Maoni yenu jf... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni yenu jf...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tiger, Dec 8, 2009.

 1. T

  Tiger JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kuna wachumba walio kwenye uhusiano kwa muda wa zaidi ya mwaka sasa,
  mwanaume anafanya kazi na ana miradi midogo pamoja na mipango ya muda mrefu ya investment.
  Mwanamke aliwahi kusoma chuo fulani lakini hakumaliza() na hivyo yuko nyumbani
  tu kwa sasa.
  Jamaa huwa akimuuliza kuwa unafikiri utakuwa tayari lini kufunga ndoa? mamaa amekuwa akisema ngoja kwanza nisome ili na mimi nipate kazi niwe na uwezo wa kukusaidia kutafuta.
  Ukweli ni kwamba jamaa yuko makini sana na mikakati ya kimaisha kuhakikisha kuwa familia yake tarajiwa itaishi katika furaha na amani(financially,spirtually & emotionally). Mara nyingi amekuwa akimuhakikishia "my wife" wake mtarajiwa kuwa "we gonna make it a worth family hata kama kwa sasa huna kipato as i have a lot of plans to share with you".
  Pamoja na kumpa mifano hai ya hizo plan bado binti ansisitiza kuwa na kipato chake kwanza.
  Jamaa anchoomba kusaidiwa ni kwaba kati yao wawili kuna mtu ana mtazamo
  mbaya au wote wawili au wote wawili wako sahihi?


  Kutokana na jibu ulilonalo unamshuri au kuwashuri nini?
  Tafadhalini jamani hii siyo hadithi ya kutunga, ushauri wenu ni wa muhimu sana.
  Kwa kuwatoa shaka wachangiaji hawa wawili wanapendana sana kwa mujibu wa kauli na matendo yao wenyewe. hakuna shaka kabisa ila shida yao ni mtazamo tu.
   
 2. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Huyo binti ni mchaga nini??? Angekuwa binti ni mkwere au wa kule Tanga tayari angeitikia mwito wa kuolewa bila kujali uwezo wa mwanaume achilia mbali future prospect yake!!!

  Binafsi naona binti ana kitu kinamtia shaka, anahisi atanyanyasika (pengine kuna dalili anaziona kutoka kwako). Kwa sababu anaweza kutafuta kitu cha kumuingizia kipato hata akiwa ndani ya ndoa tayari.

  So issue ya kusoma na kupata kazi kwanza haina mashiko!!! Ladies miaka hii wako very strategic, beware man!!!
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  mwambie jamaa ampeleke chuo, then amuoe mapema akiwa chuo huko huko.vinginevyo pamoja na jamaa kuwa na mipango mizuri ya maisha na anajituma huyo dada bado anatafuta yalipo majani mabichi (green pastures).siku hizi wasumbufu sana, hawa watu mtu unatoka nae mbali unamtunza, lakini siku moja anakutosa. pia mwambie huyo jamaa yako aangali sana maana anaweza kupoteza hata mwelekeo wa vimiradi vyake.kimsingi huyo dada hajamkubali kihivyo huyo jamaa yako ndio maana anapiga dana dana. kwa nini aliacha chuo huko nyuma huyo dada?
   
 4. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ....Kwanza nampa hongera huyu dada ana msimamo na anathamini future yake.
  Huyu dada mie naona yupo sahihi kutaka kuolewa kipindi ambacho tayari ana kazi yake, hivyo huyo jamaa kama mshiko unamruhusu anaweza kumsaidia huyu dada kwenda chuo, kipindi huyu mdada yupo chuo jamaa naweza kumuoa kipindi hicho.

  Kama kweli huyo kaka anampenda huyo dada, ampeleke chuo maana atakuwa kamuhakikishia elimu ili baadaye aje kupata kazi.
   
 5. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kama wanapendana na wakiweka pamoja kipato wanaweza kula na kulala basi waoane tu...kuongeza kipato ni maisha ya kila siku as long as we all live, elimu haina mwisho, mambo ya chuo nk yanaweza kufanyika ndani ya ndoa...mi huwa sielewe kwa nini watu wana kataa kuolewa na wanaowapenda ati mpaka wapate kazi...wengine wanasingizia ati hawataki kuanza kupata watoto mpaka wapate kazi kwanza wakati huo huo tayari wanaishi kama mke na mume wakipeana unyumba na benefit nyingine zoote za ndoa..
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Huyo mwanamke hajamkubali jamaa 100%, kuna doubts fulani hapo, wanawake bwana kwenye situation kama hizo huwa hawasemi ukweli. Kuna dada mmoja nafanya nae kazi alikuwa na mwanaume ambae ametimia kila idara upande wa majamboz tu huyo dada alikuwa anasema hamfikishi, ila kazi nzuri pesa matunzo alikuwa akiyapata vizuri, jamaa alikuwa tayari kumuoa wakati wowote ulee demu akikubali, lkn demu kumbe ana jamaa yake ni mwanafuzi alikuwa anasoma UD yeye ndo kampenda yule jamaa balaa anasema fimbo yake si mchezo, demu alikataa kuolewa na yule jamaa, yule jamaa wa UD akamaliza pale akaenda nje kusoma akarudi demu bd alikataa kuolewa na jamaa na mpaka sasa ni wachumba. na yule mwanafunzi wa UD na yeye keshapata kazi so in near future watafunga ndoa. Kuna vitu huyo jamaa hamridhishi huyo mwanamke. ndo maana kuna msemo unasema mwanamke akisema A na maanisha B. anaposema anataka mpaka asome inawezekana kuna mtu anasubiriwa hapo siku ya siku jamaa ataambiwa nakwenda labda Dodoma au somewhere else kumbe demu ndo anaenda olewa, jamaa awe makini sana na demu sio mipango mizuri, kipato, na maisha mazuri yanamvutia mwanamke.
   
 7. T

  Tiger JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2009
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Naomba kurejesha shukurani za dhati kwa wote waliochangia kwa niaba ya ndugu yetu mpendwa.
  Nitamfikishia jamaa ushauri wenu wote na yeye mwenyewe atabaki kuufanyia kazi.
  Pia Mungu akipenda nitawaletea feedback siku moja.

  Asanteni nyote kwa busara zenu na Mubgu awabariki.
   
 8. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  My young sister is looking for security, na kwa namna fulani anahisi kama jamaa hayupo commited. Katika akili ya kawaida, kama kweli wamepandana ningetarajia huyu mshikaji amuwezeshe huyo dada kumalizia elimu yake. Ni kweli, kuna risk behind it, kv kuna mijamaa kibao ambayo ilikuja kutemwa na mademu wao baada ya kuwa wameshawagharamia elimu. I hope uchumba wao si huu uchumba wa mjini( mnajuwa wenyewe peke yenu, labda na washikaji, halafu mnaitana wachumba-kumbe mtu na girlfriend/boyfriend wake!). Na kutokana na magutugutu anayoonesha huyo sister, kuna kila dalili kwamba ni uchumba wa town. Kama ndivyo, basi waweke mambo hadharani, waweke uchumba official, jamaa atoe mahari na mamo yote muhimu kisha afunge nae ndoa muda mfupi kabla au baada ya kuanza chuo. Naamini anachohitaji huyo dada sio kazi kwanza, bali competitive edge ili hata baadae akija kubwagwa, aweze kusimama mwenyewe!
   
Loading...