Maoni yangu kuhusu Shirika la Bima ya Afya Tanzania (NHIF) na uendeshaji wake

ndege joni

JF-Expert Member
May 23, 2017
673
1,083
Habari za wakati huu wasomaji wote watakaopitia hii thread

Nimekuwa mwanachama mchangiaji wa Shirika la Bima la Afya (NHIF) kwa muda wa miaka 8 mpaka sasa japo pia nimekuwa napata huduma kwa zaidi ya miaka 20 kama mtegemezi. Kabla ya awamu hii wanachama tulipata huduma mbovu na kwa kweli sikuwa na hamu nayo nilikuwa naenda maabara na kupima na kununua dawa.

Tangu ameingia Rais Magufuli, (simpendelei ila ndo ukweli wenyewe) huduma zimekuwa bora sana kwa wanachama nadhani kuliko wakati wowote tangu shirika lianzishwe (sina uhakika kama kuna anayepinga aje). Kwa hili hongera sana NHIF na serikali kwa ujumla.

Hoja yangu ni jinsi huduma inavyotolewa hasa kwa hospitali za binafsi. Kwa kawaida tukipata huduma ujumbe unaingia kwenye simu kuwa kadi imetumika hospital fulani n.k... ... lakini ujumbe hausemi ni huduma gani imetolewa na dawa gani zimetolewa (hata kama mambo ya malipo ni siri) sio vibaya mwanachama kuhakikisha kuwa ni kweli huduma hiyo imetolewa? Ili kuhakikisha malipo yanayotolewa na Serikali ni sahihi. Hii itasaidia kuondoa malipo hewa kwa huduma.

Japo sijui utaratibu wa malipo ukoje lakini itasaidia kupunguza malipo ambayo mwanachama hayatambui. Hospitali Wanaweza wakaingiza malipo ambayo mwanachama hajahudumiwa ikawa ni hasara kwa serikali.

Labda kama kuna anayejua zaidi anaweza kunisaidia kuhusu hilo
 
Hakuna watu wanaofaidi pesa za serikali kama Hawa watumishi wa hospitali binafsi na pharmacy kubwa wanaotumia mfumo wa NHIF.

Na wanapenda sana ukienda wakupime, then Typhoid na UTI ni lazima uwe nayo hata kama umezaliwa leo na lazima wakupe dossage, ila pamoja na yote bado pia serikali inawafaidi watumishi mara 3 zaidi, ukipiga mahesabu mtumishi mmoja anakatwaje kwa mwaka mzima times idadi ya watumishi wote wa umma na wagonjwa wanaugua mara ngapi utagundua wanafaidi sana
 
Back
Top Bottom