Dodoma: Dereva wa Tundu Lissu, Dr. Mashinji, Watakiwa kuripoti Polisi, Magari 8 Nissan Patrol yakamatwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Polisi Dodoma limekamata magari 8 na aina ya Nissan Patrol kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa risasi Tundu Lissu, RPC Muroto asema

Pia jeshi hilo linaendelea kutoa wito kwa wananchi walio taarifa kuwapa ushirikiano ili kuwarahisishia kazi

Amesema tokea tukio la kushambuliwa kwa mbunge huyo dereva wake ajulikanaye kwa jina la Adam bado hajaonekana ila ameona mahojiano yake kwenye gazeti la Mtanzania na kutoa wito kuwa afike ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Dodoma au ofisi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai Dar kwa kuwa wanaamini ana taarifa za siri na kutofika kwake kutawapa mashaka kwamba kuna jambo anaficha

Na sheria kifungu cha 9 na 10 kidogo sehemu ya 2 inasema mtu mwenye taarifa kuhusiana na uhalifu na akakataa kuwapa polisi taarifa hizo atakuwa anatenda kosa la jinai

Pia amesema jeshi la polisi ndilo lenye mamlaka pekee ya kufanya uchunguzi kwenye makosa yote ya jinai na limemekwa na mamlaka na kumtaka Katibu mkuu wa Chadema Vincent Mashinji aliyekuwa akisema anawafahamu waliofanya shambulio hilo kufika ofisi ya mkuu wa upelelezi Dodoma au mkurugenzi wa makosa ya jinai Dar kuwapa maelezo

Pia amesema jeshi lisiingiliwe na tukio hilo lisipelekwe kisiasa na kuchochea wananchi kuichukia serikali yao, matukio mengi yametokea na polisi wamefanikisha kupata wahalifu akitolea mfano matukio ya Kibiti na Mbande na Kongowe ambapo polisi walipoteza maisha

Watuhumiwa wengine 30 wamekamatwa kwa matukio mbalimbali ikiwemo kukutwa na bangi na pombe aina ya gongo
53b73c84c9e70560db3543495cc8eb08.jpg

Chanzo: Mwananchi

MY TAKE
Polisi waanze na Walinzi/Polisi wa mageti yanayoingia kwa Lissu. Huwezi pita kwenye geti linaloenda kwenye makazi ya Viongozi bila Kibali. Na nyumba ya Lissu ipo jirani na nyumba ya Spika. Je wale maaskari hawajasikia Milio ya Risasi 32?

Kwanini waliwafungulia wahalifu hata baada ya tukio?

Tuanze na Askari wa zamu nyumba za Viongozi wa pale getini.

Camera inaonesha gari lililopita ni plate namba gani? Tupeni namba tuanze kuisaka, kusema gari nyeupe tu haitoshi, magari meupe mengi.

UPDATES:

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Mashinji ajipeleka Polisi. Zaidi soma=>Ulimi wamkaanga Mashinji wa CHADEMA ajisalimisha kwa Polisi kama alivyotakiwa kufanya
 
Polisi Mkoa wa Dodoma limetaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kifika kwa RPC au Ofisi ya DCI-Dar kwa Mahojiano.
942d461c7e3103c86561f01cdec8ea31.jpg
Ahojiwe vizuri kabisa, kwa nini yeye hakupatwa hata na risasi moja?? Na kwa nini alimzuia Mh. Lissu asitoke kwenye gari?? Na kwa nini alivyoona anafuatiliwa na kuthibitisha hakugeuza hata kwenda sehemu salama kama bungeni??? Na kwa nini alienda kuitegesha gari sehemu nyeupe ili iwe rahisi kuchukua picha na kuzieneza kwenye mitandao???
 
Maswali ya kipolis hayo?
Au ya kwako?
"KWANINI YEYE HAKUPATWA HATA NA RISASI MOJA?"

May Allah bless Me and You
 
Eti kwanini hakumruhusu lissu ashuke ili achakazwe risasi? ilo ndio swali kuu bashite na dikteta uchwara wamewatuma awo misukule wao waulize.maana wameshindwa kutekeleza adhma yao kwa sababu dereva alizuia lisu asishuke
 
Ahojiwe vizuri kabisa, kwa nini yeye hakupatwa hata na risasi moja?? Na kwa nini alimzuia Mh. Lissu asitoke kwenye gari?? Na kwa nini alivyoona anafuatiliwa na kuthibitisha hakugeuza hata kwenda sehemu salama kama bungeni??? Na kwa nini alienda kuitegesha gari sehemu nyeupe ili iwe rahisi kuchukua picha na kuzieneza kwenye mitandao???
Wewe ulitaka akapaki gari msituni?
 
Back
Top Bottom