Maoni yangu dhidi ya "Baadhi ya wananchi wahuni" wa Arusha kujaribu kuzuia wanahabari wa TBC

Avatar yako inanipa picha wewe ni wa kundi gani...MHUNI tu.

Duh, kumbe hivi ndiyo viashiria vyako vya kuwaita watu wahuni? Basi nimepata jibu! Kwahiyo Yule mzee wenu Muuaji ni mhuni kwa kuwa ilakuwa anavaa cheni shingoni na kiunoni??
 
Mwandishi wa habari anafanya kazi popote bila kujaribu vitisho ndo maana hii leo unapata habari kutoka sehemu za vita na ngumu kwa mtu wa kawaida kufikia. Tatizo wengi wenu mnahisi siasa ni uadui na kupotosha wengine. Mbona uongozi wa CDM hawakutoa malalamiko kuwa TBC wanaripoti habari isivyotakiwa?

mbowe alitoa lawama kwenye uzinduzi wa m4c. Unabisha bila data
 
Mwandishi angeweza kupata uhalali kwa kujitofautisha na anaowaita "baadhi ya wahuni".
Kadri anavyojibizana na watu humu, anaonesha tofauti ya kiwango cha uhuni.
Kwanza nikiri si halali kwa mtu/watu kuzuiawengine kufanya kazi, hii si halali kwa mwandishi wa StarTV, BBC, TBC vile vile si sawa kwa utingo wa dala dala wala mfagizi ofisini.
Ila tujiulize, kwa nini TBC na sio chombo kingine cha habari?
Bila ushabiki wowote, TBC imekuwa ikitumika vibaya na watawala kutimiza matakwa yao.
Utakumbuka wakati wa uzinduzi wa kampeni za CDM pale Jangwani 2010 baada ya Marando kumtaja BWM na kashfa zake eti signal zikawa hazishiki vizuri. Marin Hassan alinusuriwa na viongozi wa CDM na polisi, na kwa hakika siku ile uharibifu wa mali na maisha ungeweza kutokea.
Mkaanzisha kipindi kizuri cha Mchakato Majimboni. Mkatishiwa sana na CCM na mwishowe kipindi kikapwaya kwa sababu mlidhibiti sana wauliza maswali.
Bado tunakumbuka sanaa ya maigizo iliyofanya na Tido Mhando kwa Kikwete.. Sijawahi kumsikia na kumuona Tido akiedesha mahojiano dhaifu kama kipindi kile.
Baadae Tido alichinjiwa baharini kwa madai kwamba zaidi ya 50% ya majimbo ambayo programu ya mchakato majimboni ilifika yalikwenda kwa upinzani.
Sote tuna kumbukumbu jinsi TBC inavyoripoti vipindi vya bunge kibaguzi. Siku Dr. Slaa (akiwa MB) akihutubia TBC ilichakachachua kama ambavyo huendelea kufanya kwa bunge hili wabunge machachari wanapoongea.
Sasa "baadhi ya wahuni wa Arusha" ni walipa kodi wa nchi hii, na TBC ni mali yao sawa na mali zao nyingine zozote. Ile ilipaswa kuwa salamu tosha (sanduku la maoni la kisiasa).
Suluhu si kutafuta mchawi ila kufanya tathmini ya dhati juu ya uendeshaji wa TBC. Kuna weledi na uadilifu wa kiasi gani? Tuazime dhana ya wanasheria kwamba "si tu haki itendeke ila ionekane kutendeka" ama dhana ya wahasibu "si tu mkaguzi anapaswa kuwa huru ila aonekane yuko huru"
Na msiniite mnajimu siku TBC wakifanyiwa shambulio hatari na "baadhi ya wahuni" litakalopelekea uharibifu mkubwa wa mali, na bila kukutisha kifo.
Kule #twitter kuna kampeni inaitwa #occupytbc ifuatiliye tafadhali

ahaa, unataka nikae kimya watu wanapotoa comments za kipuuzi? Hakuna mwenye hati miliki ya kujiona yeye ni bora zaidi ya wengine, kuna watu humu wanafikiri wote tunaichukia CCM, am sorry to disappoint you guys, i have never hate any political party kwanza vyama vingi wapo marafiki zangu wa karibu, sasa iweje leo nikitofautiana kimtazamo iwe kosa machoni kwa wengine?
 
Dotto Athumani -Nadhani research yako kama ulikuwa unafanya purposive utakuwa umepata majibu kulingana na response hii kutoka kwa vijana wa Chadema hapa

Sasa tupe tafsiri yako juu ya ''Mhuni'' ili tuweze kufanya tathmini na sisi hapa. Maake mtu anaweza kufanya research kwa kutumia hypothesis testing ili kuthibitisha wazo lake kama ni sahihi ama si sahihi kupitia JF.
 
Ivi nawe ni mwandishi wa habari kumbe.
Kanjanja hili Mkapa alikuwa hayapendi makanjanja kama hili.
 
Kama watu wa Ar ni wahuni kwa sababu wamewazuia waandishi wa tbb,basi tbc ndio wahuni zaidi kwa kubagua habari za watz kwa makusudi.
 
Ni ukweli kwamba TBC wamefungwa breaks na wanasiasa kiasi kwamba wanachotangaza hakiwaridhishi watu wengi bila kujali itikadi za kisiasa. Wamepotoka kimaadili kiasi kwamba wanaonyesha mambo hayastahili kuonyeshwa na Television ya taifa.
Habari zao nyingi zinaegemea upande fulani na wanasahau kuwa wanaendesha shughuli zao kwa kodi za wananchi wote. TBC mkitaka msemwe vizuri tangazeni mambo yanayowahusu wananchi wote wa tz na si kubagua. Msiogope yaliyomkuta Mkurugenzi wa zamani - Mhando.
Hata hivyo kitendo cha kuwazuia kufanya kazi zao mahali po pote si cha haki na si uungwana kufanya hivyo.
CDM nayo isiendekeze wapenzi na wanachama wa aina hii kwani wanaleta picha mbaya machoni mwa watu makini.
 
I did not expect positive reaction hasa kama wanatoa watu waliojificha nyuma ya avatars...lazima mjue kuwa CCM inawachama zaidi ya milioni tano, hatuwezi kuwapuuza eti kwa sababu watu fulani wanajihisi wako sahihi kupita wengine. Wewe umenithibitishia kuwa "Mhuni mmoja wapo"

ripota wa kigoma. Ngoja nifuatilie ujinga wako
 
JAMANI Hebu twende taratibu Dotto Athumani naomba unisahihishe nitakapokuwa nimekosea. TBC ni chombo cha umma kinachoendeshwa na kodi za WATANZANIA, Is that Right?

Wenye Chombo wamesema kwamba hawataki mchukue habari kwasababu mnawaletea habari zilizochachulia?

Je unapata wapi moral authority ya kuwaita wenye chombo wahuni?

Kama malengo ya TBC ni kuengemea CCM kwanini msijitoe TBC na mkaanzisha TVCCM na habari zenu zikawa BIASEd towards CCM kama lilivyo UHURU na hiyo TVCCM ikaendeshwa kwa kodi za wana-CCM tu? Huoni huo mnaofanya ni UFISADI mwingine kama wa EPA, Richmond, Deep green etc

Ungekuwa mwandishi makini na sio KANJANJA angefanya utafiti mdogo kulikoni wenye chombo wakikataze chombo chao kuwaletea habari? Then from there ungeweza kujua chanzo cha tatizo na huo utakuwa mwanzo mzuri wa ku-solve tatizo.
 
Sasa tuelewane vizuri mnataka tubadilishe hii thread iwe ya kutukanana? Mbona mnakosa uvumilivu wandugu, tuzungumze hoja, nimesema si jambo la busara kuwazuia waandishi kufanya kazi yao kwa kigezo cha kutoa ripoti isiyo wapendezesha upande wenu...sasa matusi yanatoka wapi? Neno uhuni ni la kawaida sana sidhani kama linaweza kuwaumiza kiasi mshindwe kuiona mada ya msingi....Punguzeni jazba THINKERS!
 
Dotto akili zote umemwachia kurwa...
Na akili chache ulizobaki nazo ni za kuendea chooni
 
we ndio muhuni usiyejua wahuni! maana mmezoea kuandika habari za kutetea magamba wenzenu! na wewe umetumwa na waandishi wenzio!
 
Sijakusoma kabisa mkuu, unataka kuniambia siruhusiwe kutoa maoni yangu? Kama hakuna "formal complaits" kutoka uongozi wa CDM basi madai yenu mengi ni ya kishabiki. Na kama hamridhishwi na namna TBC inavyoripoti habari basi njia ya kuwazuia kabisa si sahihi.

tuna uhuru huo. Kodi yetu lazima iheshimiwe. Mbona hatukosoi gazeti la uhuru?
 
Back
Top Bottom