Maoni yangu kwa album ya Harmonize (High School)

Akae atulie atafute Management nzuri.

Ukiwa na Album Nzuri kama huna atakaye iiuza ni Bureee, watu watawekeana kwenye flash Wataenda
 
Album mbovu,
Huyu jamaa huwa anajua sana kuandika na mamelody lakini sijui zinaenda wapi siku hizi.
Halafu hii tabia ya kuchukua vionjo vya nyimbo za wengine inamshusha sana!
 
Kiukweli sijaipenda.
Na sijui kwanini huyu mwamba anapenda kuimba kingereza sana.

Sio siri kwa content za kibongobongo maneno ya kingereza yanafit kwa kuchomekea chomekea tu na sio ngoma nzima au robo tatu ya ngoma yako yote iwe kimombo tupu. Na bahati mbaya zaidi mwamba inaonekana hana misamiati mingi ya lugha hiyo, kinachopelea nyimbo zake za kingereza kua na maneno yaleyale.

Sasa kama ile singeli jamani daah, na bahati yake tu ipo ndani ya album. Kama ndo ingekua katoa kama single tu ingebuma ndani na nje.
 
Album mbovu,
Huyu jamaa huwa anajua sana kuandika na mamelody lakini sijui zinaenda wapi siku hizi.
Halafu hii tabia ya kuchukua vionjo vya nyimbo za wengine inamshusha sana!
Mkuu nikikumbuka zile ngoma zake..
Matatizo
Bado
Aiyola
Show me.
Paranawe ft rayvany
Shula ft korede bello

Aisee konde yule alikua wa moto kichizi, saivi anapuyanga mnoo.
 
Harmonize msanii Bora,tatizo yeye ni mfupi saaana analeta shida kuangalia video zake maana kwa ukubwa wa TV yangu inches 62 anaoneka kituko
 
Kondeboy ni fighter af mtu wa Wana Sana , kutojifungamanisha na wadada Sana kama ilivyozoeleka Kwa wanamziki wa WCB kumempa hipe Kwa Wana wa kitaa, kwenye vijiwe vya washikaji Kondeboy anakubalika kinyama
Had wee umemkubali bas case kwisha,
 
Ngoma nazozielewa kwenye hii album
1/ Influencer
2/ Single
3/ Why
4/One question
5/ Mtaje
6/Always
7/I can't stop
8/Mood
9/Serious love ( japo sijaelewa ilivyomaliziwa kule mwisho producer alizima beat kienyeji sana )
10/What do you miss
11/Turn up
 
Mimi ni chizi muziki napenda kila aina ya muziki najua mziki mzuri na mbaya.

Tukianza na ushabiki mimi ni timu Diamond

Yani Simba namkubali kindaki ndaki ata akifanyaga upuuzi huwa naona sawa tu. Ila niwe mkweli tuu leo nimesikiliza album ya Harmonize aisee huyu jamaa ni noma katika nyimbo 17 nimependa nyimbo kama 10.

Mara nyingi wasanii wa bongo wakitoa album unaishia kupenda 3 mpaka 5. Yaani toka waanze kutoa maalubam yao ukiacha ile ya darasa basi hii itakuwa ya pili kuipenda.

Nimegundua kitu kwa Hamo, Harmonize hana sauti nzuri ya kuvutia ila ni fundi mzuri wa kucheza na melody. Ndo mana pia tunamuana anafanya vizuri kwenye amapiano na kwenye hii album amenisibitishia hilo kupitia nyimbo yake ya singeli alo imba kiingereza.

Na chakumalizia ni kwamba jamaa naona anaharibu tu kwenye video yaani anakuwa ajiongezi kabisa anashindwa hata na MARIOO.

Audio worldwide halafu video za kawaida.

nyau)
Basi sema unakuja saa ngapi ama kwenu umeshakatazwa
Said kichwa nitamueka wapi na mkongo nimeshampakaza
Iyo mitungi ndo usiseme utakunywa utasaza
Kama pesa ndo zipo nyingi kuzigawa nimeshaanza

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom