Maoni: Zoezi la kukamata CD, DVD feki lifanywe kwa uangalifu mkubwa

kanyarukwetu

Member
Jul 31, 2014
80
95
Zoezi la kukamata Cd,Dvd kwaa maana kwamba feki linaathiri uchumi wa vijana kwa kukamata mali zao ,serekali ichunguze vizuri ,tatizo sio cd fake tatizo ni juu ya tafsri ya filamu hizo, kwa kuwa watanzania wengi hawajui lugha ya kingereza kichina kihindi na kifaransa ,ndipo tunapata tatizo, shida amabayo inapelekea wasanii wa kitanzania kulalamikia kazi zao hazinunuliwi kufuatia uingizwaji wa filamu za kigeni ambazo kwa asilimia mia moja zinakonga mioyo ya watanzania zikiwa na maudhui ya kutosha pamoja na mbinu za kisasa zinazokwenda na wakati.

Ijulikane ,Mnamo mwaka 2005-2006-2007 filamu za kigeni zilianza kuingia kwa mfumo wa Bru-ray Disc Dvd hizo zilikuwa na uwezo wa kubeba filamu 10 hadi 20,
soko la bongo movie nalo lilikuwa limepamba moto kwelikweli enzi za kina Marehemu kanumba na ray kulikuwa na ushindani ambao ulipekea mpaka Bongo movie ikaanza kuvuka mipaka ndani na nje ya nchi,watanzania pia walitaka kutizama filamu hizo za kigeni lakini ,zilikuwa na lugha ambayo walipata shauku ya kujua kinachozungumziwa ni nini katika filamu hizo ndipo ma dj nao wakaanza kutafsir kutoka enzi hizo mpaka leo ,baada ya ubunifu kupungua kwenye bongo movie na picha za kigeni kupata umaarufu, ndipo kesi inaanza hapa mtu ameona ofsi yake imeenza kudolola anawapa shida mamilioni ya watanzania wanao lipa kodi,kwa kubeba computer zao. inafika hatua mpaka hata haamini TRA ambao wanatoa stika ,ambazo watanzania wanalipa kodi ,lengo lake movie za nje zisiingie nchini,Sasa kama movie zenu hazina kiwango na zama zimebadilika mtawalazimisha watanzania kuzitizama picha ambazo hazina maadili? acheni kuwapa watanzania stress katika kipindi hiki kigumu. kwa hiyo Msama wewe unatafuta ugari peke yako acha kuvurugia watanzania TRA toka zamani wakikuta unafanya biashara wanahimiza ulipe mapato na ndio wengi wanafanya hivyo

kama TRA wanatoa stika na bado unakataa.unadai maafisa wanahonga unataka msaada gani
Kama swala linalenga serekali ipate mapato hiyo kazi waachie TRA.
ikiwa siku hizi msanii wa kitanzania akitoa wimbo wake jambo la kwanza lazima uaweke
youtube ambapo pia hupata pesa nyingi ,watu hupakua wimbo huo kwenye simu au computer na anatumia pesa ,pia kuna huyu ambaye simu yake haina uwezo anataka pia
ausikilize itabidi aende akachangie pesa kidogo


zamani mwaka 2007-2008 -2009 kulikuwa na DVD original Brue-ray disc ambazo zilikuwa na uwezo wa kubeba movie 15 na zaidi ,na subtitle yake ilikuwa english french na chinese ziliwapa shida watanzania kutafsiri ndipo ma Dj wakaanza kuzidurufu ili kila mmoja ambae alikuwa na kiu cha kujua filam hizo au picha hiyo inazungumziwa kitu gani
wamefanya kazi kubwa sana ,huku pia soko la bongo movie wakati ule lilikuwa na mashindano kweli kweli ,enzi za akina ray na kanumba, mpaka wakatambulisha nchi yetu kimataifa zaidi.
leo watu wameecha kulima wanakimbilia mjini kuwa wasanii , mpaka wakati movie zinajaa kwa week movie zaidi ya 30
kitendo ambacho hata HOLLYWOOD huko malekani hawafanyi hivyo


jambo mhimu zama zimebadilika ,wabadilike ,waache mara moja kuchukua mali za watanzania, Msama nenda nje ya nchi ukajifunze kwa nini kazi zenu hazinunuliwi
zungukeni hata kwa watanzania mchukue maoni kwa nini watanzania wanapenda kazi za nje kuliko za ndani?
 

kumteme

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
285
250
Mkuu sio wauza Cd tu mpaka waingiza nyimbo computer zao zinachukuliwa na wao pia
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
51,323
2,000
Hawa wanataka kulazimisha watu wangalie hawa wapaka poda bongo movie yenyewe hawana kbiti kbsa

Ova
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
41,439
2,000
Wewe unajua Blu-ray au unajisemea tu? Hizo kopi feki za kariakoo unaita Blu-ray? Kwanza ukiwa blu-ray player original ukiweka hizo dvd za kichina inagoma kuonesha inakuandikia hii ulioweka ni pirate hairuhusiwi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom