Maono: Namuona Tundu Lissu akiachana kabisa na siasa na kujielekeza kwenye kazi ya Mungu!

Utasubiri sana Lissu kupanda madhabahuni. Hujui kuwa kazi anayoifanya sasa ni maagizo ya Mungu na ndio maana akasema "mwanangu Lissu hutakufa ila utaishi upate kuwatumikia watu wangu dhidi ya hawa viongozi washirikina, wauaji na mafisadi hadi kieleweke'
Mkono was Mungu tumeuona dhidi ya risasi 38
Wameshaanza kuogopa baada ya kugundua kuwa Lissu yu hai na yupo tayari kuwataja waliokusudia kumuuwa
 
Moja ya mambo au sifa kuu za Mungu ni HAKI, atahubiri haki kwa kila mtanzania. haki ni kinyume na dhuruma na udicteta uchwara. Tundu Lissu atapigania wanyonge na walio nyimwa na kudhurumiwa haki zao.
 
Na ajabu ni kuwa hadi leo hii hao majambazi hawajakamatwa
Lissu mwenyewe anaharibu upelelezi anasema anawajua,dereva nae kajichimbia hukohuko,tuwasubiri wawataje kupitia mkanda maalum wa video
 
Lissu sio Dkt Ulimboka!

Unadhani Dr.Ulimboka alinyamaza??Unakijua alichokiandika na kumuachia Mwanasheria wake akipresent wakati kesi ikiendelea??Je Serikali ilimwita Dr.Ulimboka au Mwanasheria wake??Kama hapana basi usikiseme usichokijua.
 
Kwa namna alivyopita katika tanuru la kisiasa na misukosuko yote ile, namuona Tundu Antipas Lissu akiachana kabisa na mambo ya siasa na kwenda kutoa ushuhuda wa yale Mungu amemtendea. Ni kwa neema ya Mungu tu Lissu alipona katika tukio lile la kijambazi, hivyo ana kila sababu ya kwenda kuihubiri injili ya uponyaji. Chadema wamwache Lissu na familia yake sasa ili wapate fursa ya kuwa na maamuzi yao kama familia na chama kirudi huku duniani kuendelea na shughuli za siasa zilizosimama kwa zaidi ya mwezi sasa!

Lile halikuwa tukio la kijambazi bali la kigaidi.
 
Thubutu! Lissu aachane na siasa wakati 2020 anatarajiwa kupambana na Dikteta Uchwara kwenye kinyang'anyiro cha urais. Huyu ndo anakwenda kumrejesha Sizonje kwenye uchungaji wa ng'ombe kule Chatou.
 
Kwahiyo wewe unawalaani?
Mimi nawalaani wale waliompeleka Nairobi Hospital, hospitali ghali afrika na ufujaji wa fedha uliofuatia,wakati Muhimbili wangefanya kazi yote bila kutembeza bakuli la mchango.
 
Aachane na siasa? Hayo yatakuwa maono ya kishetani maana hata huko kwenye siasa ataweza kutangaza enjili!! Sasa hivi kisiasa TALM anang'ara hawezi kuachana na siasa!!
 
Kwa namna alivyopita katika tanuru la kisiasa na misukosuko yote ile, namuona Tundu Antipas Lissu akiachana kabisa na mambo ya siasa na kwenda kutoa ushuhuda wa yale Mungu amemtendea. Ni kwa neema ya Mungu tu Lissu alipona katika tukio lile la kijambazi, hivyo ana kila sababu ya kwenda kuihubiri injili ya uponyaji. Chadema wamwache Lissu na familia yake sasa ili wapate fursa ya kuwa na maamuzi yao kama familia na chama kirudi huku duniani kuendelea na shughuli za siasa zilizosimama kwa zaidi ya mwezi sasa!

Mbona mama Lwakatare haaichi siasa?
 
Mimi nawalaani wale waliompeleka Nairobi Hospital, hospitali ghali afrika na ufujaji wa fedha uliofuatia,wakati Muhimbili wangefanya kazi yote bila kutembeza bakuli la mchango.

Baadaya kuwalaani umepata faida gani?

MBWIGA.jpg
 
Mimi nawalaani wale waliompeleka Nairobi Hospital, hospitali ghali afrika na ufujaji wa fedha uliofuatia,wakati Muhimbili wangefanya kazi yote bila kutembeza bakuli la mchango.
Kajinyonge basi wewe ndubwi
 
Back
Top Bottom