotokea Lyatonga Mrema alipohamia NCCR-Mageuzi au Shibuda alipohamia CDM. Si dalili njema.
   
 11. y

  yaya JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, kwa uchambuzi wako huu tufanye wewe unafaa kuwa Rais wa TZ!!!????
  Kwa dhana kama hizi itabidi tuombe UN waturudishie Waingereza, ili turudi kuwa chini ya uangalizi wao mpaka atakapopatikana Nyerere mwingine.
   
 12. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  wazo la mzee 6 kuhamia airtel(cdm)ni jema ila kugombea urais mmh au mmesahau yale ya DOVUTWA F na kombat zake lakin kumbe alikuwa mfukon wa JIKE I!
   
 13. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbona WAGALA tupu na kibaraka mmoja? No wonder muslim community does not trust this GANG of thugs!
   
 14. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwa hiyo unamaanisha kuwa tz particularlaly cdm hakuna anayefaa kuongoza nchi jampo kwa miaka mitano tu?. Je ulitegemea kwamba dr. Slaa aendelee kuijenga bifu kwa jk aliyepitishwa na tume ya uchaguzi bila ridhaa ya wtz waliowengi? Kama majibu yako kwa maswali haya yatakuwa ndiyo basi huelewi siasa nini! Hakuna mtz asiyejua udhaifu wa jk. Jk anashaushika saidi kama ataongeleshwa kwa lugha ya kutongozwa lakini siyo kwa mabavu. Dr slaa anajua hilo. Jk mambo mengi ya nchi hii hayajui kwa hiyo anaongoza nchi kwa kudura za mwenyezi Mungu. Dr slaa anajua hilo, ndiyo maana hakuidumbukiza nchi kwenye machafuko ya wenyewe kwa wenyewe 2010. Dr slaa amemheshimu mjinga aiepushe nchi balaa. Busara ya dr slaa ndiyo inayokufanya uendelee kuiona tz kuwa kisiwa cha amani. Wakati mwingine tuheshimu na kujali busara za watu badala ya kuibeza kana kwamba siyo kitu. Mungu ibariki tz Mungu mbariki Dr. Slaa kwa kuonyesha busara iliyotukuka katika siasa za tz!!!
   
 15. Abastian

  Abastian JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2016
  Joined: Sep 28, 2015
  Messages: 556
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 60
  Duuuuuh!!!!! sijui ingekuaje??
   
 16. M

  Mbase1970 JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2016
  Joined: Jun 11, 2015
  Messages: 3,221
  Likes Received: 2,011
  Trophy Points: 280
  Asante kwa thread yako, lakini nahisi umesahau CDM ilivomakini, ni ngumu na haitopata kuwa rahisi mwanachama kutoka ccm ahamie CDM alafu ndani ya miaka 2 ama 3 agombee Uraisi!!

  Hilo sahau mkuu!! CDM pamesheheni vichwa timamu hawawezi kumkaribisha mtu mchumia tumbo kama 6 alafu eti agombee Uraisi, hata U-mwenyekiti wa BAVICHA hapati yule!!

  Alafu Mwakyembe kwani amepona? hii nimeikopi kutoka kwa moja wa mwana CDM nashangaa umakini wao uliishia wapi walipomteua mtu baada ya kuwa mwanachama kwa masaa 24
   
Loading...