Maoni yangu juu ya tukio la Askari Polisi dhidi ya Mwanajeshi katika benki fulani jijini Dar es Salaam

Kijana kijana

JF-Expert Member
Mar 11, 2018
2,546
2,616
Habari za muda wakuu. Natumai wazima, naporomoka katika mada moja kwa moja...

Kuna tukio limetokea la askari wetu wa Tanzania(JWTZ na Polisi)ambalo limetikisha jiji kwa ujumla huku pakiwa na mishangao ya hapa na pale.

Labda nitoe elimu hii kwa ndugu zangu wote ambao bado hawajafahamu sheria na taratibu za mambo haya ya kijeshi fuatilieni.

Kwanza kabisa hakuna atakae kutambua kama wewe ni askari ikiwa tu huna uniform labda ujitambulishe kwa kitambulisho chako.

Pili, kila mtu anapofanya kazi katika ofisi yake basi huongozwa na taratibu za sheria za ofisi yake hiyo. Mfano ukienda benki unatakiwa ufuate taratibu za pale na kufuata huko ni kule kuambiwa hapo usipite hiki usifanye na utaacha kufanya kwa sababu upo katika himaya ya mtu mwingine.

Tatu, tutambue kwamba kuna kitu kinaitwa customer care. Hili suala lipo katika ofisi zote ambazo zina-deal na kusikiliza shida za watu mfano benki, vituo vya polisi (narudia vituo vya polisi yaani vituoni, au C,R.O) na sehemu zinginezo ambazo husikiliza shida za watu.

Sasa tukija katika tukio hili la juzi ni kwamba inaonekana huyo Mwanajeshi hakuwa na sare yeyote na alikuwa katika process za kutoa pesa sasa wale F.F.U walipofika waka mcommand aache anachotaka kufanya ili wao wamalize shughuli yao hiyo waondoke.

Kwanza tambua msomaji kwamba askari polisi anakuwa na sheria zinamuongoza hasa katika ishu nzito kama hiyo ya ku escort pesa sehemu mbalimbali kwa sababu ikitokea pesa zimeporwa basi huenda naye akahusishwa kwa sababu kawekwa ulinzi ili naye azitunze na ndiyo mana analipwa kwa kusindikiza huko. Kwahivyo ni sehemu ambayo Askari Polisi anakuwa makini mnooo.

Sasa walipofika benki yule mwanajeshi kupewa kauli ya kukomandiwa na kuamrishwa inaonyesha akamaindi; na hili simlaumu sana kwa sababu mafahari wawili hawakai zizi moja. Halafu kitu cha kujiuliza sasa, huyu jamaa Askari hajui kama kijeshi kuna maeneo maalum ambayo humo ni kutumia command tu na sio vinginevyo? Askari gani huyu hajui kwamba kuna maneneo ambayo lazima itumike command kutokana na uhatari wake? Kama alijua vipi naye akataka aambiwe kistaarabu? Kama hakujua hatuoni kama huyu kafanya kitendo cha kiraia na kipuuzi kabisa?

Halafu jambo lingine ukiwa kozi mtu unafundishwa na waalimu ambao wana mitusi na mikero na maneno ya ajabu wanakutamkia kuruta ili tu uzowee uone kawaida na hivyo ukifika mtaani ukakuta mtu anakupa maneno machafu wewe tayari unakuwa mkakamavu wa moyo na unaona ni kawaida tu na unapotezea. Huu ndio uaskari ni ukakamavu wa mwili na moyo. Sasa huyu mwanajeshi gani ambae command ya askar mwenzie ilimtia povu na kuanza kugoma? Kapita wapi mwanajeshi huyu kama sio unanga tu?

Halafu watu wanasema aambiwe kistaarabu au wangefanya customer care hawajui kama customer care zina sehemu zake? Hivi mtu unapokatisha kwenye kambi ya jeshi halafu wakakuona wenyewe unadhani utaambiwa kistaarabu tu au utakula tifu? Sasa ikiwa kukatisha kwenye kambi watu wanakula tifu vipi mtu kapewa dhamana ya kusindikiza pesa benki na ana silaha halafu unajitia ubabe akuache tu?

Pia yule askari aliyekuwa pembeni simlaumu kupiga risasi kwa sababu alipoona mwenzie mtutu umeshikwa huenda alijua jamaa anataka kupora silaha au kufanya kitu mbaya sasa vipi asifanye hivyo?

Lakini kimakosa kamshuti mwenzie. Na lau askari wawili wakiwa lindo na mmoja akanyang'anywa silaha kisha huyu mwingine akawepo ikawa hajapiga hata risasi basi anashtakiwa kabisa na huenda akatuhumiwa ni katika hao waliofanya dili ya kupora. Lakini alitakiwa huyu bwana asimsogelee(zero distance) yule jeshi kiasi cha kushika mtutu ilibidi akae mbali kidogo.

Kitaratibu askari polisi walikuwa katika eneo lao lakazi ambalo ni hatari hivyo lazima lugha ibadilike kabisa ili kukuonyesha wewe unaeambiwa ujue ni eneo hatari kwa sababu hata majambazi wakivamia wanaweza kukupiga na wewe risasi wasichague hvyo kutoka kwako mapema ndiyo usalama wako.

Nimalize kwa kusema enyi mnaoshabikia na kuona mjeda ni kidume basi nadhani hamjajua na kufikiria mara mbili juu ya usahihi wa nidhamu za kiaskari na kwa mtindo huu bwana tutaumia raia wengi sana kwa sababu ni watu tusiotambua maeneo ya watu na kazi zao.
 
umesoma kiushabiki sana
ungetusaidia tufahamu taratibu za kiusalama kama umenikuta ndani ya chumba cha Atm nachukua pesa kisha unatoa amri bila maelekezo ya kistaarabu kwa kuwa ww ni polisi nami ni jwtz au ni raia tu nitakuelewaje?tujaribu kuwa na kauli nzuri kwa raia hata ikibidi kutoa maelekezo kistaarbu na kuacha tabia za kibabe zisizokuwa na tija
 
Hakuna unachojua.. Command language sio kufoka.. Ni command.. Content yake.. Ukiona kuna mtu unaenda kumlinda yeye au unalinda pesa?!

Acheni kushabikia ujinga.. Unatoa maelekezo.. Na ikibidi unaestablish perimeter .. Unafanya zoezi lako.. Ukifika ukamkuta MTU amekwishafika na anafanya zoezi unangoja.. Unatoa taarifa kwa watumiaji wengine.. Wanakaa kando.

Ongea na wenye akili wakufundishe sio una shabikia ujinga humu.
 
Hoja zako siyo makini sana hao ffu awakuwa na akili ya kiaskari unamsogelea MTU huku umemwonyeshea mtutu hadi anajiami kwa kuukamata ilo ni tatizo Mara nyingi askari utoa kauli chafu na zakuudhi kwa watu wakidhani ni RAIA wa kawaida hiyo imesababishia askari wengi kujikuta matatizoni pale wanapokumbana na wakubwa zaidi yao
 
Wewe mbona unaandika vitu usivyokuwa na elimu navyo! Unataka kuwajaza ushamba na ulimbukeni watu hapa. Unaandika habari ndefu bila kuwa na cha maana chochote.

Huyo askari kwanini akatishe mtu anayetoa fedha? Kwani kutoa fedha kunachukua muda gani? Eti komandi. Wewe unafikiria kila sehemu ni kutoa komandi tu. Umezoea kuamuriwa kama mbwa unafikiri kila tukio linahitaji amri? Alitakiwa amwache amalizie kutoa fedha halafu kama kulikuwa na wateja wengine wanasubiri basi angewaambia kwa maelezo ya kiungwana kuwa wasubiri. Na sio komandi!
 
Back
Top Bottom