Ryan The King
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 2,788
- 2,690
Habarini Wakuu!!
Kama kichwa kinavyojieleza nimeona nitumia fursa hii kuungana na nyie kwaajili ya kuangazia yale machache yatakayoweza kutokea katika miaka ya 2030 kuendelea.
Nikiwa Kama kijana mdogo Mara nyingi huwa nafikiri na kuangalia kasi ya ulimwengu ambayo kwa mtu makini lazima ishughulishe fikra zake.
Hakuna ubishi kuwa mpaka sasa Maisha ni Magumu japo bado yapo matumaini kwa kiasi Fulani. Ugumu huu wa Maisha unachagizwa na utolewaji wa elimu ambao haukidhi haja ya watu kukabiliana na mazingira. Tumeona jinsi ongezeko kubwa la vijana wenye elimu ya kizungu wanaozurura huku na huko kutafuta ajira bila mafanikio yoyote.
Elimu yetu kwa sasa sio tena mkombozi bali imegeuka mzigo wa msumari kwetu. Hakuna jambo la maana kwa vijana wanaopata elimu hii zaidi ya kuongea kingereza ambacho hata hicho nacho kimekuwa cha makengeza.
Hata hao waliotangulia kusoma Mara baada ya Uhuru hakuna la maana watakaloweza kujisifu mbele ya kizazi chetu na kizazi kijacho zaidi ya kuungana na Wazungu kuuza Rasilimali za taifa hili.
Kwa namna hii basi matokeo ya elimu itolewayo tunayaona Leo na kizazi kijacho kitazidi kuathirika zaidi Kama elimu hii haitafanyiwa marekebisho makubwa.
Ifikapo kuanzia mwaka 2030 nayaona maisha yaliyomfano wa kuzimu.
Nawaona vijana wa kitanzania wakinyanyasika katika nchi yao. Japo kwa sasa kwa kiasi watu hunyanyasika lakini miaka kuanzia 2030 Kama hapatakuwa na mabadiliko ya hali ya sasa basi nawaona vijana, wazee, Wanawake na watoto wakiteseka katika mateso Makuu.
Sababu kubwa ya mateso ni ukosefu wa Maarifa. Kwani elimu itolewayo haina uhusiano na changamoto za kimazingira yanayowazunguka.
Mtu fulani huweza kujisemea moyoni huenda Mimi ni mpiga ramli au nabii wa uongo lakini ukweli ni kuwa miaka hiyo maisha yatabadilika Sana.
Katika kujadili jambo hili watu wenye akili lazima wazingatie mambo yafuatayo;-
1. Ongezeko kubwa la idadi ya watu.
2. Mabadiliko ya tabia ya nchi.
3. Falsafa na mitizamo ya watu kuhusu maisha.
4. Sera za mataifa makubwa kuhusu nchi za ulimwengu wa tatu.
- Sera za kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, kijamii n.k.
5. Teknolojia na maarifa ya wakati husika.
Jambo ambalo watu makini watakuwa wanalifikiria ni suala la ongeko la watu. Mataifa makubwa yaliyoendelea huliangalia hili kuliko jambo lolote lile.
Hata kwa hapa Tanzania watu makini hawana budi kulizingatia jambo hili.
Ongezeko la watu huleta ushindani zaidi katika maisha. Watu hushindania rasilimali zilizopo ambazo huenda zikawa chache. Kwa nchi yetu ya Tanzania tumebarikiwa rasilimali nyingi Sana Kama vile Ardhi, madini, Wanyama, watu, maji n.k.
Embu fikiria ikiwa tupo watu 50Mil lakini maisha ni magumu unadhani maisha yatakuwaje tukifika watu 100Mil.
Jibu kila mtu analo.
Kuongezeka sio tatizo bali tatizo lipo katika suala la utoaji wa ujuzi na maarifa kwa jamii.
Watu wengi hukimbilia Mjini(sio tatizo) lakini wanapaswa kujua kuwa wameacha rasilimali ardhi ambayo kwa miaka ya 2030 itakuwa mshike mshike kuipata. Huenda mjini kukodi chumba au nyumba kwaajili ya kuishi. Hawanunui ardhi pindi wawapo vizuri kiuchumi jambo ambalo litawagharimu watoto wao ambao kwa ligi ya miaka ya 2030 hawataiweza. Wengi wao watakuwa wamekata tamaa kuliko wazazi wao waishio zama za sasa.
Ni Lazima mwenye akili anielewa kuwa ardhi ni muhimi sana. Nunua kwa kadri uwezavyo kwa maana mambo ya baadae ni mshike mshike.
Naiona Tanzania yenye vijana Mashoga na Wasagaji waliopindukia.
Japokuwa serikali inapinga jambo hili(Sahihi) lakini miaka ya 2030 naona Ndoa za jinsia moja zikihalalishwa.
Hii ni kutokana na sababu nyingi tuu.
Kwanza kabisa ni ukosefu wa lishe ya asili ambayo ni hatari kwa miili ya wanadamu.
Pia suala la serikali ya sasa kupuuzia vile vijana wanavyojiamulia mambo yao ya mitindo ya maisha kwa mfano kutembea uchi, wanaume kutoboa masikoo na kuvaa hereni, serikali na jamii kuruhusu Wasichana na wavulana kujiingiza katika michezo yenye dalili hatarishi za umalaya, ushoga, na usagaji Kama mashindano ya Umiss, Fashion, umodo. N.k.
Jambo hili litafanya kizazi cha miaka ya 2030 kuona mambo hayo ni utamaduni wetu kumbe sio.
Miaka hii naiona Tanzania katika ukosefu wa amani. Unaotokana na vijana kukosa ajira, maisha magumu yaliyokisiri, ukosefu wa maadili, uonevu na dhuluma, ukiukwaji wa haki za binadamu n.k.
Ukosefu wa Amani utaanzishwa na vikundi vya vijana mahali mahali nchini ambavyo kipindi hiki tumezoea kuona vijana wasio na elimu Kama vile panya road, Mbwa mwitu(Dar es salaam) n.k lakini miaka hii vikundi hivyo vitakuwa na vijana wasomi wenye taaluma zao na wengine waliopata mafunzo ya kijeshi.
Kutokana na uwepo wa njaa na upungufu wa Chakula matukio mengi ya uporaji yataongezeka. Mvua hazitakuwa za Mara kwa Mara hivyo serikali yapaswa kutafuta maarifa na ujuzi wa kutumia kilimo cha umwagiliaji, kuchimba visima vya maji kutoka ardhini na kuyageuza kuwa maji mazuri kwa kilimo Kama yatakuwa na chumvi Sana.
Jambo hili litasaidia.
Machafuko mengi yatasababishwa na ongezeko la watoto wa mitaani ambao wazazi wao iwe wamekufa, wametengana, au maisha magumu katika familia.
Sababu kubwa inayooneka ni kuwa wanawake wengi katika miaka hii watakuwa single Mama kutokana na kudai haki sawa kwani wengi watakuwa wanajishughulisha na shughuli za uzalishaji mali tofauti na wanaume ambao watakuwa hawana kazi.
Taifa linapaswa liangalie mambo haya kwa kina kabla hayajatokea kwani mambo haya yanazuilika.
Je wewe unafikiri nini kitakuwepo Tanzania miaka ya 2030?.