Ukweli ni kwamba kuna watu lazima tutoke ndio tupate angalau kidogo cha kulisha familia. Ikatokea serikali imechukua hatua kama za Rwanda, Kenya na nchi nyingine zilizoamua kuchukua hatua ya Lockdown basi ni kiama kwa baadhi yetu.
Majuzi nilikuwa naongea na Dereva daladala mmoja anasema sasa hivi wanapeleka hesabu elfu arobaini halafu wanaishia kugawana elfu tano tano au kumi kumi yeye na konda wake. Hii ni kwasababu tu baadhi ya watu wameamua kuchukua tahadhari wenyewe ya kukaa ndani.
Wenye magari nao wanaona bora kupaki tu.
Ni ukweli usiopingika tunahitaji tahadhari ya hali ya juu sana kwasababu mwisho wa siku tutaishia kufa kama kuku wa kideri
Ila mimi naungana na Mwenzangu Donald Trump lockdown itakuwa na madhara makubwa kuliko ugonjwa wenyewe.
Kama account yako imeshiba na una uwezo wa kulisha familia mpaka huu ugonjwa utakopisha naomba usitukejeli sisi maskini wewe Jipe karantini acha wengine tupambane na hali zetu