Maoni Yangu: Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Chombo Huru Kiutendaji. Ninayo Maajabu Nane (8) ya Tume ambayo Hayazungumzwi

Uwazitu, Tume ya Uchaguzi haismamii Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ule uko chini ya TAMISEMI.

Tume hainawahi kumwamru Mkurugenzi kusababisha Vurugu. Dhima kuu ya Tume ni kuhakisha kuwa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unakua huru na wa Haki.

Aliyemtangaza Nape, Mbowe na Matiko, Zitto na Komu ni si hao Wakurugenzi?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
hauendi kufa mkuu, unaenda kufanyiwa majaribio tu kwa ajili ya kuikomboa dunia na janga la corona.
Twende wote, maana nimegundua hata wew kwa upande unaousimamia huna hoja.

Mimi nimesema Tume ni huru katika Mambo hayo 8,na kueleza. Wew unasema si huru, hoja niende Ufaransa kutest Corona. Mipaka imefungwa, wakifungua twende wote Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuomba wew, useme Uhuru wa Tume unanitafsiri kwa angle ipi? Na uje na elimu yako, ili nami niweze kujifunza kutoka kwako!

Sent using Jamii Forums mobile app

Ibara ya 74(1) ya JMT inasema kuwa Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:-

(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;

(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;

(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.

Kama wajumbe wa Tume ya ya uchaguzi wanateuliwa na Rais wa Tanzania, je huo uhuru wa Tume unatoka wapi?

Unafikiri hao wateuzi wake watatenda kinyume na matakwa ya mteuzi wao ambaye ni Rais wa Tanzania?

Tungesema kuwa kuna uhuru wa Tume ya Uchaguzi endapo kungekuwa na mambo haya:-
1. Kuna usawa wa uteuzi wa wajumbe hao.
2. Wajumbe wasiteuliwe na Rais.
3. Wajumbe wa Tume ya uchaguzi wateuliwe kutoka vyama vyote vya siasa yaani kila chama kitoe wajumbe wake watatu .

KATIBA MPYA NI SULUHISHO LA KUDUMU.
 
Ulitaka nani akasimishwe majukumu hayo ili uamini kuwa yupo huru? Anapovaa kofia ya mtendaji ktk tume ya taifa, automatically ile inampa mamlaka ya kutimiza majukumu yake kwa uhuru uliondani ya katiba (usio holela)!

Shida unapomuangalia mkurugenzi wa wilaya kwa jicho la ukurungezi pasi kuangalia majukumu mapya anayotekeleza muda huo kama mtendaji ktk tume ya taifa ya uchaguzi!
 
RAYAN THE DON, Vyama vikiwa 100 wajumbe nao wawe 100 . Mpaka Mwaka Jana Uchaguzi kulikuwa na Vyama 22 vyenye usajili wa Kudumu, kwa hiyo wawepo wajumbe 22?

Mfano, hata Katiba Inayopendekezwa bado imempa Jukumu Rais, kuteua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume.

Wajumbe waliopo Sasa Kuna Mmoja anatoka Chama Cha Wanasheria Tangayika.

Kwa hiyo ndugu yangu, Mimi kwa namna Sheria zinasomamia Uchaguzi zilivyo, sioni tatizo kwazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani mkapa kakushikia akili, hebu elezea kivipi unaamini tume haiko huru?
 
Lugumgya,
..sasa kwanini sasa hivi wajumbe wanatoka chama kimoja tu, CCM?

..katika hivyo vyama 22 kwanini wasitoke walau ktk vyama 5?

..CCM kwanini mnakuwa WABINAFSI namna hii?
 
Lugumgya,
Kwanza, sheria hizo zina loopholes nyingi sana mkuu. Hivyo hufanya uchaguzi kutokuwa haki na huru kwa sababu wajumbe wa Tume ya uchaguzi wao wenyewe haupo huru. Hawapo huru kwa sababu wanaogopa kutenda kinyume na mteuzi wao(Raisi).

Pili, hao wajumbe waliotajwa na katiba ya JMT wakitenda kinyume na matarajio ya mteuzi wao watalisha nini matumbo yao? Bila shaka lolote kuna uwezekano mkubwa wa kutotenda haki ili kutetea vibarua vyao.

Tatu, huyo mjumbe anayetoka TLS aondolewe ili wajumbe wachaguliwe toka vyama pinzani bila kujali wingi wa vyama vya siasa vilivyopo nchini.

Mwisho, jaribu kufuatilia mchakato wa upatikanaji wa wajumbe wa Tume ya uchaguzi kule Marekani linganisha na taratibu za huku TZ ndipo utagundua kuna tuna sheria za hovyo pamoja na tume ya hovyo.
 
Ndugu hicho kitu kinaitwa 'dilution effect'! Uwiano wa idadi ya watz ambao ni wanachama wa ccm vs nyamba vingine ni kubwa sana, ccm inao wanachama wengi sana ukilinganisha vyama vingine vyote kwa mpigo.

Kwa hiyo uwezekano wa wateule wa tume ya uchaguzi kuwa wanachama wa ccm ni mkubwa mno, na hivyo siwezi shangaa hata kama niliambiwa karibu wajumbe wote ni wanachama wa ccm!

Kigezo cha uanachama ktk kuteuwa wajumbe wa NEC hakina mashiko(unreliable) kwani hata uzoefu wa miaka ya hivi karibuni umetufundisha jinsi kigezo cha uanachama wa mtu usivyotegemewa(not reliable) kwani watu wameshuhudiwa kuhamahama vyama.

Kwa hiyo ni jambo jema sana katiba haikuruhusu swala la uanachama wa mtu kuwa kigezo cha kuteuliwa kwenye NEC, bali utanzania wake ambao hauwezi badirikabadirika!
 
NdgJoka kuu, idadi kuwa ya wajumbe NEC kuwa wanachama wa ccm Ndugu hicho kitu kinaitwa 'dilution effect'! Uwiano wa idadi ya Watanzania ambao ni wanachama wa ccm vs vyama vingine ni kubwa sana, ccm inao wanachama wengi sana ukilinganisha vyama vingine vyote kwa mpigo.

Kwa hiyo uwezekano wa wateule wa tume ya uchaguzi kuwa wanachama wa ccm ni mkubwa mno, na hivyo siwezi shangaa hata kama nilkiambiwa karibu wajumbe wote ni wanachama wa CCM!

Kigezo cha uanachama ktk kuteuwa wajumbe wa NEC hakina mashiko(unreliable) kwani hata uzoefu wa miaka ya hivi karibuni umetufundisha jinsi kigezo cha uanachama wa mtu usivyotegemewa(not reliable) kwani watu wameshuhudiwa kuhamahama vyama.

Kwa hiyo ni jambo jema sana katiba haikuruhusu swala la uanachama wa mtu kuwa kigezo cha kuteuliwa kwenye NEC, bali utanzania wake ambao hauwezi badirikabadirika!
 
Hero,
..asante.

..una HOJA nzuri tu.

..lakini hoja ulizotoa hazihalalishi tume ijazwe wanachama wa ccm, na vyama mbadala visishirikishwe kabisa.

..mimi nadhani kulitakiwa kuwe na USHIRIKISHWAJI wa wadau wengi zaidi ktk tume, na hatua zote za uchaguzi.

..CCM mnapaswa kuelewa kuwa hii nchi ni ya Watanzania wote, na siyo nyinyi peke yenu.
 
Kikubwa nilichojifunza ni hilo jina la Lugumya ni neno la KISUKUMA lenye maana ya mtu Bahili.
Haya maneno alisikika mpemba mmoja anasema wakati anakunywa alkasusu.
 
Lugumgya,
Kwani unaomba kukosolewa,nani alikufundisha halafu aje kukukosoa.Jikosoe mwenyewe kwani hata unachozungumza huku hukijui.Wewe hukumbuki wala huoni unajifanya unaona kwa kutokuona,na unajifanya husikii kwa kutosikia wakati unasikia ila hutaki kusikia wala kuelewa.

Hapo nimekuchanganya kidogo.Ila baadaye utaelewa tu.Kumbuka lugha hii.Nimekupa magari,dola unayo,ole wako utangaze mpinzani kashinda.Wewe kwa akili yako kubwa Tume hii ni huru.

Tena koma kuandika ujinga huku.Mwenzako alikuwa hivi hivi,juzi katudanganya eti anaachana na fani yake akavalishwe rangi ya mchicha akagombee ubunge siasa.Alikuwa anaandika ujinga kama huu naona wajinga wenzake wanataka kumfadhili.Nadhani na wewe uliona na wewe umedandia.Pole subiri kuitwa
 
Back
Top Bottom