Maoni yangu kuhusu utafiti wa TWAWEZA

Jereman

Senior Member
Jun 29, 2016
140
124
Na Thadei Ole Mushi.

Nimeona utafiti wa Twaweza kwa kifupi sana ila nasikitishwa na jinsi watu na hasa waandishi wetu wanavyoimanipulate jamii. Nimesoma tweeter za magazeti mbalimbali pamoja na watu maarufu kama Milard Ayo ila zimeandikwa kishabiki sana. Ukweli wa mambo kwa kila variable huu hapa....

Kila chama kinaweza kutumia maoni yangu haya ni mtizamo huru.

1. KIPENGELE CHA ELIMU

Kwenye kipengele cha elimu kipo kama ifuatavy:-

i) Wenye Elimu ya juu CCM imeongoza eneo hili kwa kupata asilimia 46% huku chadema ikipata kura 21%

[HASHTAG]#Tafsiri[/HASHTAG].
Hili ndio eneo la kupata viongozi na watendaji mbalimbali wa serikali. Kwa maana hiyo kwenye swala la vyama hivi viwili kupata wagombea wenye sifa na weledi CCM ina wigo mkubwa zaidi kuliko Chadema.

Ni kundi la kwanza muhimu ambalo kila chama lilipaswa kulishawishi kwa kuwa linaaminika kwenye jamii. Kwa maana hiyo katika eneo hili Chadema inahitaji kulifanyia kazi sana kundi hili ili kupata watu sahihi wa kuweza kuichallenge serikali.

ii) Waliomaliza primary CCM imeongeza tena eneo hili kwa kuwa na asilimia 66 huku Chadema ikiwa na asilimia 17.

[HASHTAG]#Tafsiri[/HASHTAG].

Hili ndio kundi kubwa zaidi kielimu Tanzania. Kundi hili pamoja na kutokutabirika kwenye uchaguzi ila si eneo la kubeza.

Kwangu mm hili ndio kundi linaloweza kushawishika kwa urahisi. Ni kundi la kulinda kila saa maana leo wanaweza kuwa huku kesho wanaweza kuwa upande mwingene.

Kama CDM haitawekeza katika kubaini kundi hili na kutafuta matatizo yao watapata shida sana kwenye uchaguzi mkuu. Ni kundi rahisi sana kulibadilisha kimtizamo na fikra...

iii) Ambao hawakusoma kabisa CCM Imepata asilimia 72 huku Chadema ikiambulia asilimia 14.

[HASHTAG]#Tafsiri[/HASHTAG]

Kundi hili halina tofauti na kundi lililopita. Ni kundi ambalo hupatikana zaidi vijijini. Mara nyingi kundi hili hutokea kwenye jamii za kifugaji na wavuvi au jamii nyingine zenye sifa ya kuhama hama.

Kama ilivyo kwa kundi lililopita ni rahisi kubadili mtizamo wao kama upande wa pili watalibaini kundi hili na kutafuta matatizo yao na kuyaseme.

2. HALI ZA KIUCHUMI.

Kwenye kipengele hiki CCM imeshinda vipengele vyote yaani kuanzia maskini kabisa, maskini, wenye kipato cha chini, matajiri na matajiri sana. Uwiano wa asilimia kwa kila kipengele ni kuanzia 60+ kwa CCM huku Chadema ikiambulia wastani wa asilimia 15+ kwa kila kipemgele.

Nitafafanua hapa vipengele Vitatu tu.

i) Kipengele cha watu maskini sana CCM imeshinda kwa kupata asilimia 69% dhidi ya asilimia 16 za chadema.

[HASHTAG]#Tafsiri[/HASHTAG].

Bado chadema haijawekeza kwenye kundi hili. Toka uchaguzi mkuu upite hawaongeii Lugha ya kimaskini. Badala ya kuwatetea maskini mara nyingi wamekuwa wakiwatetea maswahiba wa Lowassa ambao ni kundi la matajiri.

ii) Kundi la watu wenye kipato cha wastani CCM imeshinda kwa asilimia 68 huku chadema ikiambulia asilimia 17.

[HASHTAG]#Tafsiri[/HASHTAG].

Hili ni kundi muhumu mno ni kundi wanalotokea tabaka la wafanyakazi na wafanyabiashara wa kati.

Ni kiungo kikuu cha jamii kwenye swala la kiuchumi. Wanapatikana kila mahali kutokana na kuwa wengi ni wafanyakazi.

Kwa chama chochote kikiweza kuwapata hawa watakuwa wamechanga karata zao vizuri kwani watakuwa wamepata wawakilishi wao kila mahali nchini.

Ccm hapa inaonekana kufanya vizuri zaidi ya Chadema. Lazma chama kijitathimini kwa nn wanashindwa kuwasemea wafanyakazi ambao kila siku mbaya wao ni serikali kila mahali duniani...... ni eneo muhimu mno la kufanyia kazi.

iii) kwenye kundi la matajiri CCM imeshinda kwa asilimia 53 huku chadema wakiwa na asilimia 21.

[HASHTAG]#Tafsiri[/HASHTAG].

Sera za mheshimiwa raisi JPM mara nyingi zinekuwa zikiibua sintofahamu kwa matajiri. Ccm pamoja na kuongoza kundi hili ila imeongoza kwa asilimia kidogo sana. Ukichukua asilimia 53 za ccm unabakiza asilimia 47 zikiwa hazikuungi mkono.

Ni kundi ambalo njia zao za kujipati fedha zimefungwa au kupunguzwa. Ni jambo la kuamua tu.... kupitia Lowassa chadema inaweza kuja kufanya vizuri zaidi kwenye eneo hili.

3. KIUMRI.

Kwenye kipengele cha Umri CCM imeonekana kushinda pia vipengele vyote.

i) Kundi la miaka 50+ ndio kundi ambalo CCM imefanya vizuri zaidi. Hapa ccm imepata asilimia 80 dhidi ya asilimia 8 tu za chadema.

[HASHTAG]#Tafsiri[/HASHTAG].

Si kundi muhimu sana kwenye maswala ya kisiasa kwa sasa kwa kuwa kwa mujibu wa sensa ya 2012 hawafikii hata nusu ya kundi la vijana.

Ni kundi ambalo faida yake unaipata tu kwa kuwa ni watu ambao hawaoni hatari kupoteza muda wa masaa mawili kusimama kwenda kupiga kura tofauti na vijana. Hawa pia hujiandikisha karibia wote kupiga kura.

Wengi wao wamezaliwa TANU ikiwa madarakani. Kwao vyama vingi si muhimu sana bado wanaishi maisha ya Nyerere.

Chadema haijawafikia watu hawa ... hawana smartphone hawa ..... lazma uende field ukakae nao kuwashawishi.

Na ukiangalia pia kundi linalofuata la miaka 40-49 ccm imepata asilimia nyingi pia 68 kwa 16 bado sifa zao hazitofautiani sana na za hapo juu.

ii) Kundi la miaka 18-29 ndio kundi ambalo ndilo kundi ambalo CCM wanapaswa kulifanyia kazi.

Ccm imepata asilimia 55 kwa hiyo kuna asilimia 45 ambazo zipo njee. Ni kundi ambalo wengi wamezaliwa kipindi cha mfumo wa vyama vingi.

Ni kundi la vijana ambao wapo vyuoni na wengine wapo mtaani wanatafuta kazi. Migogoro ya mikopo na kukosekana kwa ajira panailetea ccm shida hapa.

Ni kundi ambalo linashuhudia kila kosa la serikali kutokana na kuathirika na kukua kwa tecnolojia ya habari na mawasiliano. Hawa karibia wote wana smart phones wapo kwenye magroup mbalimbali.

Ndio wasambazaji wakuu wa habari ziwe ni za uongo au za ukweli.... chadema inaonekana imewekeza kwenye kundi hili.

Hasara yao sio wapiga kura wengi ni wazee wa amsha amsha ila kujiandikisha ni vigumu. Ni kundi ambalo linahama hama leo hapa kesho kule kutokana na kutafuta maisha. Wengi wapo mijini.

Faida yao hawabadiliki kwa uraisi kutokana na umri wao .... vurugu za maono (Ubishi).

4. KIPENGELE CHA MAKAZI.

Hapa kuna vipengele viwili tu mjini na vijijini vyote CCM imeshinda. Ila vijijini imeshinda vizuri zaidi imepata asilimia 68 kwa 14 za chadema. Eneo ccm walilofanya vibaya ni mjini wana asilimia 57 kuna asilimia nyingine 43 zipo njee ni nyingi sana.

[HASHTAG]#Tafsiri[/HASHTAG].

Mjini ndio eneo wanalokutana wasomi wengi, vijana wengi, matajiri wakubwa wengi.

Makundi haya yote si rafiki kwa CCM sana kama ambavyo nimeshaelezea hapo juu. Techolojia ya mawasiliano pia ipo hapa inaathiri asilimia hizi za CCM. Matatizo ya wamachinga nayo yanaleta matatizo kwa ccm hapa.

5. KIPENGELE CHA JINSIA.

Kwenye kipengele hiki ccm imeshinda vipengele vyote. Ccm imefanya vizuri zaidi kwenye kundi la wanawake kuliko chadema.

Ccm imepata asilimia 68 dhidi ya 14 kwenye kundi la wanawake.

Faida ya kundi hili ni wapiga kura na wapo wengi zaidi. Kwa Chadema kuna mfumo dume hakuna wanawake wengi ambao ni viongozi wanaoweza kuwasemea wanawake hawa......

MWISHO.

Waandishi wetu wanapotaka kuandika habari za kiutafiti waziripoti kama zilivyo kama hawana weledi wa kutafsiri data hizo.

Au watafute wataalamu wawahoji ili kupata mitizamo yao kuliko kuandika uongo.

Ole Mushi
 
Hizi ni campaign huku wengine wakipigwa mkwara wa kutokufanya siasa. TWAWEZA daima wanacheza ngoma ya Magogoni, kama CCM wanafanya vizuri kiasi hicho hofu ya kuzuia wapinzani wake inatoka wapi?!

Mleta hoja (mchambuzi) CCM bila police ni wepesi na hawana nguvu kiivyo
 
CCM bila police na tume yao ya uchaguzi pamoja na katiba yao mbovu watanyweka kama chai ya maziwa
 
kwa miaka miwili sasa taasisi ya kitafiti TWAWEZA naishuhudia ikitoa tafiti za masuala ya kisiasa zaidi kuliko masuala mengine
labda ndo lengo lake kubwa
 
kwa miaka miwili sasa taasisi ya kitafiti TWAWEZA naishuhudia ikitoa tafiti za masuala ya kisiasa zaidi kuliko masuala mengine
labda ndo lengo lake kubwa
Twaweza huwa wanatoa ripoti nyingi sana zinazohusu elimu,afya na huduma mbalimbali za kijamii ,Siasa huwa inapewa attention sana
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom