Maoni yangu mechi ya Chelsea vs Manchester United

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
509
1,000
Fair result kwa Man United, alama moja mbele ya Chelsea ilikuwa na maana kubwa sana kwa Man United, ubora wa mpinzani wake na matokeo aliyoyapata hivi karibuni unapiga tu makofi kwa mlichokipata.

Nilielewa kwanini Michael Carrick aliamua kumuanzisha nje Cristiano Ronaldo, alitaka wachezaji wake wa mbele wakimbie muda wote kwa sababu aliamua timu yake ibaki chini na kushambulia kwa counter.

Michael Carrick katika 4-3-1-2, ilikuwa ni ngumu kushindana na Chelsea katika eneo la kiungo ambao walifaidika kwa kuwa na idadi kubwa ya wachezaji ( numerical advantage ) wakaigawa United na kuvunja mawasiliano baina ya viungo watatu wa kati ( Fred, Scott na Matic ) na wachezaji wa mbele.

Kosa moja tu la Thiago Silva lingemfanya Carrick awe shujaa kutokana na mpango ulioingia nao, ilikuwa ni ngumu kuona United wanapataje bao, goli la Sancho likaufungua mchezo na timu zote mbili zikaanza kupishana, ubora wa pasi, kuishinda mipira ya pili na kutumika nafasi.
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,727
2,000
Kwa hiyo matokeo ni ngapi ngapi?
Maana sisi wengine tulishaacha kufuatilia sana haya mambo ya mpira mara kwa mara.
 

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
509
1,000
Mlipuko wana mechi 8 hawajapata ushindi dhidi ya United
IMG-20211128-WA0341.jpg
 

Tanayzer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
2,865
2,000
Poor reasoning! Umetawaliwa na akili za uyanga na usimba, kwa hiyo hiyo ndo inaondoa dhana ya uwezo mdogo wa United?
Ngoja nimsaidie...wangekuwa na uwezo mdogo si mngewafunga?

au haujui mlishindwa funga kwa open play hadi refa awatengee tuta.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom