Maoni yangu: Secretariati yetu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kufanya kazi mbili maana muda si rafiki

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
948
2,857
MAONI YANGU KWA SECRETARIATI YETU YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM, KUFANYA KAZI MBILI KWA MAANA MUDA SI RAFIKI.

Leo 11:11hrs 05/06/2021

1. Kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-25

2. Kuimarisha Chama Cha Mapinduzi kwa kusimamia maswala yote ya Ukuaji wa Chama kwenye maeneo yote Kiuchumi, kibiashara, kijamii na ongezeko la wanachama,

3. Kuitangaza CCM,yaani Brand Management ili tusirudi zama za 2015.

Chadema na Act wameanza kupita kila Jimbo kujenga Chama na matunda yao yataonekana 2025.

Kwa ufupi awa Wapinzani hawana jema hata moja kwa CCM,kwa Serikali na kwa Tanzania,wanataka nchi isitawalike na ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 isitekelezeke.

Lengo kubwa la Wapinzani wanataka Uchaguzi wa 2025 waweze pata kura na Ufuasi mwingi wa Watanzania kuliko CCM na wameanza kuzungukia majimbo kutafuta wafuasi wakipigia simu wafuasi wa Team Mabadiliko 2015 waweze kurudi Chadema na kuyatafuta tena mabadiliko kama walivyofanya kwenye Uchaguzi wa Mwaka 2015.

Secretariati ya CCM yapaswa kujua kuwa CCM ina mkataba mmoja tu na Watanzania wote Wazalendo,wanyonge wasio na sauti na wenye sauti,Matajiri na masikini walikipigia Chama Chetu Cha CCM kura za kishindo kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 na kushinda zaidi ya asilimia 80%.

Mafanikio Makubwa na Heshima kubwa ya CCM kwa miaka hii mitano 2020-2025 ni Utekelezaji wa Kishindo wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 25 maana ndio kinachosubiriea sana na Watanzania woote Wazalendo.
 
Sio kwamba hawana jema KWA ccm,na nchi isitawalike how, ? alihali wote ni watz,

Hoja zingine KWA chama Chako ni nzuri tu, ila uliposema wanataka nchi isitawalike ndo umeteleza mkuu


Cha muhim kila chama iwe ccm,Chadema n.k kijikite kwenye ubunifu wa kuvutia wanachama, kadri kinavyoweza na mahamuzi yabaki KWA wananchi,nani anaestahili kuwaongoza KWA kupitia chama kipi basi,

Binafsi natamani kila chama kiwe na nguvu ili kuleta ushindani wa kisiasa wenye tija , Ccm hata ikiongoza miaka mia ili Hali viongozi wamepatika KWA njia ya haki KWA kupitia tume huru , sawa kabisa Wala hakuna shida, hivyo hivyo chama kingine kikichukua dola KWA taratibu hizo, hakuna shida,
 
Back
Top Bottom