#COVID19 Maoni yangu binafsi kuhusu mkopo wa Trilioni 1.3 ya COVID-19

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Jana kwenye taarifa ya habari tulihabarishwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania imepokea mkopo wa 1.3 trillioni ili kupambana na ugonjwa hatari ya Covid-19.

Binafsi sisemi au sikatai mkopo huu ila nasema fedha hizi ni nyingi sana kwa ajili ya mkopo.

Kama juzi juzi tulipokea dozi millioni moja na hazijaisha kwa ajili ya uchanjaji kwa nini nchi inachukua mkopo mkubwa kama huo?.

Kama nchi tunayo matatizo mengi tungekopa fedha tukaelekeza kwenye maeneo yenye matatizo kuliko kukopa fedha nyingi kama ilivyotajwa na huku watu wengi hawataki kuchanjwa.

Kwa hili namkumbuka sana Mhe. Magufuli asingekubali jambo kama hili.

Haya ni maoni yangu binafsi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom