Maoni yangu kuhusu suala la BASATA na Wasanii wa Tanzania

monde arabe

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
8,444
12,981
Habar ndugu wanabodi,

Najua kila mtu kwa hivi sasa anafahamu kinachoendelea kati ya Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) na wasanii na kabla sijaeleza mengi sana naomba nianze kwa kuufichua ujinga walionao wasanii hawa wa Kitanzania;

Hawa wasanii wetu ni watu wa hovyo kuwahi kutokea katika uso wa Dunia (hapa nazungumzia zaidi wasanii wa bongo flavour, bongo movie na hata wale wanaofanya muziki wa dansi). Hawa wasanii walio wengi ni wadangaji wanaoendesha shughuli hizo kwa mgongo wa sanaa (watu wao wa karibu wanadai kuwa wengine ni mashoga, wengine wanauza papuchi na hata wapo wengine wanaouza Channel 'O' ili waweze kuishi mjini)

Hawa wasanii wamekuwa wakiishi maisha ya kuigiza sana mara wanaendesha mandinga ya bei mbaya, mara wanafanya birthday parties za gharama kubwa, mara wameruka kwenda mambele kama vile States, Hong Kong, Brazil na kwingineko, mara wanatupia picha kwenye mitandao wapo kwenye majumba ya kifahari na show off nyingi zisizo na maana.

Lakini wanapoumwa ama kupatwa na matatizo yao binafsi huirudia jamii na kuiomba msaada na huwa wanaenda mbali na kuyachukulia matatzo yao binafsi kuwa ni matatzo ya jamii nzima (rejea kwa Wastara and the like)

TATIZO KUBWA KWA HAWA WASANII

Mnamo mwaka 2015 walikuwa vifua mbele kuipigia CCM kampeni (hili siyo tatzo kwa kuwa ilikuwa ni issue ya kibiashara na ktk biashara kila mtu au kampuni hutazama zaidi faida) lakini nje ya biashara walikuwa wanajua kabisa mambo mabaya ambayo Watanzania tulitendewa na bado tunatendewa na CCM kama chama tawala. Wananchi wengi wamefilisiwa, wamewekwa vizuizini, wameuawa, wamesababishiwa umasikini na CCM na yote hayo wasanii hawa walikuwa wakiyaona lakini katika kampeni wakasimama upande wa chama.

Baadhi hata ya wasanii wakaanza kualikwa kwenye jumba la magogoni kwaajili ya kwenda kula na kunywa. Hakuna hata mmoja aliyeweza kusimama kwenye upande wa haki kwa kuwa walijua kuwa hicho ni kilio cha watanzania na siyo kilio chao.

Najiuliza wako wapi wasanii au wanamuziki kama akina Bob Marley, Anikulapo Felakuti na wengineo wengi walioweza kukemea maovu kwa njia ya sanaa wakiwemo wasanii wa Hollywood na Bollywood ambao mpaka hivi leo bado wanazi-chalenge nchi zao na watawala wao japo ni watawala wenye nguvu.

TATIZO LA WASANII NA BASATA

Hii nchi ina watu wajanja sana tangu kitambo. Serikali ya CCM imeamua kuwakamua mpaka damu hawa wasanii uchwara kwa sababu zifuatazo;

1. Serikali haitaki pawepo na wasanii wengi kwenye game so imeamua kuweka vigezo ambavyo baadhi ya watu watashindwa kuvitekeleza na hivyo hawatatambulika kama wasanii na ukitokea wakajihusisha na sanaa wakati hawana vigezo basi watachukuliwa kama wavunjifu wa sheria na wale watakaobaki kwenye game kama Mpoto na wenzake basi Serikali itakuwa inawatumia kwenye kazi zake za kiserikali

2. Serikali imeamua kufanya hivyo ili iweze kupata fedha walizopewa mwaka 2015 na pia imeamua kuwakamua ili kupata fedha watakazolipwa mwaka 2020 so fedha watakazolipwa mwaka 2020 zitakuwa ni zile walizochunwa kupitia BASATA kama kodi, fedha za utambulisho kama wasanii (viingilio vya kujiunga na BASATA).

Kumbuka hata Mkuu wa Kaya alisema wale wafungwa waliopo magereza wafanye kazi ili kupata chakula chao wenyewe wasiitegemee Serikali. Kwa muktadha huo CCM imewachukulia kama wafungwa ambao mtajilisha wenyewe

FAIDA YA WAZO LA BASATA

1. Kwanza watapunguza mbwembwe kwenye mitandao kwa kuwa wengi hamtakuwa na fedha za kufanyia show off

2. Tutapata nafasi ya kusikiliza muziki mzuri na mtamu kutoka mataifa mengine kama vile Kongo, Uganda, Kenya na kwingineko kwa kuwa hata hiyo miziki yenu yenyewe haina quality (wasanii wanafana kuanzia sauti, beats mpaka namna ya uandishi na pia kuna kelele nyingi sana kwenye nyimbo zenu zisizo na ulazima)

3. Mtapata nafasi ya kuijua vizuri CCM kama wasanii pamoja na kuweza kufanya kazi nyingine kama vile kulima, kwenda shule

Asanteni
 
Mkuu wa kaya, ananifurahishaga mda mwingne.

Hawa watu wanamaisha ya kujionesha sana na wanapopatwa na tatizo wanataka liwe la Watanzania

Hivi kwanini kila inapotokea msiba Steve ndo anakuwa mbele sana kwenye msba, anaiba au?
 
ewe mtoa maada kwan CCM na BASATA wanauhusiano gan?
Mkuu,uliacha shule ukiwa darasa la kwanza muhula wa kwanza au muhula wa pili?
Chukua hiyo lecture ya bure;BASATA (baraza la sanaa la Taifa/Tanzania)
baraza hili lipo chini ya Wizara inayohusika na mambo ya sanaa na michezo na viongozi wakuu wa taasisi hii huwa ni waziri na naibu waziri wa wizara ya inayohusika na masuala ya sanaa na michezo
Hawa mawaziri huwa ni wabunge wa chama tawala so,wanapopewa au kuteuliwa kuwa mawaziri kazi yao ni kusimamia yale yanayopangwa na serikali na serikali huundwa na chama tawala na ndyo maana hawa mawaziri na wabunge wanatokana na vyama

Taarifa;ubunge na uwazir huwa ni Mali ya chama!
 
Nasikiliza miziki laini na mitamu ya kwa Trump, Miziki kama R&B, BLUES, POP, COUNTRY, Unapata vitu vitamu vya Celine Dion,Laura,Westlife,E.John,J.Collins,Backstreet,Boyzone,Nsync, N.K
UNAPATA KITU LAINI ROHO INAPENDA.
 
Kuna ukweli kiasi ila umeonesha Hasira Kali sana, kwa kifupi wasanii hawa wanafahamu njaa zao.. wamekwama kujinasua hawana tofauti na wasomi; wao pia wamefeli kuinua uchumi na ustawi wa jamii..kila mtu amebaki anapigania mkate wake bila kuzingatia jamii kwa ujumla..wazawa watakuwa Wapagazi na wageni (Investors) watavuta Upepo
 
Tangu nimeanza kuzika wasanii... Ni mmoja tuu msiba ulikua kwake anapoishi. (Kanumba)
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom