#COVID19 Maoni yangu kuhusu chanjo ya Korona

Mkemia kay

Senior Member
Jan 25, 2020
125
122
Je, umeshawai kujiuliza ni nani aliwaambia watanzania kwamba chanjo ya korona ina madhara, kama vile kuganda kwa damu yani blood clotting?

- Ukiachana na Hayati JPM aliyekuwa akiimba huu wimbo, na pia umewai kujiuliza nani alimwambia chanjo ina madhara?

●Mambo manne niliyoyaona
1. Sisi watanzania hatukuwai kutengeneza iyo chanjo ya korona

2. Sisi watanzania hatukuwai kuitumia iyo chanjo ya korona ili kubaini ayo madhara ya iyo chanjo.

3. Ni wazungu hao walitengeneza iyo chanjo ya korona wakaitumia na hao hao wakaona baadhi ya madhara ya iyo chanjo wakaitangazia dunia kuhusu madhara ya iyo chanjo ambayo wametengeneza wao na sisi watanzania tukasikia kwamba ukitumia iyo chanjo damu inaganda.

4. Sisi watanzania hatukuwai kutengeneza wala kuandika vitabu vyovyote vya sayansi vinavyoelezea namna gani dawa au chanjo inatengenezwa na ni muda gani inachukua kukamilika kwa chanjo au dawa yoyote, ni wao wazungu wametufundisha huo utaalamu. Mimi na shaada yangu ya kwanza ya Ukemia sikuwai kuona kabisa hiki kitu ingawa ni sehemu ya taaluma yangu. Profesa wangu aliyenifundisha computational quantum Chemistry Prof. Surendra Babu alikuwa Mhindi alisema dawa au chanjo inaweza kuwa assembled kwa kumpyuta ndani ya Munda mfupi kwa kutumia computational chemistry ila shida ni pale kwenye analytical chemistry itatumia muda mwingi mpaka kukamilika kwa iyo dawa ua chanjo. Maneno kama ayo ayo niliyapata kwa profesa aliyenifundisha Medicinal Chemistry Prof. Barjarang alikuwa Mhindi pia.

●Mwisho
-Kuna uhalisia Mkubwa wa watanzania wengi kukataa chanjo ya korona kwa sababu walioitengeneza ndo walioitumia na wakatutangazia kwamba imeleta madhara kwa baadhi ya watu.

- Haikuitaji kuwa na PhD kulinganisha baadhi ya mambo

#changamoto yangu ni "Kuitumia akili yote katika kusoma" lakini sio kwamba sina akili
 
Kwa muujibu wa takwimu zilizotolewa na mtaalam leo, kati ya watu millioni moja ni wanne tu ndio wameripotiwa kupata matatizo kama hayo ya damu kuganda. Yani asilimia 0.0004%

Chanjo sio lazima, ni hiyari. Anaetaka achome, asietaka atulie. Tiache maneno maneno!
 
Back
Top Bottom