Maoni yangu: Tofauti kubwa ya Serikali ya Rais Magufuli na ya Kikwete kwenye pesa

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Kwa maoni yangu tofauti kubwa sana iliyopo kati ya Serikali ya Rais Magufuli na ile ya Raisi mstaafu Kikwete ni kuwa Raisi Kikwete alikuwa ana uwezo mkubwa wa kuzitafuta pesa za ndani na za nje na kuzipata lakini kwenye matumizi matumizi mengi yalikuwa ya hovyo hovyo kama Raisi Magufuli anavyosema mara nyingi kuwa huko nyuma kulikuwa na matumizi ya hovyo hovyo ambayo yeye Raisi Magufuli kayaziba.

Tukija kwa Raisi Magufuli yuko vizuri mno kwenye matumizi ya pesa .Matumizi ya hovyo hovyo hayapo au yamepungua.Kwenye kubana matumizi na matumizi ya pesa yuko vizuri mno lakini kwenye uwezo mkubwa wa kutafuta na kupata pesa za ndani na nje uwezo ni mdogo ndio maana hadi waziri wa fedha Mpango analalamika kafika mahali naye kama waziri ka STUCK!!!!

Ufumbuzi kwa maoni yangu Timu ya Kikwete bingwa wa kutafuta pesa za ndani na nje ziungane na timu ya Magufuli mabingwa wa kutumia vizuri pesa zlizopatikana za ndani na nje waunde timu moja ili mambo yaende.Tuna mengi tumejiifunza kwa Magufuli mazuri na mabaya na kuna mengi tumejifunza kwa Kikwete mazuri na mabaya.Lakini kwa maoni yangu Raisi anahitaji watu wa team Kikwete wamsaidie hasa kwenye eneo la kupata pesa za ndani na nje .Hili eneo ni nyeti na wataalamu wake ni wachache mno,Akiwapata hata wakitaka mamilioni awalipe tu wamsaidie.Mzee Kikwete chonde chonde mpe timu yako ya wataalamu wabobezi wa maswala ya kupata pesa za ndani na nje ya nchi wamsaidie Raisi Magufuli.
 
Jiwe alishasema wastaafu waache vihere here wakae wale pensheni zao.
Kwa hulka hio sidhani kama kuna timu ya JK wanaweza kujitolea kufanya kazi na huyu jamaa.

Kumbuka kwenye kuzisaka pia kuna kuzitumia pia, hapo ndipo kwenye utamu wa fedha.
Mentality hiyo Jiwe hana.
Kutumia yeye anaona ni ubadhirifu, wakati kutumia pesa ni kuzungusha pesa.
 
  1. Kununua wapinzani ili waunge mkono juhudi ndo matumizi mazuri?
  2. Kurudiarudia chaguzi kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu ndo matumizi mazuri ya pesa
  3. Kuyeyuka kwa Trilion 1.5 ndiyo matumizi mazuri ya pesa?
  4. Ujenzi wa uwanja wa ndege Chato nayo ni matumizi mazuri ya hela?
  5. Vipi kuhusu kutumia pesa nje ya bajeti na bila kuidhinishwa na bunge, kwako ni matumizi mazuri ya pesa?

kama kuna matumizi mazuri ya pesa
  • mbona wafanyakazi hawalipwi nyongeza na kupandishwa madaraja kwa mujibu wa sheria za kazi?
  • mbona wakulima wa korosho hawalipwi?
 
  1. Kununua wapinzani ili waunge mkono juhudi ndo matumizi mazuri?
  2. Kurudiarudia chaguzi kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu ndo matumizi mazuri ya pesa
  3. Kuyeyuka kwa Trilion 1.5 ndiyo matumizi mazuri ya pesa?

kama kuna matumizi mazuri ya pesa
  • mbona wafanyakazi hawalipwi nyongeza na kupandishwa madaraja kwa mujibu wa sheria za kazi?
  • mbona wakulima wa korosho hawalipwi?
Wana kumbukumbu fupi sana hawa watu
 
Hela za ndani? Mbona Magufuli anakusanya hela nyingi za ndani (kodi) kuliko Kikwete?

hahahahaaha mpaka makusanyo ya mageti ya stand,na hela zote za halmashauri zinaenda kwake.. Mwenzie hizo zilibaki hukohuko halmashauri na matumizi yalipangwa huko huko.. Alitoka kaacha 900bil makusanyo ya mwezi sasa hivi max ni 1.3tril tofauti ya 400bil..

Fuatilia makusanyo aliyoacha BWM aliyoacha JK na atakayoacha JPM halafu uwapime..
 
Matumizi ya hovyo hovyo ya Kikwete yanajumuisha na yale ya kununua MV Bagamoyo?

Magufuli kinachomponza ni kauli zake za kejeli na majigambo hadi kwa wahisani.

Kila siku anawaita mabeberu alafu anaenda kuwaomba hela, kila siku anajigamba nchi kua Donor alafu anaenda kuwapigia magoti.

Kuendesha nchi sio mchezo.
 
JK alitengeneza vyanzo vingi vya ndani vya kukusanya kodi kwa kustimulate uchumi mtaani kifupi alijaribu kumlisha ng'ombe majani ili amkamue..

Kwa JK sekta binafsi ilichangamka na watanzania wengi wakaanza kuwa wafanyabiashara wa kimataifa na ndani..
Uwepo wa hela ulisaidia watu kusafiri, kujifunza na kutafuta fursa sehemu mbalimbali duniani.. Hali ile ilisababisha kila sekta kuwa ya kibiashara kuanzia michezo, filamu mpaka mazao..

Utawala wa JK ndio utawala pekee watu walikimbilia kujiajiri na vijana hawakutamani sana kuajiriwa bali walijikita kutanua mawazo wajiajiri na kuzungusha hela mtaani..

Alipopaacha JK palihitaji akili nyingi kidogo kutwist na kufukia mapungufu kama usimamizi mbovu wa mali za umma, uwajibikaji na ufisadi.. Akili hiyo ingepatikana bila shaka leo hii tungekuwa mbali kiuchumi..

JPM ana dhamira na moyo wa dhati kabisa ila wanaomzunguka wako theoretical zaidi na sio practically..
 
Waziri wa fedha kasema hakuna au pesa unayozungumzia ni hiyo buku 7 mnayolipwa kila siku Lumumba
sjui kwanini kuna baadhi ya wapumbavu wanaamini mtu aspikuwa na mtazamo wake basi ni either lumumba or nyumbu respectively,,,,,,,,,,,,,!!!skia ww black dude,,,,,,mm sio lumumba kw kukusaidia tu,na wala sio nyumbu kw taarifa yako,hii kauli yangu sio research tittle ila ni observable fact,hii serikali ina hela kuliko ya kikwete,ishu ya hela kukauka mtaani ni ishu nyingne, uzi ulikuwa categorically comperative kati ya hizi regimes mbili,pumbavu zako
 
Tutasingizia ushoga nk lakini wenzetu walioendelea wana focus zaidi mahara palipo utawala bora unaojali demokrasia.Wakitoa misaada jicho lao ni demokrasia inayowahakikishia kama fedha zao zinatumika vizuri na kwa uwazi bila ya upendeleo wa kikundi cha watu wachache.Mifano ya nchi za Afrika kama Ghana,Kenya,Namibia,South Africa ,Nageria na nyingine zinazofuata demokrasia ya kweli mbona maendeleo ya nchi zao yanatia matumaini.
 
Back
Top Bottom