Maoni yangu kwa Wapinzani hapa Tanzania

yeddy guyy

JF-Expert Member
Mar 31, 2015
627
489
Mambo yanaenda kasi sana hebu ona haya

1. Juma Haji Duni mwaka 2016 alitumia miezi 3 kuhamia Chadema na kurudi CUF. Huku kunaitwa kutokujitambua unataka nini hasa.

2. Lowassa kajiandaa kwa miaka 20 kuingia ikulu na kakosa Magufuli kwa miezi mitatu tu kaingia Ikulu. Huku kunaitwa ni kupoteza muda

3. Mrema anataka Ukawa mpya kati ya CCM na TLP CCM wakakataa rais akamteua kuwa mwenyekiti wa Parole, huku ni kunaitwa kukanyaga ganda la Ndizi.

4. Chadema mwanzoni ilidai Magufuli anatumia sera za Ccm lakini leo sera zile zile zimewabadilikia na wanadai ni udikteta. Huku kunaitwa kusahau kulikopitiliza.

5. Sumaye toka nia ya kugombea uraisi hadi kugombea uenyekiti wa chadema mkoa wa Pwani. Hii ni sawa na mtu aliyeenda kuwinda Tembo akarudi na panya.

6. Mbatia toka kuwa mwenyekiti wa chama hadi kuwa msemaji wa Chadema. Hii ni sawa na mtoto aliyeenda kumsalimia bibi yake akakuta anapika wali akagoma kurudi akalala huko huko.

7. Maalim Seif Toka kumshtaki Shein ICC na kushindwa kufungua mashtaka hayo hadi kukataa kumpa mkono kama adhabu ...... hii ni sawa na kupigwa kelbu na kwa kuwa huna la kumfanya ukaamua kugoma kula.

8.Haina miaka Mingi toka Chadema wawatuhumu cuf kuwa wanaunga mkono ndoa za jinsia Moja (waliberal) nakumbuka walitaka kupigana bungeni hawa leo wameungana. Huku kunaitwa

9. Maalim Seifu toka kuhutubia Maelfu pale Kibanda Maiti huku akiwa na walinzi, ofisi na wapambe hadi kuonekana akitembea na miguu na fimbo mkononi ....... huku kunaitwa kuzurura.

10. Mbowe toka kutangaza operation Ukuta hadi kubomolewa kwa Ukuta wa Bilcanas na operation ikaishia hapo hapo kwa visingizio lukuki..... huku kunaitwa mama mkanye mwanao.

11. Lowasa katoka kuwa Waziri mkuu hadi kuwa raisi wa Facebook. Huku kunaitwa bora liende.

12. Lowassa kazunguka nchi nzima akiwa dhohofu wa Afya kunadi wagombea wa Cuf huku lipumba akimpinga baada ya cuf kuongeza wabunge kutokana na juhudi za lowassa lipumba karudi kuja kula Ruzuku...... huku kunaitwa Timing

13. Watu 14 wa CUF kuwapiga watu 400 kwenye mkutano nalo linapaswa kuingizwa kwenye kitabu cha maajabu ya Dunia..... huku kunaitwa wingi si hoja, hoja ni Weledi.

14.Maalim Seifu kuikimbia ofisi yake buguruni huku akifanyia shughuli zake vichochoroni. Huku kunaitwa woga uliopitiliza.

Mungu ibariki Tanzania Ccm oyeee
 
duni hakuhamia chadema km unavyomaanisha ww kimsingi angerud tu CUF hilo kila mtu anafaham kasoro ww...ht vilaza wa lumumba wanajua hilo so km hadi lumumba wamekushnda cjui tukuweke kwe kundi gan
 
1. Juma Haji Duni mwaka 2016 alitumia miezi 3 kuhamia Chadema na kurudi CUF..... Huku kunaitwa kutokujitambua unataka nini hasa.

2. Lowassa kajiandaa kwa miaka 20 kuingia ikulu na kakosa Magufuli kwa miezi mitatu tu kaingia ikulu....Huku kunaitwa ni kupoteza muda

3. Mrema anataka Ukawa mpya kati ya CCM na TLP CCM wakakataa rais akamteua kuwa mwenyekiti wa Parole.... huku ni kunaitwa kukanyaga ganda la Ndizi.

4. Chadema mwanzoni ilidai Magufuli anatumia sera za Ccm lakini leo sera zile zile zimewabadilikia na wanadai ni udikteta...... Huku kunaitwa kusahau kulikopitiliza.

5. Sumaye toka nia ya kugombea uraisi hadi kugombea uenyekiti wa chadema mkoa wa Pwani ...... hii ni sawa na mtu aliyeenda kuwinda Tembo akarudi na panya.

6. Mbatia toka kuwa mwenyekiti wa chama hadi kuwa msemaji wa Chadema..... hii ni sawa na mtoto aliyeenda kumsalimia bibi yake akakuta anapika wali akagoma kurudi akalala huko huko.

7. Maalim Seif Toka kumshtaki Shein ICC na kushindwa kufungua mashtaka hayo hadi kukataa kumpa mkono kama adhabu ...... hii ni sawa na kupigwa kelbu na kwa kuwa huna la kumfanya ukaamua kugoma kula.

8.Haina miaka Mingi toka Chadema wawatuhumu cuf kuwa wanaunga mkono ndoa za jinsia Moja (waliberal) nakumbuka walitaka kupigana bungeni hawa leo wameungana....... Huku kunaitwa

9. Maalim Seifu toka kuhutubia Maelfu pale Kibanda Maiti huku akiwa na walinzi, ofisi na wapambe hadi kuonekana akitembea na miguu na fimbo mkononi ....... huku kunaitwa kuzurura.

10. Mbowe toka kutangaza operation Ukuta hadi kubomolewa kwa Ukuta wa Bilcanas na operation ikaishia hapo hapo kwa visingizio lukuki..... huku kunaitwa mama mkanye mwanao.

11. Lowasa katoka kuwa Waziri mkuu hadi kuwa raisi wa Facebook ....... huku kunaitwa bora liende.

12. Lowassa kazunguka nchi nzima akiwa dhohofu wa Afya kunadi wagombea wa Cuf huku lipumba akimpinga baada ya cuf kuongeza wabunge kutokana na juhudi za lowassa lipumba karudi kuja kula Ruzuku...... huku kunaitwa Timing

13. Watu 14 wa CUF kuwapiga watu 400 kwenye mkutano nalo linapaswa kuingizwa kwenye kitabu cha maajabu ya Dunia..... huku kunaitwa wingi si hoja, hoja ni Weledi.

14.Maalim Seifu kuikimbia ofisi yake buguruni huku akifanyia shughuli zake vichochoroni .... huku kunaitwa woga uliopitiliza.

Mungu ibariki Tanzania
Ccm kanyaga twende
Mpaka tutaheshimia Lipumba Dume Maalim Seif kwaheri

Na: Faida potea Kijana wa mwanza mdogomdogo mpaka Dodoma 2020 Ishallah
 
"Naondoka nikiwa naacha uhusiano wa Kenya na Tanzania ukiwa mzuri kuliko wakati mwingine wowote. Nina uhakika hautabadilika. Labda tupate mtu MPUMBAVU KWELI, wa AJABU SANA, ambapo kwa Tanzania watu hao wapo wachache sana" - J.M. Kikwete; Nairobi, 2015.
 
Kweli dunia imetia nanga...ngoja niongeze tuu popcorn nione hii series itaishia wapi
 
"Naondoka nikiwa naacha uhusiano wa Kenya na Tanzania ukiwa mzuri kuliko wakati mwingine wowote. Nina uhakika hautabadilika. Labda tupate mtu MPUMBAVU KWELI, wa AJABU SANA, ambapo kwa Tanzania watu hao wapo wachache sana" - J.M. Kikwete; Nairobi, 2015.
Aisee hii aliisema kweli au?
 
Huyo kishapatikana na aliyetoa kauli hii ndiye aliyesumkumizia Ikulu pamoja na fisadi mwenzie.

Back
Top Bottom